Mwanangu Mwanauba, jifya moja haliinjiki chungu

Mwanangu Mwanauba, jifya moja haliinjiki chungu

kwiii kumbe na wewe ulishasikia eeh ,ujue ndo maana wanawake wengi hata mirija ya uzazi inaziba ..kuingiza ingiza mavitu huko ....... siwezi hata chumvi mie asietaka na asile
na ile unaweka nyama huko siku tatu mpaka inapikika inakuwa lainiiiiiiii unampa mmeo limbwata hahahahahhahahah wanaume wanabebeshwa mengi sana .
 
mmmmm Alikua anafurahisha wageni Mwanauba achuje linalo mfaa achukue lisilomfaa amuachie nayo...na wale walokua wakicheka wanajifurahisha nafsi zao wengine wanamuona anasema sawa wengine ndio kama wewe amekuchefua roho..
lakini kwakweli hawa watu wanaongea pumba sana wakati mwengine....
 
wazo zuri huwezi kula ugali maharage kila leo unakinai ujue
images
keki yakoya kitchen party hiyo ya mafiga matatu
 
na ile unaweka nyama huko siku tatu mpaka inapikika inakuwa lainiiiiiiii unampa mmeo limbwata hahahahahhahahah wanaume wanabebeshwa mengi sana .
ahahaaaa duh tena kongoro
 
si ladha ni maujuzi kunako hawa wanaume wanatofautiana shosti kuna mmoja nilikuwa naye nilikuwa nawaza hata kugegedana naye kwajinsi alivokuwa kilaza ila huyu wa sasa usipime ni mjuzi balaa
kwa hiyo wanaume wana ladha tofautitofauti ?
 
si ladha ni maujuzi kunako hawa wanaume wanatofautiana shosti kuna mmoja nilikuwa naye nilikuwa nawaza hata kugegedana naye kwajinsi alivokuwa kilaza ila huyu wa sasa usipime ni mjuzi balaa

teh teh teh, haya bwana kwa raha zako mtoto wa kike..
 
Hao watakuwa waswahili tu wenye kuendekeza mambo ya mitala
 
kweli shosti maplay-boy wako vizuri nazani practice inawapa uperfect jaribu uone ila usiwe na moyo mwepesi wa kulia wivu wala usifall in love na player
nasikia maplayer boy watam kweloi nkweli
 
kweli shosti maplay-boy wako vizuri nazani practice inawapa uperfect jaribu uone ila usiwe na moyo mwepesi wa kulia wivu wala usifall in love na player
mimi nipo na playerboy mstaafu
 
Nawapenda wote!!
Ni juzi tu nilialikwa kwenye kitchen party ya jirani yangu Mwanauba, nilijuta kwanini nilikwenda maana nilijikuta nikipoteza raha yangu yote.....

Mama mmoja ambaye alialikwa kumfunda Mwanauba alikuwa akiongea maneno ambayo yalikuwa yakiniuzi kila alipoendelea kuongea, nilitembeza macho yangu huku na huku kutizama wenzangu kama walipokeaje yale mahusia ya kungwi kwa bibi harusi Yule mtarajiwa, chakushangaza watu walikuwa na furaha ya ajabu, hasa wanawake waliokwenye ndoa wa pale mtaani, walishangilia na kupiga vigelegele za shangwe!!

Moyoni sikuona kama huo ndio ulikuwa wakati muafaka wakusemea maneno yale pale ukumbini, nilidhani mambo ya ndani watakua wameshamwambia Mwanauba na pale ukumbini ni kuserebuka tu Utamu wa Yesu!!

Alianza hivi, “Mwanangu Mwanauba ukibeba ndoo ubebe na kidumu mkononi, kuna bahati mbaya mwanangu waweza jikwaa ndoo ikaanguka na maji yakamwagika ukabaki na kidumu kikakufaa kuoshea vyombo, kumbuka siku zote chombo hakiendi ila kwa nyenzo mwanangu, Mwanauba mkono mmoja hauchinji ng'ombe hata siku moja kaa ukijua hilo mwanangu, hakika Mwanauba…tendegu moja halisimamishi kitanda tumia akili!!

Watu walipiga kelele za furaha wakati kungwi Yule akimalizia na kusema hivi, mwanangu Mwanauba namalizia na kusema hivi, “jifya moja haliinjiki chungu, sharti matatu ili chungu kikae vema jikoni” asante MC asante sana!!!

Mie nilibaki hoi nikijiuliza hawa makungwi wanatufundisha nini?? Wanaifundisha nini jamii?? Je Mwanauba jirani yangu amejifunza kitu gani pale!! Mbona wakina mama nanihii walikuwa wakishangilia sana na kupiga vigelegele kwa kuonyesha waliambiwa kitu ambacho wanakifanya au walitamani kukifanya hivyo walikosa mshauri tu!!

Baada ya sherehe nilijirudia zangu nyumbani kwangu kama shomoro alienyeshewa na mvua!!

Nawatakia wakati mwema rafiki zangu!!

Siku nyingine ukialikwa kwenye kitchen party, wapotezee!!! vinginevyo, wataendela kukuchefua na kukukwaza. Pole sana, yamekukuta eeeeeeeehhhhh!!!!
 
"........... wi Smile leka na na ulana lu monomao.........."
Nivea?????
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ndio shida ya kuokota makungwi uswahilini na hapo ukute limesha achika mara kumi zaidi ndio maana anampotosha mdada wa watu
 
pole sana shosti huwa hawastaafu mwenyewe wangu anajidai amestaafu lakini ni juzi tu kaniletea miwasho once a player always a player asili ya maji ni baridi na hilo halitobadilika miaka dahari
mimi nipo na playerboy mstaafu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom