Mwanasheria anahitajika: Nataka kuwashitaki CRDB Morogoro kwa kuifunga akaunti yangu ikiwa na hela

idtech

Member
Jan 4, 2016
91
222
Mrejeasho.

Hawa wapuuzi wameifungua lisaa moja baada ya hii post.
Tunasafari ndefu kama Watanzia kwa hizi taasisi zetu ambazo full admns ni Watanzania wenyewe. Hatuko committed kwa kazi zetu, huduma zetu ni mbovu mno and no one cares.

Habari wakuu,

Naomba kama wewe ni mwansheria ama una firm ya sheria soma hitaji langu hapa then kama utaona kuna uwezekano wa kushinda kesi basi njoo imbox.

Nilifungua acc ya benk Crdb tawi la Morogoro miaka kama mitano hivi iliyopita kipindi naishi Moro nikiwa na mishe zangu hapo.

Nilihamia Mwanza nikaendelea kuitumia acc hiyo na nilimpa mwajiri wangu acc hiyo salary ikiwa inapitia huko.
Mara ya mwisho nimetoa hela mwezi wa kwanza tareh 30 kwenye ATM bila shida.

Tarehe 02 mwezi huu wa pili nilitaka kutoa hela kwenye ATM ikashindikana na hapo ndo tatizo lilipoanzia. Nilidhani ni tatizo dogo tu lingeweza kusovika kwa tawi lolote lile la hiyo benki.

Niliaenda CRDB Kinyata Mwanza nikawaeleza, wakaangalia acc yangu then wakaniambia wenye kuifungua ni huko Moro, wakaniambia tunawaandikia email kuomba kuifungua. Nikawauliza itakuwa tayari kwa muda gani. Wakadai ni hadi email ijibiwe na hawajui itajibiwa lini. Siku iliyofuata nilienda wakanipa jibu simple, email hajajibiwa.

Nikaona isiwe tabu nikatafuta namba ya huduma kwa wateja ya CRDB nikapa nilivyowapigia wakanipa majibu simple. " Nenda na kitambulisho chako cha NIDA tawi lolote la CRDB lililokaribu yako wakufungulie,". Sasa kwa vile kazini kwangu kuna hiyo benki nikaamua kuwatumia wao.

Wakapiga simu directly kwa branch Manager, simu haikupokelewa wakapiga tena hivyo hivyo, hakupokelewa.

Wakawaandikia compliance wao email wakaweka details za acc yangu wakaniambia nitapigiwa simu na hao compliance. Siku zikaenda no calls.

Nikarudi tena hapo nao wakashangaa kuona tatizo langu halijatatuliwa, wakawapigia Compliance waambiwa tuliaandikia email CRDB Moro waishughulikie, wakaamua kumpigia manager wakiwa wameunga watu watatu.

Baada ya simu kuita kwa muda mrefu manager akapokea, akaelezwa tatizo langu. Manager hakutoa majibu akasema nakuja. Wakasubiri zaidi ya nusu saa manager hakutokea, wakampigia staff wa kawaida wakamweleza tatizo langu, staff akaangalia acc yangu akasema acc imekamilika ila staff aliyeisajili ndo alisahau kuweka details zao za ndani ambazo mimi sijui ni details gani aliacha kuweka. Wakasema huyo staff kwa sasa kahamishiwa Mtwara. Wakamuomba aishughulikie akasema anaifanyia kazi.

Days goes on. Hakuna acc haijafinguliwa, nikarudi tena wakapiga simu. This time response is worse, wanadai aliyeifungua alikuwa intern hakujua vitu vingine vinavyohitajika, staff wa Moro wanashauri kwa vile acc ina matitizo waifute.

Staff wa hapa ofisini akamuuliza unaifutaje acc ya mteja ambayo ina hela zake? Huyo staff aliekuwa anaongea naye akasema basi asubiri wamtafute huyo intern aje aifungue.

Hapo ndo tulipofikia, so far nimekopa kila sehemu, na mwanangu anaumwa ndani sina hata mia mbovu.

Kama wewe ni mwanasheria na umesoma lalamiko langu, na ukaona unaweza kushinda case hii ni inbox. Na ingependeza akawa ni mwanasheria wa Mwanza.

Asante
 
Hicho ndicho kilichonifanya kutunza pesa zangu zaid ya billion 2 nifungua account moja ya nchi za afrika mashariki niliuzouza dhahabu maana bank za humu tz kina mambo ya ajabu.

Kufungiwa account inauma Sana usiombe ikutokee iskie kwa mwingine. Mtafute Tundu lissu Kama atapata nafasi he will help you.
 
Habari wakuu,

Naomba kama wew ni mwansheria ama unafirm ya sheria soma hitaji langu hapa then kama utaona kunauwezekano wa kushinda kesi basi njoo imbox.
Daaah pole sana chief.

Ila endapo technology ya crypto isingeingiliwa na hivi vijamaa kutoka stanford university vinavyojidai vinajua kumbe ovyo tu na mwisho kufanya ionekane kama scam, basi matatizo kama haya tusingekua nayo tena.

Bank za tz wana nyodo za kipuuzi sana, hamna sekta naichukia tz kama banking, ni hvo tu haina mbadala. Natumia equity kutunza hela, siwezi weka bank yyt ya tz, maybe kama ni gateway tu ya kupokea lkn sikalishi hela humo
 
Thanks mzee Kali, the more you become quite, the more your able to hear
 
Benki za kitanzania CRDB na NMB hazijielewi kabisa. Zina upuuzi mwingi na wengi hawajui kazi zao, wamewekwa hapo na ndugu tu. Fanya uwashtaki. Equity ingekuwa sehemu nyingi ningekuwa sina haja ya kuwa na akaunti na hawa wapuuzi.
 
Sjui kwa nini benk zetu zinakwama wapi! May be ni hilo la kuwekana na wanakimbizwa sana na hizo benk za wakenya. Imagine zamani mtu kuwa na Acc CRDB inakulazimu uwe na wadhamin watano wenye acc hiyo benki😳😳.

Kitu amacho naamini wengi walishindwa, wamekujagundua hilo hitaji linawakimbiza wengi too late. Equity ilikuwa ni ID yako tu ya taifa unapata account bila kupitia kwa balozi kujieleza.

Leo NMB mtu haudepost cheque kama wew sio uliyeandika hiyo cheque ama ulieandikiwa. Lakn Equity mtu yoyote anadepost cheque bila shida yoyote ile.

Mnakumbuka NMB mtu ukipoteza card ilivyokuwa shida kutoa hela.

Hizi benki zetu ni taabu tupu. Basi tu mwajiri wangu nilazima hela ipitie huko.
 
Hawana uwezo kabia. Equity unajaza kuwa unahitaji card yako ifanye na visa, ukirudi nyumbani card ipo active. NMB eti mpaka ujaze mafomu gani sijui mengine!!! Ukiwaangalia walivyovaa nadhifu unaweza sema ni watu wa maana kumbe kichwani hamna kitu. Habari za anayeshughulikia ishu yako kaenda likizo ni nyingi sana huko.
 
Pole Sana Unapita Kwenye Changamoto Ila Hakikisha Unawapeleka Mbele Wajifunze
Nilipita Gairo CRDB, Natoa Cash ATM Akaja Mfanyakazi Wa Hiyo Bank
Ananiona Mimi Kama Vile Natoka Kijijini

Ananiuliza Umejiunga Simbanking Nikamjibu Hapana
Kwanini , Nikamjibu Huduma Hiyo Siitaki Kwakuwa Ina Makato

Akasema Simbanking Ni Lazima Kwa Mteja Wa CRDB
Nikamjibu Vema Itakapokuwa Simbanking Ni Lazima Basi Nitatoa Cash Zangu Zote
Nikamtolea Card Ya Bank Nyingine Nikamuonyesha Nikamwambia Umeiona Hii

Yaani Kuna Wakati Hizi Banks Ni Upuuzi Bora Cash Kuweka Kwenye Jaba Kama Kakobe
 
Habari wakuu,

Naomba kama wew ni mwansheria ama unafirm ya sheria soma hitaji langu hapa then kama utaona kunauwezekano wa kushinda kesi basi njoo imbox.
Kwanza pole mkuu. Mimi ni lawyer ila siko Moro.

Kwa uzoefu wangu mabenki mengi huwa yanapuuza mambo kwa wateja wa kawaida mpk pale utakapomu-engage Mwanasheria (Wakili) kwenye jambo lako; hapo ndiyo wanaanza kukuona uko serious.

Hatua ya kwanza ni kuwaandikia DEMAND NOTICE AND AN INTENTION TO SUE (HATI YA MADAI NA KUSUDIO LA KUSHTAKI). Hii ni barua ambayo unaweza kuiandika hata wewe mwenyewe (ingawa ni vema zaidi ikiandikwa na Wakili kwasababu inakua na lugha kali kidogo ya Kisheria).

Ikiwafikia lazima wakutafute kwasababu wanajua kesi ikienda Mahakamani jambo litakuwa kubwa zaidi. Pesa ambayo utamlipa Mwanasheria watakurudishia endapo wakikuita kwa ajili ya settlement.

Hapo kuna hela mkuu, ukimpata Mwasheria smart.

Kimsingi hapo una CAUSE OF ACTION (SABABU YA KUSHTAKI) nzuri tu ya UZEMBE KWA UPANDE WA BENKI.

Njoo PM kwa msaada zaidi, naweza kukuandikia nikai-scan nikakutumia ukanilipa kifuta jasho. Kila la kheri mkuu. Ila narudia tena, pole sana.
 
Hicho ndicho kilichonifanya kutunza pesa zangu zaid ya billion 2 nifungua account moja ya nchi za afrika mashariki niliuzouza dhahabu maana bank za humu tz kina mambo ya ajabu.

Kufungiwa account inauma Sana usiombe ikutokee iskie kwa mwingine. Mtafute Tundu lissu Kama atapata nafasi he will help you.
Mkuu naomba laki 2 tu nilipe kodi.
 
Back
Top Bottom