Mwanamke wa aina gani anafaa kuwa naye kwenye mahusiano?

Habari jf

Mimi ni kijana wa miaka 25 naishi morogoro na najitegemea nilikuwa naomba ushauri juu ya mwanamke wa aina gani naweza kuwa nae akanipa furaha na hata kufika malengo yetu

Ahsanteni sana

Ningekuwa wewe ningezingatia yafwatayo;

1. Je, ananipenda kweli au ananipendea hela zangu? Hapa nitafanya uchunguzi binafsi ikiwepo kumpitisha kwenye ukata wa kujitakia pamoja na ubaili tu wa makusudi ili nione atafanyaje.

2. Je, anamtazamo gani wa maisha ya kifamilia husuani kesho? Ni mtu ambaye kwake burudani na furaha za ujana ni muhimu kuliko kesho? Kwamba viwanja, shghuli na shosti zake ni muhimu kuliko kesho?

3. Anapenda kujishughulisha kiuchumi au ni wewe tu ndo mwenye kuleta hadi chumvi huku yeye akinenepesha chura? Kwamba atakusubiri mpaka urudi ndo utoe hela ulizopata kwenye mihangaiko ndo aanze kuandaa chakula?

4. Mtazamo wake kuhusu ndugu zako ni upi? Je anaonekana kuwa mtu ambaye ataiunganisha familia au atakutenganisha na ndugu?

5. Je, kuna vitu ambavyo mnawaza kwa kufanana au mnakubaliana? Hapa ni maadili na misingi za kifamilia labda namna mtakavyolea watoto na kuishi ndani.

6. Wewe mwenyewe unamuonaje? Ni mtu anayestahili heshima yako?

7. Vipi katika kutafuta wakati wa ugomvi, ni mtu wa namna gani? Anatumia njia zipi kufikisha ujumbe hususani anapokuwa ameghafirika na je anatumia njia gani kutatua mgogoro?


Ndoa ni zaidi ya mbususu.
 
Back
Top Bottom