Mwanangu hataki kuongea nami, nafanyaje?

Psychology natumaini imekusaidia kuishi na kila mtu hasa baba ako na familia yenu kwa ujumla, kwasababu naamini unaweza kumsoma kila mtu
Mamii nimejipanga kuwa baba bora ambae ahjawahi kuwepo.. najifunza makosa ya walio tulea.. Nimesomea Psychology, nasoma sana vitabu vya mambo ya makuzi na malezi najitahidi kujianda kuwa baba mzuri huko mbeleni
I
 
Hili jambo lipo,ila dingi Langu alikuwa peace kinoma yani,kuna time mpaka tulikuwa tunapga story za mademu hasa hawa wa bongo movie na wale wa kitaa,

Ila ninacho mshukuru mzee alikuwa na itikadi moja kutusisitiza wanae "wanangu kusoma siyo kushindana,wew soma ili usipate chini ya alama (C)"

Mzee alikuwa ana wambia kabisa,wanangu cwez kuwakataza kufanya ngono ila kumbukeni ukimwi upo,ukipata kademu chapa ila ukumbuke kondom tu,

Hicho kitu kilifanya nisome kwa kurelax na kujiamini.

Mzee alikuwa ni mtu safi tofauti na wazee wengne,

Kuna watu walikuwa wanadai pale kitaa kuwa mzee anatulea vby cha ajabu watoto wao saiv ndo wavuta bangi na hawana mwelekeo huku sisi tukipeta tu,hivi vitisho wanavyo tumia hasa hawa baba zetu kwa kudhani ndo malez bora Mara nyingi ndo hufanya tuwaogope baadhi ya baba zetu

Rest in peace Dingi.
 
usije kuwa ndugu yangu, maana kama mzee kabisa full ukauzu.
 
pole kwa kufia hata mm tukiongea na e sana kwa simu basi tunakua tuanajadili mademu.. anauliza eehh unaoa lini, una mademu wangap sasa hv.. ukiwa na demu niambie. hapo anakua yuko na marafiki zake kalewa
 
Psychology natumaini imekusaidia kuishi na kila mtu hasa baba ako na familia yenu kwa ujumla, kwasababu naamini unaweza kumsoma kila mtu

I
Nashukuru kwa hilo limenisaidia sana maishani jinsi ya kukopi na tabia za watu
 
pole kwa kufia hata mm tukiongea na e sana kwa simu basi tunakua tuanajadili mademu.. anauliza eehh unaoa lini, una mademu wangap sasa hv.. ukiwa na demu niambie. hapo anakua yuko na marafiki zake kalewa
yeah hvo Ndo fresh,dingi zetu Wanapenda ushikaj na sisi watoto wao ila sema Ndo hvo tuna waogopa..
 
Mpe faraja baba usifanye makosa, mimi natamani baba yangu angerejea ili nifanye marekebisho
Kwakweli ninaanza leo hii sitaki nijute kama weewe. Uwe unanikumbusha....
 
pole kwa kufia hata mm tukiongea na e sana kwa simu basi tunakua tuanajadili mademu.. anauliza eehh unaoa lini, una mademu wangap sasa hv.. ukiwa na demu niambie. hapo anakua yuko na marafiki zake kalewa
Duu hongerni mim Mzee Wang upige story za madem sipat picha
 
Nadhan ungetumia hekima kuongelea vyema ishu yako na baba ako bila kuwakandia wenzio na kuwaita watoto wa mama, huo. Unaofanya ni upuuzi
 
Usipojenga urafiki na watoto wako wakiwa bado wadogo, wakazoea kujiachia wakaongea nawewe. Usitarajie wawe rafiki zako wanapokuwa wakubwa.

Mtoto umleavyo, ndiyo akuavyo. Samaki mkunje angali mbichi.

I'm experiencing the same shit. Inafika mahali unajaribu kucreate friendship lakini unaskia moyo unakwambia hapa haiwezekani. Nilichojifunza ni kwamba...SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI,,MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO.

Jamii isije ikalaumu watoto kwa lolote! Hayo yote mnayoyaona ni matokeo ya malezi. Ukilea vizuri utapata matokeo mazuri na kinyume chake ni sahihi kabisa.
 
