ndyoko
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,971
- 1,650
Muda huu tunapoongelea uhuru wa miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, kuna mwanamke hapa Chan'ombe Dodoma limemshuka, tena looooooooooooooote! Ameolewa ana miaka 9 ktk ndoa yake ingawa hajabahatika kuzaa ktk ndoa yake hii. Mumewe siku zote hakujua kuwa kabla ya kuoana alishazaa mtoto wa 'ujanani'. Hakumueleza mumewe wakati wa urafiki, uchumba na baada ya ndoa. Juzi huyo mtoto wake wa ujanani alokuwa akiishi na bibi alifariki hapa dodoma, hivyo ilibidi mama na mumewe waje dodoma, huku mume akijua kuwa mtoto aliyefariki alikuwa ni wa kaka wa mkewe. Hakukuwa na jipya lililoendelea zaidi ya hali ya majonzi miongoni mwa wafiwa.
Hali libadilika leo asubuhi wakati wa maandalizi ya kwenda kuzika wakati wa kuaga mwili. Mama alipoenda kwa jeneza, si ndo akaanza kulia kwamba anamuachia upweke kwani yeye ndiye alikuwa mwanawe pekee, ataishije bila kuwa na mtoto. Siku zote alikuwa akijivunia kuwa mzazi sababu ya yeye ingawa alikuwa akisemwa hazai na watu na majirani. Minong'ono ikawa mingi pale msibani baada ya kuona ameng'ang'ania kwa jeneza zaidi ya dk 5 ambapo ililazimu watu waende kumuondoa ili taratibu za mazishi ziende kama ilivyopangwa.
wakati minong'ono ikiendelea ndipo mumewe alipojua na kuthibitish kwamba kumbe mtoto aliyekuwa akimjua kama mpwa wa mkewe, ukweli alikuwa ni mtoto wa mkewe. Jamaa alimaindi sana, na nusura aondoke msibani ila busara ya wazee ilisaidia jamaa abaki msibani na kuendelea na mazishi. Ajabu mara baada ya kurudi mazishini, pamoja na juhudi za wazee na ndugu kumuomba baki ili waliongelee hilo, jamaa alifungasha vitu vyake na kurudi dar, pamoja na juhudi za mkewe kumsihi ili wamalize issue hii kabla ya kurudi zao dar na mumewe. Hakuna nayejua nini kitafuatia baada ya 'aibu' hii kujulikana.
My take: Chondechonde kina dadana wanaume pia, kama mtu kakupenda epuka kumdanganya issue ambazo ziko wazi kama hii au kabila yako. Mambo hayo hayana kificho yatakuja julikana tu. Na ukweli utakapojulikana utakosa pa kuuficha uso wako.