Mwanamke wa kunipa mtoto tu

Mimi sijali mkuu, kuwa na mtoto siyo kosa hata kdg na si lazima awe wa jf
Vip nikutimie namba zao mkuuView attachment 2379229
JamiiForums254860030.jpg


Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Amani iwe kwenu wapendwa.

Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 40 BILA MTOTO WALA MKE (ni member wa muda humu, sema nimeamua kutumia id tofauti ili kutunza heshima).

Ni mtumishi kwenye kampuni binafsi inayoendesha shughuli zake Dar es Salaam. Kwa nyakati tofauti nimekuwa na mahusiano na wadada tofauti lakini naona hakuna ambayo yalifikia kwenye ndoa.

Kuna wakati huwa najifikiria labda mimi ndiyo nina kasoro lakini mwishowe naishia kusema labda mimi sikubahatika.

Kwa sasa, suala la kutengeneza mahusiano kwangu limekuwa changamoto, kazi yangu inanibana sana, mambo yangu binafsi, pia naona uzee umeingia kiasi kwamba nashindwa kuendana na mahitaji ya wadada wengi kama kuwasiliana mara kwa mara, kuvumiliana vumiliana vitu ambavyo ukiviangalia unaona kabisa hapa mtu alitakiwa ajielewe.

Hivyo,
Naona ni wakati nitafute mwanamama/mdada wa kuzaa naye mtoto tushirikiane kumlea pamoja.

Vigezo:
~ Awe tayari kupima afya
~ Awe mkristo umri na rangi yoyote
~ Awe na akili akili kidogo
~ Asiwe anawaza tu ndoa akilini mwake
~ Awe tayari kumpima DNA mtoto baada ya kujifungua.

MIMI,
Nitajitolea gharama zote za kumtunza wakati wa ujauzito (maisha ya kawaida tu lakini, yasiwe luxury sana), hata baada ya kujifungua nitaendelea kutoa matumizi ya mtoto.

Naomba kuwasilisha.

Note: Kwa wale wenye kejeli, ni kweli mimi ni domo zege, kwahiyo msirudie rudie hilo hapa.
Umeshapata?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom