Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,080
- 1,448
MAMBO 6 NINGEJIFUNZA KABLA YA KUFIKA MIAKA 30
NAMBA 1
Mwanamke anayekupenda kwa dhati, huwa tayari kubadilika kwa ajili yako.
Atarekebisha tabia yake, sauti yake, mienendo yake na kila kitu kinachoweza kuhatarisha kukupoteza.
Mapenzi ya kweli huambatana na jitihada za kulinda uhusiano.
NAMBA 2
Kama mwanaume, epuka kujionyesha.
Jifanye huna pesa hata kama mifuko yako imejaa fedha.
Watu wengi hubadilika wanapoona mafanikio yako, na si kila anayekusogelea ana nia njema.
Unyenyekevu hukulinda zaidi kuliko kujionyesha.
NAMBA 3
Katika kizazi hiki, wanaume wenye nia safi hupitia changamoto kubwa sana.
Ukweli, uaminifu na moyo wa dhati mara nyingi havithaminiwi kama zamani.
Lakini usibadili utu wako kwa sababu ya dunia iliyobadilika.
NAMBA 4
Wewe ni mwanaume.
Asilimia kubwa ya mawazo yako inapaswa kuelekezwa kwenye:
Kutafuta pesa
Kuinua maisha yako
Kujenga future yako
Kutengeneza heshima yako
Sio kutumia muda mwingi kuwaza nani hakukusalimii au nani haongei na wewe.
Mwanaume mwenye malengo makubwa huwa bize kujijenga.
NAMBA 5
Usiwe mchoyo unapowekeza kwenye maisha yako mwenyewe.
Vaa nguo zenye ubora
Fanya mazoezi
Soma vitabu bora
Jifunze kwa watu sahihi
Kula chakula bora
Uwekezaji wa bei rahisi mara nyingi huleta matokeo ya bei rahisi.
Maisha bora yanahitaji kiwango bora.
NAMBA 6
Kata mahusiano na mtu yeyote anayekudanganya, anayekudharau, anayekutumia au anayekufanyia mzaha wa kukuumiza.
Hata kama ni rafiki wa karibu au ndugu.
Amani yako ya akili ni muhimu kuliko kulazimisha mahusiano yasiyo na heshima.
Maisha humfundisha mwanaume kupitia maumivu, makosa na experience.
Lakini mwanaume mwenye hekima hujifunza mapema kabla maisha hayajamlazimisha kwa nguvu.
Abuuabdillah ✍️
0744 883 353