Aaaah wee, huo mchepuko ulikifuata nyumbani kwako, ukafunua hotpot ukakuwekea limbwata? Si umeufuata mwenyewe huko nje? Tukiwaambia tulieni na wake zenu, mnadai ooh sisi kuwa na wanawake wengi ni asili yetu. Me kalichume tu janga huko nje, utalila na kulitafuna peke ako. Na wengine hakuna cha limbwata wala nini, ulimbukeni wao tu
Hata kama ilitokea sababu yoyote mkajikuta kwenye ndoa bila kutegemea, basi ikubali tu hiyo ndoa yako iboreshe, itunze na utaifurahia, otherwise usimuoe mtu kama unajua utampa tu mateso. Na wengine wanaoa kwa mapenzi yao, ila baadaye ndo utasikia "wewe sio hadhi yangu", nenda kwa wenye hadhi yako basi, ila omba usije ukarudi kwangu tu. Afu mwingine kisa hampendi tena mke, ndo na watoto hawajali tena, inahusu nini