Ushauri: Mke kamalizia kulipa gharama ya kiwanja ambacho mume wake alikuwa anamnunulia mchepuko

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,326
98,594
Wakuu

MDA SI mrefu nmetoka kupigiwa Simu na rafiki yangu mmoja wa karibu Sana Ni DOKTA hospital moja ya wahindi hapa mjini,Na anamiliki duka moja la dawa za binadamu kubwa Kiasi ambalo suka ilo mkewe ndo muuzaji na msimamizi mkuu wa kila mara. Sasa Jamaa kapigia akinipa taarifa nzito sana khs jambo moja.

Ni kwamba
kile kiwanja nilichosaini Kama shahidi wake kwa ajili ya manunuzi na kumjengea mchepuko wake nyumba tayar kaenda MKE wake na mil 2 cash pesa ilobaki ili kukimalizia kabisa.

Ni Hivi wakuu,
Katika harakati za hapa na pale, jamaa yangu uyu nilimshaur Bora amjengee TU mchepuko wake maana Kodi anakokaa anayomlipia kubwa Sana na inamuumiza (double ya nnayomlipia mchepuko wangu mimi).Jamaa kweli akakubali.

Kiwanja kimetafutwa kimepatikana na maafikiano yamefikiwa kilipiwe pesa mil. 8 cash ila iwe ni kwa installment 3 ndani ya miez 3 tu.
Yaani January tulipoenda wote kililipiwa mil 3 cash- Tukasainishana awamu ya kwanza tukaondoka.

February, - Jamaa akamuingizia TU mzee Ela mil.3 kwenye bank. Akanipa taarifa tu ila Hatukwenda kule saiti kusaini. Mzee akasema tutakuja kusainishana mwishoni kabisa tukimaliza biashara.

Jana anasema kapigiwa na mzee mwenye kiwanja kwamba mkataba uko tayar Mbona haji wakakabidhiane na viongozi wa serikali. Kila Siku anapiga kalenda.

Jamaa akajitetea mzee amvumilie kwanza mpk amalizane na TRA tar 30 March kwenye maswala ya Kodi ya mapato. Mzee akamjibu kwamba mbona ela iliyobaki tayar ishalipwa, ililetwa na mama (yaani mkewe).

Mzee Anasema Kuna mmama alimpigia akijitambulisha kwamba mme wake DOKTA flani kampa maelekezo pesa ilobaki mil.2 cash aje aimalizie, sasa wakutane wapi akabidhiwe?

Mzee kamjibu kwamba wakutane saiti maana Hakua mbali na pale. Akasema mama mwnyw alikuja na gari yake ile ile jamaa aliyokuja nayo siku ya mwanzo pale saiti kwake Akiwa Yuko na mtoto mdogo na binti mmoja kafunga nywele kwa juu kuja kumalizia Ela.

Na kuondoka zake kwamba mkataba watakuja jumapili ijayo.Jumapili imefika hawajaja Ndo ikabd ampigie jamaa. Sasa Jamaa akasema kwa maelezo yake akahisi labda mzee yule anamjaribu. Ila Kama ni gari Huenda iwe imetumika wikendi TU maana ndo humuachia mkewe apeleke Watoto wake kanisani, yeye ubaki nyumbani kupumzika.

Sasa Leo jion kaenda kumhoji binti wa kazi kama Kuna sehem yoyote alienda na mama ake, binti kweli kakiri Kuna mahali jumapili moja walienda na mama ake baada ya kutoka misa nje ya mji kidg.

Ila yeye alibaki kwenye gari mama akaenda kuongea na wazee flani, baadae mzee mmoja akawa anamsindikiza mpk kwny Gari wakasalimiana ila yeye akujua walienda kufanya Nini kule Maana mama akumwambia kilichompeleka mpk wanarudi.

Sasa Jamaa kachanganyikiwa apa kaniomba ushaur afanyeje kulimaliza hili.Nmemwambia nipe muda nitafakari Kwanza tunafanyaje.

Kiukweli
Mimi mwnyw hata Cha kumshaur sahii Ni kipi nmekosa.

Maana Kama kweli yule MAMA alijua nilikua shahidi tayar nishajijengea chuki kwamba nmehusika kwenye dhambi ya mmewe. Mimi na mmewe Ni wale wale.

Afu kibaya zaidi Mimi Ndo huwa msuluhishi wao kila Mara pale wanapogombana, shemej huja kushtakia kwangu Nawasuluhisha.

Sasa kwahili nashangaa shemej yangu hajaja kunambia chochote.

Yaan Shemej yangu uyu huwa ananiamini Sana kias kwamba ata jamaa akienda kwenye Mambo yake akimwambia TU kua Yuko namimi, mkewe anakua na amani KABISA mmewe Yuko sehem salama.

Kwenye ugomvi shemej anamshaur kila mara kufuata nyayo zangu jins nilivotulia na familia yangu bila mambo mengi ya michepuko michepuko.

Sasa
Nishaurini vema niweze kumshaur vizur uyu jamaa yangu ili kuokoa ndoa yake.

Pili nishaurini namuingia vipi uyu shemej yang Kama kweli akija kujua nmehusika kwny kile kiwanja kwenye dhambi ya mmewe. Napangua vipi mapigo.

NAWASILISHA
 
Hahahahah ya leo kali!

Ina maana shemeji yako alishasanukia mchongo ila kaamua akamalize show kibingwa. Sasa hapo mtachagua kusuka au kunyoa maana hamna jinsi zaidi ya kupiga kimya ni kumfata mwenye kiwanja na kumchana live tu kuwa show ishakuwa kali.

Wife kalipia kiwanja cha mchepuko so wa assume tu kuwa hakuna kilichotokea wampe documaa shemeji yako. Ila kimsingi wote mshaonekana mafala tu.😅 Kaukeni hapo haina bobo!

Mwambie jamaa yako awe makini na simu yake na awe mtu wa kufuta meseji kila wakati. 100% meseji ndio zimemponza...Mie baada ya kugundua sms zinanichomaga mara nyingi nimetia pini whatsapp. Mama akishika simu anaombaga aangalie picha kisha anapekua pekua call logs na whatsapp.
 
Wakuu
MDA SI mrefu nmetoka kupigiwa Simu na rafiki yangu mmoja wa karibu Sana Ni DOKTA hospital moja ya wahindi hapa mjini,Na anamiliki duka moja la dawa za binadamu kubwa Kiasi ambalo suka ilo mkewe ndo muuzaji na msimamizi mkuu wa kila mara.
Sasa Jamaa kapigia akinipa taarifa nzito sana khs jambo moja.

Kwanza wewe na huyo jamaa mnatia aibu, mwanamke anawazidi vipi kwenye mbinu za kijasusi?

Inawezekana mwanamke hajui kiwanja ni cha mchepuko, unless tume establish chanzo cha taarifa.

Mwambie apige kimya hivyo hivyo, asijiguse na wakati wa mkataba aende na mke wake kimya kimya undava undava, bila kujitetea.

Mchepuko wamezaa naye? Kama sio mjue mnazingua, hakuna faida yeyote kwa mchepuko, zaidi ya matatizo tu, na uwajibikaji kama atakuwa na mtoto wenu.
 
Wakuu
MDA SI mrefu nmetoka kupigiwa Simu na rafiki yangu mmoja wa karibu Sana Ni DOKTA hospital moja ya wahindi hapa mjini,Na anamiliki duka moja la dawa za binadamu kubwa Kiasi ambalo suka ilo mkewe ndo muuzaji na msimamizi mkuu wa kila mara.
Sasa Jamaa kapigia akinipa taarifa nzito sana khs jambo moja.
Duh!
Kwa kuwa mke hakukamilisha uandikaji wa mkataba wa mauziano, jamaa akaandikishe tu umiliki wa familia ( yy na mke), afu ajipange upya kumtafutia kwingine huyo mchepuko kama ataendelea naye.

Seems huyo wife anajua mengi juu ya mmewe na mchepuko kuliko mnavyofikiria!

Labda kafanya 'hacking' anapokea mawasiliano yoote mfululizo - wasap, sms, calls.. so anajua kila kitu!

Na kama ni hivyo, huyo jamaa yako itabidi tu ampe huyo mchepuko mafao ya maana (terminal benefits) afu aachane naye mazima ili kuokoa ndoa yake, au km dini yake inaruhusu, amuoe😊
 
Hahahahah ya leo kali!

Ina maana shemeji yako alishasanukia mchongo ila kaamua akamalize show kibingwa. Sasa hapo mtachagua kusuka au kunyoa maana hamna jinsi zaidi ya kupiga kimya ni kumfata mwenye kiwanja na kumchana live tu kuwa show ishakuwa kali.

Wife kalipia kiwanja cha mchepuko so wa assume tu kuwa hakuna kilichotokea wampe documaa shemeji yako. Ila kimsingi wote mshaonekana mafala tu. Kaukeni hapo haina bobo!

Mwambie jamaa yako awe makini na simu yake na awe mtu wa kufuta meseji kila wakati. 100% meseji ndio zimemponza...Mie baada ya kugundua sms zinanichomaga mara nyingi nimetia pini whatsapp. Mama akishika simu anaombaga aangalie picha kisha anapekua pekua call logs na whatsapp.
Tabu zote za nini ndugu

Kiukweli nimechelewa sana kutoelewa raha ya uaminifu kwenye ndoa ya wawili tu(Me + Ke).

Hakuna mapepo/ulinzi wa uhakika kiroho.

Hakuna mawazo yasiyo na ulazima/hakuna kuzeeka kizembe.

Hakuna wasiwasi wa kujistukia hata simu yako ikiwa haina neno siri (miaka mitano bila ya neno siri).

Hakuna pasua kichwa kuhangaikia Ke mwingine na watoto wa nnje zaidi ya Ke halali wa ndoa yangu tu, familia ya nyumbani kwetu na mara 1 1 ukweni.

Uchumi umeimarika na kuhifadhiwa kwa zaidi ya 90%.

Kuaminiwa na Ke hata nikienda popote pale duniani na kukaa mbali naye hata kwa zaidi ya siku, mwezi, mwaka na kuendelea.

Baraka za Mungu ni nyingi sana hadi nashindwa kuzielezea hapa.

Wakuu kama hamuelewi maana halisi ya amani rohoni basi onjeni mfumo wa uaminifu katika ndoa ili mshuhudie raha ya kipekee sana
 
Ni nzuri kama unamke wa kipwani full kukupa mchezo enjoyable bila kelele kama hawa wanawake wa kibara. Wengine wake wasumbufu mtu unataka mchezo unapangiwa ratiba kama vile shirikisho la mpira.

Tunatafta michepuko sio kwa kuwa hatupendi uaminifu ila sababu inaboa kulazimisha sex na kugonga demu kama maiti hamna emotional connection during sex.

Wake wengi wana kero za uvivu wa kutoa penzi so unatafta sub tu anaekupa game kila saa unavyotaka wewe.
 
Mwenyekiti wa vijana ana misala mingi sana aiseee halafu vyote huwa ni majanga sana , ivi hizo ela huwa hamna ndugu zenu wenye uhitaji nazo kbsa, halafu washikaji mnafanya movements za kishamba sana sasa cha kufanya we tulia tu ili kulinda heshima yako itakuwa vizuri kama huyo shemeji yako hakusoma na kupewa document zote japo ninahisi kama chai vile
 
• Chukueni million 6 yenu. Ataamua ama arudishiwe million 2 yake ama aongezee iliyobaki anunue kiwanja

• Saini mkataba then muuze kiwanja kwa kupata bei kubwa zaidi.

• Badilisheni mkataba wa mnunuzi uonekane wewe ndio mnunuzi na rafiki yako awe shahidi halafu wewe umrudishie hiyo pesa shem.

• Mwachieni kiwanja mzee mama na mkubali mmepoteza hii match, mjipange zaidi. Hapa rafiki yako akubali amenunua kimyakimya sababu alitaka kum-surprise.

• Muhimu kuliko yote: tafuteni chanzo chake cha taarifa.
 
Unachepuka hadi unajengea hawara nyumba, bure kabisaaaa
Si akili zao ndugu, Suleiman mwenyewe alimuasi Mungu kwa michepuko 1000.

Daudi alianguka kiimani sababu ya kuchepuka na mke wa Mtu, na Mtoto aliyezaa na Mke wa Mtu(Bethsheba) alikufa toka kwa ahadi ya Mungu kuwa "hakika Mtoto atakufa"

Bado tena Mtoto wa Daudi(Absalom) aliendelea kuwa adhabu kwa Daudi baada ya Absalom kumuasi Baba yake mzazi(Daudi) alipomuwinda kumpindua na baadhi ya Askari akitaka ufalme kisha Daudi alikimbia na Absalom alizini na Ke(Michepuko) ya Baba yake Daudi.

Asiyejua athari za michepuko ni wa kumpatia pole na kumwombea apone katika huo utumwa.

Michepuko ndiyo kwa asilimia kubwa huhangaika na Waganga wa kienyeji kwa namna yoyote ile ili kumpindua Mke halali katika ndoa.

Huu ujasiri si wa Mke wa ndoa bali ni michepuko ndiyo hufanya hivi
View attachment 2163618View attachment 2163619
 
Ni nzuri kama unamke wa kipwani full kukupa mchezo enjoyable bila kelele kama hawa wanawake wa kibara. Wengine wake wasumbufu mtu unataka mchezo unapangiwa ratiba kama vile shirikisho la mpira.

Tunatafta michepuko sio kwa kuwa hatupendi uaminifu ila sababu inaboa kulazimisha sex na kugonga demu kama maiti hamna emotional connection during sex. Wake wengi wana kero za uvivu wa kutoa penzi so unatafta sub tu anaekupa game kila saa unavyotaka wewe.
Poleni sana wakuu kwa kupata Ke pasua kichwa.

Basi Mungu ashukuriwe kwa kutujalia sisi Me wengine Ke wanaojielewa.
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom