Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,075
Hata mimi nimemshangaa leo, Mwanasheria mkuu, ambaye kwa taaluma yake ile nyingine ya 'professional boxer' amekuwa mpole kiasi cha kuwakumbusha na kuwasihi ukawa kuwa wanasali kanisa moja, kwa hiyo wakumbuke maandiko ya vitabu vya dini, vinavyosema sameheni mara 7 mara 70!Mpaka anambembeza hivyo kawa mpole. Mpaka anawakumbushia kwamba wanasali wote so what.
Huyo 'bondia' ambaye siku zote yeyote anayetofautiana naye mawazo, huwa anatishia kumpiga, amekuwa mpole vile, kiasi cha kuwasihi sana ukawa warudi bungemi, kwa kuwa bila wao hakuna katiba mpya!
Sasa tunasubiri kwa hamu kauli za kina Wassira, Lukuvi na Nape Nnauye, ambao walitamba sana siku za nyuma kuwa, kuwa kutoka kwa ukawa bungeni siyo issue kabisa, kwa kuwa idadi ya wabunge waliobaki kwenye BMK, inatosha kabisa kuandika katiba mpya!
Kwa bahati nzuri, kada wao mwingine Mwigulu Nchemba, alifunuliwa mapema maono na Mungu, kuwa idadi ile ya wabunge iliyopo bungeni, haiwezeshi kupatikana kwa 2/3 inayotakiwa kwa pande zote 2, za Tanganyika na Zanzibar, ile katiba ipite, lakini wakampuuza!