Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Kuna msemo mmoja unasema "don't judge a book by its cover". Hii ina maana kwamba usihukumu kitu kwa mwonekano wake........ Naam hiyo iko kila mahali, ni jambo ambalo tumefundishwa na jamii kuhukumu kwa kuangalia muonekano wa mtu au kitu na hii mara nyingi hutupelekea kupata hasara au kupoteza nafasi ambayo tulikuwa tunaitafuta au tunaisubiria kwa muda mrefu.
Mara nyingi jambo hili huwa linawatokea wanawake tofauti na wanaume. Huwa inatokea mwanamke kutovutiwa na mwanaume anayejaribu kumuomba kutoka naye kwa mara kwanza. Inaweza kuwa mwanaume huyo anayo dhamira thabiti ya kupata wasaa na binti ili kuangalia mustakabali wa maisha yao ya baadae kama wanaweza kujenga familia lakini kwa bahati mbaya sana kwa jicho la kwanza mwanamke huyo anaweza kujikuta akiwa havutiwi kimapenzi na mwanaume huyo na wala hahisi msisimko wa kimapenzi juu yake.
Hali hiyo inaweza kumfanya mwanamke akakataa mwaliko huo katika namna ya kukatisha tamaa. Kauli kama, "eti nitoke na wewe, hivi unanionaje….." au "sina muda huo…." Ni kauli ambazo hutolewa na wanawake wasiovutiwa na wanaume wanaowaomba kutoka nao. Lakini pia inaweza kutokea akiwa na mashoga zake kisha mwanaume huyo akapita maeneo hayo… anaweza kumzungumzia huyo mwanaume kwa mashoga zake katika namna ya kumponda.
"Mnamuona yule mkaka, eti ananitongoza….siku hiyo mwenyewe nimetulia zangu, kanijia.. ooh dada samahani naomba kesho ujumuike na mimi kwa ajili ya kupata dinner pamoja...... Mh! Nilimpandisha na kumshusha, hivi kaniona mie ndio wa kutoka naye… he he heeeeee, hebu aniondolee mikosi mie" Anaweza kusema hivyo kwa dharau na kumalizia kwa kicheko yeye na marafiki zake. Jambo hili hutokea sana na ninaamini hata wanawake walio humu JF wanalijua.
Mimi ni muathitrika wa jambo hilo, ilitokea takriban miaka kumi iliyopita nilitokea kumpenda binti mmoja, sikumpenda ili nimpotezee muda, la hasha, nilimpenda ili kama tukikubaliana nimuoe kabisa, kwani nilivutiwa na tabia zake na pia familia anayotoka. Nilifanya majaribio kadhaa ya kutaka kuzungumza naye lakini alionekana kuwa mgumu sana, na hata nilipopata fursa ya kukutana naye katika sherehe fulani na kuzungumza naye, alionekana kuwa na msimamo huo.
Nilimwelelza dhamira yangu ya kutaka kuwa na uhusiano naye na kama tukikubaliana nimuoe. Jambo la kwanza alitaka kujua nafanya kazi gani, nilipomweleza kazi ninayofanya, hakutafuna maneno, alinikata kalma na kuniambia kwamba hayuko tayari kuolewa na mwanaume anayefanya kazi kama yangu, kwani kwa mujibu wa uzoefu wake wanaume wanaofanya kazi hiyo huwa ni malaya sana. Nikahukumiwa kwa sababu ya kazi yangu. Mwaka huo huo nikampata mama Ngina na baada ya uchumba wa miaka miwili tukafunga ndoa. Leo hii ni miaka kumi imepita yule binti hajaolewa na ana watoto wawili ambao amezalishwa na wanaume wawili tofauti.
Nimewahi kuongea na baadhi ya wanawake walioolewa ninaofanya nao kazi, na wale ninaoishi nao huko mtaani, wengi walikiri kwamba waume waliowaoa wala hawakufikiria kwamba itatokea wawapende. Walisema kwamba kwa mara ya kwanza walipokutana nao hawakuvutiwa nao na hata walipojaribu kuwatongoza waliwakataa kwa dharau na hata kuwaporomoshea matusi, lakini kutokana na wanaume hao kutokata tamaa hatimaye walijikuta wakianzisha uhusiano nao na hatimaye kufunga ndoa na sasa wanaishi kwa amani tofauti na jinsi walivyowachukulia kwa mara ya kwanza walipowaona.
Hii huwatokea wanawake wengi, kuwadharau kwa jicho la kwanza wanaume wanaojaribu kuwatongoza. Ni vyema wakati mwingine kuwapa nafasi kwani hujui mwanaume huyu anayo dhamira gani juu yako. Toa nafasi kwani kuzungumza na mwanaume ndio kufanya tendo…..? Msikilize kisha mchunguze kama anavyo vigezo unavyovitaka, lakini pia huwezi kupata majibu yote kwa wakati mmoja inahitaji kidogo kuwa karibu na mwanaume huyo ili kujiridhisha.
Naomba nitahadharishe kwamba si vyema kukimbilia kukutana kimwili kwanza, jambo hilo lina hatari yake, kwani tendo la ndoa hufunika akili kiasi cha kushindwa kufikia maamuzi yenye busara. Inashauriwa kusubiri siku 90, ndipo ufanye uamuzi wa kukutana kimwili kama unaona jambo hilo lina umuhimu sana, lakini kama ukiweza subiri mpaka mfunge ndoa. (Mara nyingi jambo hili ni gumu kwani vijana wa siku hizi wenyewe husema haiwezekani kuuziwa mbuzi kwenye gunia (LOL)
Nakubali kwamba, wakati mwingine kumkubalia mwanaume kirahisi kunaweza kushusha thamani yako lakini unapokataa kifedhuli na kutweza, unakuwa kama unajenga ukuta kwa mwanaume huyo kufanya jaribio la pili. Kuna wanaume wasiopenda kudhalilishwa, hivyo hukata tamaa na kusahau.