Mwanasheria mkuu wa Serikali, Werema aungana na UKAWA

Mwanasheria mkuu wa Serikali, Werema aungana na UKAWA

Kumbe hata Werema analijua hili, kwamba bila kile "kikundi haramu" al maarufu UKAWA hakuna katiba mpya. Cha kujiuliza kama hili linajulikana kwa nini mapesa chungu nzima yanapotezwa kila siku kwa kulipwa kama posho huku ikijulikana fika hakutakuwa na katiba mpya bila UKAWA? Ni nani ndani ya MACCM mwenye mamlaka ya kusitisha Bunge la Posho kama Kikwete hana mamlaka hayo!? Ni werema, ni Migiro, ni Sitta au ni Kificho!?
 
.we highly need reconciliation between the conflicting parties otherwise we will not get a new constitution
 
Wanataka kurudi kwenye bunge la kawaida ambalo lina wana CCM wengi wawanyonge wananchi??
 
Werema kaamua kuwaambia indirecrly ccm wasitishe BMK, anaogopa kuwaambia directly. Sikumbuki kama imewahi tokea b4 mwanasheria mkuu kufanya press conference, ni kwamba anaogopa kumwambia mfalme kuwa yuko uchi kwa hakika anaogopa lawama kuwa wananchi watasema pesa imepotea bure, mwanasheria hakuwashauri watoa maamuzi juu ya theluthi 2 za Zanzibar haziwezi kupatikana and so Bunge liahirishwe ili kutafuta maridhiano kwanza. Anapowaomba UKAWA warudi nafikiri anafanya utani, Kikubwa ni kuwa anapeleka meseji kwa watoa uamuzi kwamba bunge liahirishwe na take note that ameamua kusema baada ya kauli ya ikulu kuwa katiba itapatikana hata bila UKAWA.
 
CCM wameanza kunena lugha wasiolewana mithili ya wajenzi wa mnara wa babeli.

Maskini Sitta.
 
Kumbe hata Werema analijua hili, kwamba bila kile "kikundi haramu" al maarufu UKAWA hakuna katiba mpya. Cha kujiuliza kama hili linajulikana kwa nini mapesa chungu nzima yanapotezwa kila siku kwa kulipwa kama posho huku ikijulikana fika hakutakuwa na katiba mpya bila UKAWA? Ni nani ndani ya MACCM mwenye mamlaka ya kusitisha Bunge la Posho kama Kikwete hana mamlaka hayo!? Ni werema, ni Migiro, ni Sitta au ni Kificho!?
Hivi sasa timu nzima ya magamba, ni full kuweweseka.

Kwa kuwa game ishafika dakika ya 88, na hadi sasa scoring board inasoma UKAWA 3 CCM 0

Kwa matokeo hayo, ni dhahiri hiyo game, magamba wamepoteza mechi!
 
Kama uliwasikiliza vizuri Wasiraa, Lukuvi, Sita na tamko la ikulu utangundua wazi wanachokitafuta si kheri ya nchi hii. Wamejipenda na kupenda ccm yao kupindukia. Lukuvi anasema ' ukawa ni wachache hawawezi kuwa na hathari isipokuwa kutokuwepo kwao tu bmk na katiba mpya itapatikana'! Huyu jamaa ana akiri zaidi ya ile walotumia interahamwe mwaka 1994 April huko Rwanda.
 
Vilevile Jaji Werema alisema kwa sasa Hakuna kipengere chochote cha Sheria kinachompa Mamlaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bung la Katiba na kuwataka watu wanasema hivyo waende kusoma sheria

Sasa kama Kikwete hana mamlaka ya kulivunja Bunge la katiba, ni nani mwenye mamlaka hayo? Angeliweka hili wazi badala ya kusema tu Kikwete hana mamlaka lakini kuwa kimya ni nani mwenye mamlaka hayo.
 
Kinachofanyika dodoma ni utafunaji wa posho na sio kingine. Werema kasema kweli, bila ukawa hakuna katiba mpya!
 
Kakobe aliwaambia habari ya mnara WA Babeli wakabisha. Ndo haya tunayaona sasa "JAJI WEREMA APINGANA NA IKULU ,ASEMA BILA UKAWA HAKUNA KATIBA"

ndg. tutarajie mengi kwa hiki chama kilicho kengeuka.ukiona kinawazarau wananchi ujue safari ya kuelekea kaburini imewadia. kanu ya kenya ilipitia tabia hizi hizi za ccm matokeo yake kimefutika kabisa kule kenya.
 
Kinachofanyika dodoma ni utafunaji wa posho na sio kingine. Werema kasema kweli, bila ukawa hakuna katiba mpya!

mkuu wote waliopo pale dom ni ulafitu umewapeleka laki3 kwa day siomasihara mkuu kuna mtu mpaka anakufa hajawai piga laki3 sasa kwa nini asikamie?
 
Vilevile Jaji Werema alisema kwa sasa Hakuna kipengere chochote cha Sheria kinachompa Mamlaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bung la Katiba na kuwataka watu wanasema hivyo waende kusoma sheria

Sasa kama Kikwete hana mamlaka ya kulivunja Bunge la katiba, ni nani mwenye mamlaka hayo? Angeliweka hili wazi badala ya kusema tu Kikwete hana mamlaka lakini kuwa kimya ni nani mwenye mamlaka hayo.

nchi ihi inaenda enda kama gari lililopoteza mwelekeo?
 
Haitoshi kwa AG na wengine kama yeye wanaotoa wito kwa UKAWA kurudi bungeni bila ku - adress sababu zilizowafanya wasusie vikao vya bunge. Bila shaka hata UKAWA wenyewe wanataka warudi bungeni lakini si kwenye bunge ambalo limejitungia kanuni tata na ambalo linadai lina mamlaka hata ya kuitupa kapuni Rasimu ya Tume.
 
Mpaka anambembeza hivyo kawa mpole. Mpaka anawakumbushia kwamba wanasali wote so what.
 
Back
Top Bottom