Tofauti kati ya mwanaume na mwanamke

PromiseLand

JF-Expert Member
Jun 24, 2021
279
376
Zipo tofauti nyingi kati ya MWANAUME na MWANAMKE zinazosababisha migongano mingi kwa wahusika kwa kutokujua, laiti kama wangezijua tungepunguza migongano na migogoro isiyo ya lazima.

1) MWANAUME aliumbwa kutokana na udongo lakini MWANAMKE hakuumbwa kutokana na udongo yeye alitolewa kwenye ubavu wa MWANAUME (Mwanzo 2:7, 21-22) kwa hiyo hata kiuumbaji MWANAMKE na MWANAUME wameumbwa kwa namna tofauti.

2) Hakuna MWANAUME anayewaza kama MWANAMKE na hakuna MWANAMKE anayewaza kama MWANAUME hata kama wote wameenda shule. MWANAUME anawaza kwa mpangilio ndiyo maana hakurupuki kufanya maamuzi, lakini MWANAMKE anawaza kwa hisia ndiyo maana wanawake wanafanya makosa mengi kuliko wanaume na wanaongoza kuomba msamaha mara nyingi kuliko wanaume.

👉Kwa mfano kama kungekuwa na mabox ya zawadi 100 halafu akawapa MWANAUME na MWANAMKE wayafungue, MWANAUME atafungua box moja moja lakini MWANAMKE atatamani mabox yote 100 ayafungue kwa pamoja.

👉 MWANAMKE ana Uwezo wa kufanya jambo zaidi ya moja kwa wakati mmoja, unaweza kukuta wanawake salon kwanza wanasuka pili wanaangalia tamuthilia lakini wakati huo huo wanapiga umbea. MWANAUME huwa hawezi yeye ni jambo moja tu ndio atalifanya kwa ubora.

3) Hitaji la MWANAUME namba moja kwa MWANAMKE ni sex, MWANAUME akikosa sex anakuwa mkali, mkorofi kisaikologia anakuwa vibaya na kadiri MWANAUME anavyopata sex hihitaji zaidi kwa ufupi MWANAUME hatosheki na sex. Lakini Hitaji la MWANAMKE namba moja kutoka kwa MWANAUME siyo sex bali anahitaji kujaliwa yeye akifanya sex mara moja anaweza kukaa hata mwezi bila kuhitaji tena na tofauti hii ndiyo chanzo cha migogoro katika ndoa nyingi.

Kwa ufupi hizi ni tofauti chache kati ya nyingi ambazo wanaume na wanaume wanatofautiana tukizijua tutajua namna ya kuchukuliana na kupunguza migogoro. Weekend njema.
 
Raha ya mapenzi kuwe na migongano mkijuana sana inaboa! Mapenzi yananoga huyu kafanya hili huyu kafanya lile,mmoja akinuna anabembelezwa sio mapenzi yametulia kama maji ya mtungi ukidumbukia yanakuua taratibu.. kikubwa kwani kuchangamshana kusilete michepuko na ngono zembe tukauwana kwa magonjwa yanayoweza kuepukika!
 
Zipo tofauti nyingi kati ya MWANAUME na MWANAMKE zinazosababisha migongano mingi kwa wahusika kwa kutokujua, laiti kama wangezijua tungepunguza migongano na migogoro isiyo ya lazima.

1)MWANAUME aliumbwa kutokana na udongo lakini MWANAMKE hakuumbwa kutokana na udongo yeye alitolewa kwenye ubavu wa MWANAUME (Mwanzo 2:7, 21-22) kwa hiyo hata kiuumbaji MWANAMKE na MWANAUME wameumbwa kwa namna tofauti.

2)Hakuna MWANAUME anayewaza kama MWANAMKE na hakuna MWANAMKE anayewaza kama MWANAUME hata kama wote wameenda shule. MWANAUME anawaza kwa mpangilio ndiyo maana hakurupuki kufanya maamuzi, lakini MWANAMKE anawaza kwa hisia ndiyo maana wanawake wanafanya makosa mengi kuliko wanaume na wanaongoza kuomba msamaha mara nyingi kuliko wanaume.

👉Kwa mfano kama kungekuwa na mabox ya zawadi 100 halafu akawapa MWANAUME na MWANAMKE wayafungue , MWANAUME atafungua box moja moja lakini MWANAMKE atatamani mabox yote 100 ayafungue kwa pamoja.

👉 MWANAMKE ana Uwezo wa kufanya jambo zaidi ya moja kwa wakati mmoja, unaweza kukuta wanawake salon kwanza wanasuka pili wanaangalia tamuthilia lakini wakati huo huo wanapiga umbea. MWANAUME huwa hawezi yeye ni jambo moja tu ndio atalifanya kwa ubora.

3)Hitaji la MWANAUME namba moja kwa MWANAMKE ni sex, MWANAUME akikosa sex anakuwa mkali, mkorofi kisaikologia anakuwa vibaya na kadiri MWANAUME anavyopata sex hihitaji zaidi kwa ufupi MWANAUME hatosheki na sex. Lakini Hitaji la MWANAMKE namba moja kutoka kwa MWANAUME siyo sex bali anahitaji kujaliwa yeye akifanya sex mara moja anaweza kukaa hata mwezi bila kuhitaji tena na tofauti hii ndiyo chanzo cha migogoro katika ndoa nyingi.


Kwa ufupi hizi ni tofauti chache kati ya nyingi ambazo wanaume na wanaume wanatofautiana tukizijua tutajua namna ya kuchukuliana na kupunguza migogoro. Weekend njema.
wanawake wameumbwa kupokea pia
 
Back
Top Bottom