Jpinduzi
Senior Member
- Feb 26, 2011
- 136
- 68
Wajibu na majukumu ya mwanamke ni kama ya mwanamume, na suala lake ni kama la mume yaani suala la haki, ujumbe na marejeo. Isitoshe, mustakbali wa kazi yoyote ni dini kwa njia moja au nyengine mwanamke naye ana kazi yake.Kuna kazi zingine ambazo hakuna awezaye kuzisimamia na kuzitekeleza ila yeye, kwa maana hiyo, huwezi kupata harakati zozote zenye kufaulu ila mwanamke atakuwa na fungu lake kubwa humo. Kunahaja ya kuweka picha bora zaidi kwa mwanamke; vipi anapaswa awe, nini wajibu na majukumu yake.