Kwa hiyo utajibweteka duniani usifanye Kazi kusudi Ili uwe fakiri uwahi kuingia peponi?
Ila kasome nguzo ya tatu ya uislam....kisha jifikirie mara mbili.
Maana ya Zakat
Kilugha:Zakat ni utakaso.Qur’an (91:9)na (87:14).
Kisheria:Zakat ni sehemu ya mali ya tajiri(2.5% au 1/40) anayoitoa kwa kutekeleza amri ya Allah na kuwapa wanaostahiki baada ya kupindukia mwaka iwapo mali hiyo imefikia Nisaabu.
Nisaab:Ni kima cha chini cha mali ambacho mtu akiwa nacho au zaidi yake analazimika kutoa zakat.
1)Inahusiana na utoaji wa mali,
2)Ni faradhi tu kwa tajiri mwenye mali inayojuzu kutolewa zakat iliyofikia Nisaab, 3)Ni wajibu kwa kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake kulingana na haja iliyojitokeza inayohitaji mali au huduma au vyote.
4)Ina kiwango maalumu kama vile 2.5% au 1/40 ya mali inayojuzu kutolewa zakat,
5)Hujuzu baada ya kupindukia mwaka au baada ya mavuno.
Masharti ya Utoaji wa zakat na sadaqat
(i)Kutoa vilivyo halali.
(ii)Kutoa vilivyo vizuri.(Quran 23:51), (2:172),(2:267) na (3:92).
(iii)Kutoa kwa kati na kati.(Quran 2:219) na (17:29).
(iv)Kujiepusha naria na kufuatilia kwa masimulizi.(Quran 2:264) na (2:274).
(v)Kuwapa wanaostahiki.(Quran 9:60).
Makundi ya watu wanaostahiki kupewa zakat(9:60).
(1).Fukara.
(2).Masikini
(3).Wanaozitumikia.
(4).Wanaotiwa nguvu nyoyo zao juu ya Uislamu.
(5).Kuwakomboa watumwa.
(6).Kuwasaidia wadeni kulipa madeni yao.
(7).Katika njia ya Allah(s.w)-Fii sabilillah.
(8).Wasafiri walioharibikiwa njiani(Ibnus-sabiil).
Mali inayojuzu kutolewa Zakat,Nisaab na viwango na Muda
(1)Mazao ya shambani.Qur’an(2:267) na (6:141)
Nisaab –Wasaq tano(5) au kg 666.Kiasi -1/2 wasaq au kg 66.6 yaliyostawishwa kwa mvua.
-1/4 wasaq au kg 33.3 yaliyomwagiliwa.
Muda-Baada ya mavuno.
(2)Wanyama wafugwao
Ngamia:Nisaab-ngamia 5.
Kiasi-Mbuzi 1
Ng’ombe:Nisaab-ng’ombe 30.
Kiasi-Ndama 1 wa mwaka mmoja.
Kondoo:Nisaab-Kondoo 40.
Kiasi-kondoo 1 wa mwaka mmoja.
Mbuzi:Nisaab-mbuzi 40. Kiasi-Mbuzi 1 wa mwaka mmoja. Kiasi-1/40 au asilimia 2.5Muda-Baada ya mwaka.
(3)Dhahabu na vito vya dhahabu
Nisaab-Gramu 82.5 au Tola 7.5Kiasi-1/40 au asilimia 2.5Muda-Baada ya mwaka.
(4)Fedha na vito vya fedha.
Nisaab-Gramu 57.7 au Tola 5.2Kiasi-1/40 au asilimia 2.5Muda-Baada ya mwaka.
(5)Fedha taslim
Nisaab-Sawa na thamani ya Nisaab ya dhahabu au fedhaKiasi-1/40 au asilimia 2.5Muda-Baada ya mwaka.
(6)Mali ya biashara
Nisaab-Sawa na thamani ya Nisaab ya dhahabu au fedhaKiasi-1/40 au asilimia 2.5Muda-Baada ya mwaka.
Wewe ndiye unayehitajika kujitafakari maana bado sana uifahamu dini yako.
Maana hakuna fukara wala masikini mwenye uwezo wa kumiliki ng'ombe 30 au mbuzi 40 na akaitwa masikini.
Wewe andika andika tu unavyoona inakufurahisha ila husihusishe dini kibubusa.