Mwanamke niliyetegemea kumuoa nimekuta picha zake group la Telegram

Von_Lufuta

JF-Expert Member
Mar 19, 2023
1,530
3,607
Wakuu habari za Jumapili? Kwangu si njema hata kidogo ila nina Imani Kila mmoja ni buheri wa afya.

Nisiwachoshe sana ngoja niende moja kwa moja kwenye mada husika kuhusu yaliyonikuta japo imekuwa ghafla sana kinyume na mategemeo yangu

Ni hivi, mwaka 2019 baada ya kuona mahusiano niliyokuwa nayo na mwanamke niliyewahi kumpenda kupindukia katika maisha yangu na kudumu naye kwa takribani miaka mitano yakielekea ukingoni, niliamua kutengeneza branch kwa kuingia kwenye mahusiano na Binti mmoja mzuri sana Ili kutokubaki empty kipindi relationship na Binti wa kwanza iki-terminate.

Binti wa kwanza nilidhamiria kuwa naye ila baada ya kwenda kusoma kuna mambo yalibadilika sana kwake hivyo ikapelekea kupoteza Imani nae kabisa. Ilikuwa ni bidhaa sealed kipindi naichukua ila ndiyo hivyo tena.

Baada ya kuachana rasmi ilibidi niwekeze nguvu nyingi kwa huyu mwingine ambae hapo awali nilikuwa naye kama basi tu.

Baada ya muda nilijikuta nampenda kupindukia, ni mweupe sana, kimo Cha wastani, umbile zuri na sura yenye mvuto sana.

Kwa namna nilivyomfahamu, kwao maisha ni mazuri tu. Kuna kipindi ilikuwa kweli nakwama kiuchumi ila alinikwamua.

Tumeishi vyema na nimebahatika kukutana nae mara kadhaa na nimemfurahia.

Kiufupi nimetokea kuzama kwake mazima, sijaacha hata kandambili ili mambo yakiharibika waokoaji wajue kuna mtu kazama hapo waniokoe kupitia uwepo wa hizo kandambili.

Tulipofikia ni kuwa mwakani tufunge ndoa tu awe mke kwangu na ndivyo suala lilivyo na baadhi ya watu wangu na wake wa karibu wanalitambua hilo.

Sasa bwana, sijui imekuaje tu. Leo nikiwa katika kuperuzi peruzi kuna link ya group la Telegram niliiona sehemu nikaona isiwe case, nikajoin.

Kwenye magroup mara nyingi huwa natumia namba ambayo watu wangu wa karibu hawana Ili tusije tukakutana huko bahati mbaya kikaumana.

Group lenyewe ni la mademu kujiuza, angalau niopoe pisi ya kuibutua Jumapili ya leo mazingira ya karibu kama ningeipata.

Cha ajabu nimekutana na picha za mwanamke wangu ambae nategemea kufunga nae ndoa mwakani akiwa ameambatanisha na caption ya location alipo zimepostiwa Leo asubuhi..

Imetaja yupo Dar ambapo ndio alipo kwa sasa maana jumatano aliniaga anafuata mzigo wa biashara anayofanya. Picha zenyewe zipo kwenye mazingira ya kimalaya sana.

Mbaya zaidi sio moja, ingekuwa moja angalau ningeilazimisha akili ikatae kuwa si yeye, lakini zipo kama sita na mikao tofauti tofauti inayodhihirisha moja kwa moja ni yeye.

Jumapili yangu imevurugika ghafla sana, sijampigia simu sababu akili haipo sawa. Hata nikimpigia ntaanzaje kumwambia?

Hata nikimwambia, na Mimi nilikuwa natafuta nini huko? Aisee, yaani hata safari zake zote ninazifikiria ni kama alikuwa anaenda kuuza NYONDI tu kwa vijeba.

Kila nikifikiria mazingira yote naona kabisa hapa nimepigwa na square pipe kichwani..

Ina maana Ule ufundi wote alionao ni kwa ajili ya wateja wake?

Mbona sikujua muda wote Ule? Je tayari yupo kwa mteja?

Vipi zile pesa aliniokoa kipindi nipo vibaya kiuchumi?

Nishaurini tafadhali.

Natanguliza shukrani 🙏🙏

Mrejesho wa maongezi nae >
mrejesho wa maongezi nae baada ya kurudi upo page 11
 
Wallah
JamiiForums1464151821.jpg
 
Wewe mnunue na mkutane location.

Hapo ndio utapata cha kuanzia.

Lakini jiandae kujibu swali la "na wewe kwenye group la Malaya wanaojiuza unatafuta Nini", hapo case inakuwa closed huna Cha kumuhukumu ushajua anajiuza acahana nae...
 
Mapenzi ni kitu kinachoumiza sana.

Wengi watakupa ushauri humu wa kumuacha, Mimi nipo tofauti

Usimwambie ongeza upendo, make your plans clear to her, mpende.

if she is destined kutulia atatulia
Hauwezi jua kwingine utakako dondokea kupo vipi.

Pole mkuu, just be normal kama unampenda sana mpambanie na umbadilishe..

watu wanadumu kutokana na uvumilivu mwingi
 
Mapenzi ni kitu kinachoumiza sana....
Wengi watakupa ushauri humu wa kumuacha, Mimi nipo tofauti

Usimwambie ongeza upendo, make your plans clear to her, mpende....if she is destined kutulia atatulia
Hauwezi jua kwingine utakako dondokea kupo vipi...

Pole mkuu, just be normal kama unampenda sana mpambanie na umbadilishe....watu wanadumu kutokana na uvumilivu mwingi
Ni nabii Isaya tu aliniambiwa na Mungu akamuoe Kahaba, hata hivyo hiyo kahaba alimtesa balaa
 
Back
Top Bottom