Mwanasheria mkuu wa Serikali, Werema aungana na UKAWA

Mwanasheria mkuu wa Serikali, Werema aungana na UKAWA

Hivi kuna kazi gani six kusema rudini na tuijadili rasimu ya iliyotoka kwa wananchi ili ukawa warudi mbona ni kazi kidogo
 
Mdogo mdogo Sitta ameingizwa kingi na wenzake kutokomezwa katika siasa , na ndiyo kwisha habari yake.
 
Nilikuwa napitia magazeti ya leo kuhusu mkutano wa Werema na waandishi wa habari uliofanyika jana.

Gazeti la The Guardian limeandika kwamba "The government intends to convene an emergency meeting of the Union legislature to review and amend some sections in the Constitutional Review Act, if the Constituent Assembly (CA) will be short of the needed 2/3 quorum to endorse a newly crafted constitution draft". Tafsiri ya kilichoandikwa hapa ni kwamba endapo BMK litashindwa kupata theluthi mbili zinazohitajika kutoka kila upande wa muungano ili kupitisha Rasimu ya katiba, Bunge la Muungano litaitishwa ili kufanya mabadiliko kadhaa katiba sheria ya mabadiliko ya katiba.

Mabadiliko haya yatafanyika ili kuliwezesha BMK kupitisha rasimu bila UKAWA kuwepo. Kwa mfano kipengele cha 2/3 ya kura za kila upande kinaweza kubadilishwa ili hiyo 2/3 iwe based on wajumbe walio bungeni wakati wa kupiga kura na si kwa wajumbe wote wa BMK.

Lakini gazeti la Nipashe limeandika kwamba endapo hiyo 2/3 haitapatikana, serikali itaitisha Bunge la Jamhuri ya Muungano na kufanya marekebisho ya baadhi ya vifungu vya katiba ya 1977 k.m Tume ya Uchaguzi (NEC), suala la mgombea binafsi, madaraka ya Rais, N.K. Kwa hiyo hapa kile kitakachobadilishwa ni katiba ya 1977 na siyo sheria ya mabadilikio ya katiba.

Swali langu ni kwamba ni kipi alikisema AG?

Je ni kile kilichoandikwa na The Guardian au Nipashe?
 
Nafikiri version ya The Guardian ndiyo sahihi kwani Werema alikusudia kutisha na sio kuonyesha kushindwa kwa BMK!
 
Mkuu nipashe wako sahihi. Nimemsikia mwizi akisema hivyo kwa masikio yangu. Labda km aliongea chumbani kwake na hao guardian.
 
Nilikuwa napitia magazeti ya leo kuhusu mkutano wa Werema na waandishi wa habari uliofanyika jana.

Gazeti la The Guardian limeandika kwamba "The government intends to convene an emergency meeting of the Union legislature to review and amend some sections in the Constitutional Review Act, if the Constituent Assembly (CA) will be short of the needed 2/3 quorum to endorse a newly crafted constitution draft". Tafsiri ya kilichoandikwa hapa ni kwamba endapo BMK litashindwa kupata theluthi mbili zinazohitajika kutoka kila upande wa muungano ili kupitisha Rasimu ya katiba, Bunge la Muungano litaitishwa ili kufanya mabadiliko kadhaa katiba sheria ya mabadiliko ya katiba.

Mabadiliko haya yatafanyika ili kuliwezesha BMK kupitisha rasimu bila UKAWA kuwepo. Kwa mfano kipengele cha 2/3 ya kura za kila upande kinaweza kubadilishwa ili hiyo 2/3 iwe based on wajumbe walio bungeni wakati wa kupiga kura na si kwa wajumbe wote wa BMK.

Lakini gazeti la Nipashe limeandika kwamba endapo hiyo 2/3 haitapatikana, serikali itaitisha Bunge la Jamhuri ya Muungano na kufanya marekebisho ya baadhi ya vifungu vya katiba ya 1977 k.m Tume ya Uchaguzi (NEC), suala la mgombea binafsi, madaraka ya Rais, N.K. Kwa hiyo hapa kile kitakachobadilishwa ni katiba ya 1977 na siyo sheria ya mabadilikio ya katiba.

Swali langu ni kwamba ni kipi alikisema AG?