Nadhan ungetumia hekima kuongelea vyema ishu yako na baba ako bila kuwakandia wenzio na kuwaita watoto wa mama, huo. Unaofanya ni upuuzi
For sure...
Mm hata ukiniita mtoto wa mama kisa nampenda mama haina shida
 
Kwa kuwa ni mwanaume nitakuambia jambo hili ulizingatie sana maana utakuwa mzazi pia. Umesema dada yenu anaongea sana na baba yenu kuliko nyinyi, unafikiri kwa nini? Kuna uwezekano mkubwa pia dada yenu hayuko huru sana kuongea na mama yenu kuliko baba. Na huenda mama anamlalamikia dada yenu kumshirikisha mambo yake badala ya ya yeye mama.

Iko hivi, siku zote baba hujikuta katika upendo kwa mtoto wa kike na mama kwa mtoto wa kiume kutokana na matarajio ya wazazi yenye nia njema kwa watoto wao.

Baba siku zote anataka mtoto wake wa kiume awe mwanaume kweli anayetegemeka, jasiri, shupavu, mwenye msimamo thabiti na ikiwezekana afuate nyayo zake hata kumpita. Hilo ndio tarajio la baba yeyote, hivyo ukilegalega utakula makofi, ngumi, makofi ili kukuweka sawa. Na sehemu utakayopata kitulizo ni kwa mama na ndio sababu watoto wa kiume wengi ni watoto wa mama mpaka uzeeni. Wanahisi baba hakuwahi kuwapenda ila mama aliwapenda zaidi kitu ambacho kumbe sivyo.

Vivyo hivyo kwa watoto wa kike. Siku zote mama anataka binti yake awe mwanamke wa ukweli kama yeye akifanya uzembe anakula miko, anatandikwa na bakuli. Na mtu anayembembeleza ni baba hali inayopelekea kuwe na bond kubwa kati ya baba na binti kuliko binti na mama. Na ndio maana binti hata akiolewa mtu anayemsikiliza zaidi ni baba yake na ukikutana na mwanamke anayependwa sana na baba yake na kwao wana uwezo mwanaume utapata shida.

Jaribu kukumbuka wewe mwenyewe nini kilikufanya usiwe karibu na baba? Kwa kuwa ni mtu mzima uanaweza kutafakari yote aliyokuwa anakufanyia ilikuwa kwa nia njema au mbaya? Na umeshasema baba ana sifa ya ukimya hivyo yawezekana mengine ulimfukiria tofauti na alivyo moyoni. Mpende baba yako, ongea naye, muulize wanaendeleaje yeye na mama, muulize kuhusu shuguli zake, mpe hela ya soda au chochote anachotumia, mpe mipango yako ya maisha kisha msikilize atasemaje. Usidharau maoni yake hata kama mnatofautiana kimtazamo kwa baadhi ya mambo. Na huenda akakwambia mambo mengi ambayo huyajui kuhusu familia yenu yatakayokusaidia hata siku akitoweka duniani.
 
Umeongea point sana mkuu..Nitafanya ushauri wako
 
Huyu jamaa

1. Hana demu/ na hataki hawezi kuwa nae
2. Anakaa jikoni na kupika na mama yake wakati mzee yupo siiting room
3. Hashabikii mpira
4. Havuti sigara wala bangi
5. Meneno yake “...mpaka basi yani..”

Nahisi una umama umama wa kutosha

Mimi ni mkali sana kwa dogo inapokuja kwenye misimamo ya kimaisha, ila ni marafiki sana, na tunacheza (PS) na kuongea mengi, ila kwa namna mama yake alivyo bila mimi tungekuwa na toto kama mtoa mada
 
Ckuwahi kuishi na baba! Mama angu alikuwa mkimya sana.... Muda wote ananisikiliza mimi tu nakucheka, kutabasamu ..nampa stori zooote za siku nzima! Namwimbia! Aisee nilikuwa mapepe! Mungu amrehemu
 
Just we muulizeulize tu maswali MF.MTU flani yuko wapi anafanya nn..na yule mwengine nae yuko wapi anaendeleaje automatic mtaongea na kucheka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…