mwanao anaitwa nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mwanao anaitwa nani?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by eRRy, Mar 4, 2010.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,076
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wakatoliki - wanaume wanne na mwanamke mmoja - walikuwa wanakunywa kahawa kwenye mkahawa jioni moja. Mwanaume wa kwanza akaanza kuwaambia marafiki zake “Mwanangu ni padri, kila anapokwenda kila mtu humwita "Father"
  Yule mwanaume wa pili akadakia kwa sauti ya juu kidogo “Mwanangu ni Askofu. Kila anapokwenda kila mtu humwita “Your Grace”
  Mwanaume wa tatu akasema kwa madaha “Mwanangu yeye ni Kadinali. Anapofika kwenye halaiki kila mtu humwita “Your Eminence”
  Yule mwanaume wa nne akazungusha macho kisha akasema. “Mwanangu ni papa. Kila anapokwenda kila mtu humwita “Your Holiness”
  Mwanamke pekee katika kundi lile aliendelea kunywa kahawa yake kimya kimya bila kujali majigambo ya wale wakatoliki wenzake wa kiume. Kuona hivyo, wale wanaume wakamuomba awaambie cho chote kuhusu mtoto wake. Kwa sauti yenye mamlaka, kujiamini na majivuno kidogo akasema “Binti yangu ni mrefu, maji ya kunde, umbo la wastani namba nane, matiti makubwa, tumbo jembamba saizi 24 na mahips makubwa saizi 44. Anapofika kwenye halaiki kila mtu husema “Oh My God!”

   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 32,251
  Likes Received: 15,060
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda sana..
  Imenitengenezea siku yangu ile mbaya
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,602
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  hahahahaaa! safi sana.
   
Loading...