Je ni kile kilichoandikwa na The Guardian au Nipashe?
Pengine ni matatizo ya lugha. Kilichosemwa kwa usahihi katika hili ni kile kilichoandikwa na Nipashe. Rasimu ikishindwa kupata theluthi mbili kutoka pande zote za muungano inakufa hapo hapo na kinachofuata kwa mujibu wa AG ni kuitishwa kwa dharura Bunge la JMT ili kufanya marekebisho kwenye Katiba tuliyonayo. AG alikwenda mbali na kuainisha hata maeneo yatakayobadilishwa ikiwemo Tume ya Uchaguzi, madaraka ya Rais, mbunge binafsi n.k., mambo ambayo hauwezi kuyakuta kwenye sheria iliyosemwa na the Guardian!
 
ccm wana macho lakini hayaoni,wanachoangalia hapo ni posho sio katiba,wananchi wakiikataa au isipopatikana theluthi mbili kwao sio kitu,ndio maana wamebadilisha kanuni ili kura ipigwe siku ya mwisho wakiwa tayari wamekusanya posho zao. watu wenye akili hili waliliona mapema lakini wana ccm wamejitoa fahamu

Wadau kinachosumbua hapo si ukweli,hekima wala busara za baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba bali ni posho. Mle ndani mna werevu wengi na hata kuona wakianza kuzipigia kura kupitisha sura ya kwanza na ya sita kujua muelekeo wa sura 15 zinazofuata na kushindwa kupata theluthi mbili zinazotakiwa kisheria watakwama tena na kukosa posho. Hivyo njia ni kuvijadili vyote kwa ujumla wake ikifuatiwa na kuvitafutia theluthi mbili za pande zote mwishoni. Ikishindikana kupata hizo theluthi iwe hasara ya wananchi ila posho yao yote wanayo.Imani iliyomwaminisha spika na hata baadhi ya viongozi wenye dhamana waliopo kwenye bunge hilo ni takwimu zifuatazo. Idadi ya wajumbe Zanzibar ni 217. Wliosusa bunge ni 69. Waliobaki ni 148. Theluthi mbili yao ni 145. Wajumbe wa bara ni 412.Waliosusia bunge 57. Waliobakia bungeni ni 356.Theluthi mbili yao ni 275. Najua wapo wachache sana kwa pande zote walirudi bungeni baadae.Sasa kwa takwimu hizo wakajiridhisha theluthi mbili za kila upande zipo hata kama Ukawa wasiporudi bunge maalumu.Hapo ndipo walipojidanganya na kujiaminisha tofauti. Theluthi ya wajumbe wa bara itapatikana kirahisi kwani ni wao kwa wao.Theluthi ya upande wa wajumbe wa visiwani haitapatikana hata kqmq wameshiriki toka kwenye kamati. Ujue linapokuja suala la maslahi ya Zanzibar wanaungana wote bila kujali itikadi zao.Hata kama watazipata theluthi za pande zote bunngeni rasimu ikienda kwa wananchi kupigiwa kura Zanzibar haipiti. Mwisho mwana sheria wa serikali asijidanganye kuwa bunge la muungano likikaa na kurekebisha baadhi ya vifungu kwenye katiba iliyopo itawafanya wajumbe wa bunge maalumu kuipitisha rasimu au wajumbe wa ukawa kuridhia. Wanachotaka ni kuiona serikali ya Tanganyika ikisimama na kujitengenezea katiba yake.Hapo ndipo ninapowasifu wanasiasa vijana wenye maono kama Mwigulu na yule mjumbe wa bunge hilo mwenye umri mdogo kuliko wote kwa kuuona ukweli huu mapema na kutoa tahadhari.
 
theluthi 2 ya 3 kwenye hesabu ni (2/3)x 3= 2. hariri na kusema theluthi 2 ukimaanisha 2/3 na sio kama inavosomeka.
 
Jamani hapa muokoz pekee wa hili jahaz la katiba ni Rais wa muungano. coz yeye ndio mwenye mamlaka pekee ya decree of power. tusisubir maafa wao ccm wanachukulia poa but wajue kua huu si uchaguzi wala ushindi ila ni misingi ya nchi imara iweze kusimamishaa Taifa letu.

Nakuomba muheshimiwa wangu Rais wengi tunaijua iliokua zamira yako kwa watanzania ni kutuletea uhuru wakatiba japo wenzio wa juu wa halmashairi wamekutelekeza ukakosa msimamo lakini muheshimiwa kumbuka taifa lipo ndani ya dhamana yako tumevuka salama pongezi ni zako hatopongezwa mwingine na kinyume chake tumejikwaa mzigo ni wako na hao unaowaendekeza leo keshoo watakulizaa.

Jikumbushie tu kwa historia ya mda mfupi znz . Rais mstaafu Mh Amani Abeid karume kafanya anayoyapenda yeye mda mwingi lakin hakuchelea karibia na kumaliza mda wake kajitathmini kwa aliyoyafanya akajua lazima akiondoka jamii itamsuta kw ujanja na umakini na kujisafisha na kwa kuieka jamii sawa ametuletea kile wazanzibar tulichokipoteza mda mrefu . kuondosha mpasuko wa kisiasa znz kw kuweka maridhiano jambo ambalo watendaji wake wa ccm walilipinga na kulitolea hoja nyingi but kw vile anajua mamlaka alonayo (decree of power) japo walimtukana na kumdhalilisha but hakuyumba alisimama kiume kuhakikisha anaweka sawa taifa japo serikal ya muungano iliionyeshs eazi kuibeza znz na kusema ZNZ sio nchi hivyo aliliamuru baraza lakutunga sheria znz kufanyiwa mabadiliko makubwa ya kikatiba ilioipa nguvu nchi ya znz ambapo inekua kikwazo kw ccm waleo kuweza kuichakachua mpk kwa ridhaa ya wazanzibar wenyewe pamoja na kuwaweka p1 wa znz wote kw kuundwa kwa kamati ya maridhiano ambayo zanzibar ilikua kama ndoto. Hivyo tunanpenda na kumheshimu Rais wetu huyu ambapo imepelekea kufanya uchaguzi mkuu 2010 kw njia za aman bila kumwaga damu ambayo ni tofaut kw miaka iliyopitaa.

Nawe baba etu wa taifa Rais wetu mpendw hujacherewa usiogope wananch tupo imara na tunaona jitihada zako so keep it up utafikaa tu salaama tunakuombea.

lakini kuna msemo unasema ukitaka kumla nyani usimiangalie usonii

Karime namba ingine.wa kwetu hawezi
 
Acheni Filamu iendelee! Hii nchi kwa sasa inajiendesha tu (auto pilot). Rubani hayupo tena, wala hajali nini kinatokea kwenye usukani! Rubani yuko USA anachezea farasi wa Bush. Akitoka huko anapita Brazil kwenye zile bembea za kitalii, halafu anaenda Qatar kupumzika! Akirudi atapita Switzerland kuangalia account yake, atachepukia Uingereza kuomba msaada wa mwisho mwisho halafu ndo anarudi kumalizia siku zake za utawala!
 
Hivi huko mbele ya safari haiwezekani Mr Six kushtakiwa kwa uhalifu huu anaofanya hivi sasa?

unadhani sitta anayafanya hayo kwa maamuz yake binafsi? la hasha....sitta anafuata maelekezo ya CC ya CCM
 
Kamanda Lissu hakikisha Ukawa mnasimamia tuliyowatuma vizuri sisi wananchi,pasipo kusimamia rasmu ya Tume ya jaji Warioba na hiyo ikajadiliwa kwa mfumo wa serikali3 kamwe msirudi Dodoma
 
Watu wenye akili finyu wanashindwa kutambua kuwa UKAWA si lolote , si chochote.
Mambo yote ni Rasimu ya Katiba, na hiyo ilitengenezwa na wataalam wa sheria wakiongozwa na Jaji Warioba.

Sheria ya katiba haijatengenezwa na warioba na tume yake acha kuwa kilaza. Habari za theluthi mbili bara na visiwani ni matokeo ya sheria iliyopitishwa na bunge. Kama ukawa sio lolote basi chukueni ukoo wenu wenye akili nyingi mjipe uwakilishi toka visiwani mtimie theluthi mbili mpitishe katiba.
 
Back
Top Bottom