JACKLINE CELESTINE KITALE
Member
- Jul 29, 2021
- 81
- 158
Ni kitu cha kushangaza mpaka leo huu mfumo wa kutoa mahali bado unaendelea. Tumefundishwa tokea tulivyo kuwa shule ya msingi ya kuwa mahali sio nzuri kwa mwanamke, inashusha thamani yake katika ndoa, lakini kwanini bado tunaitumia mpaka leo? Ndoa hutokea pale ambapo watu wawili wanapopendana na kukubaliana kuishi kwa pamoja kama mume na mke.
Baada ya watu hao kukubaliana wanabidi waende kwa wazazi wao ili waweze kupata baraka kutoka kwao. Sasa tatizo ndio huanzia hapa, baada ya wazazi wao kuwatakia baraka ili waanze maisha yao , huanza kuleta mambo yasiyokuwa na msingi wala ulazima kama mambo ya mahali. Wazazi wa mwanamke wanapanga mahali kubwa ambayo mwanaume atatakiwa kulipa ili aweze kukubaliwa kumchukua mwanamke.
Nadhani mpaka hapa unakuwa umeona jinsi ambavyo hii tabia ya kulipa mahali inavyoshusha hadhi ya mwanamke na kama bado naomba nikudadavulie vizuri. Mwanamke anapotolewa mahali Ni kwamba anakuwa kama ananunuliwa. Embu jiulize wewe Kama mwanamke Kama umekubali kuwa mwili mmoja na kuanzisha maisha na huyo umpendaye kwanini yeye akulipie mahali?
Kwanini alipe pesa ili akupate? Na akishindwa kukulipia hiyo mahali maanake atashindwa kukoa huoni hiyo ni kama biashara? Na Muda mwingine familia ya mwanamke wanakubaliana na familia ya mwanaume, kuwa mwanaume huyo amuoe binti yao kwa mkopo atakuwa akilipa kidogo kidogo, yaani hapa ndio unaona mfanano uliopo na biashara za mangi za kila siku. Sasa kwanini wewe ukubali kuwa au kufanywa Kama bidhaa?
Andiko kutoka gazeti la BBC linasema kuwa, “Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinaongoza kwa kuwa na bei kubwa za mahali, na hii ndio sababu kubwa inayofanya vijana wa kitanzania wasiwe na ndoa rasmi (vijana wengi wanaamua kuchukuana tu na kuishi pamoja bila hata kuoana). Na mahali huwa kubwa kutegemeana na rangi ya mwanamke, mwanamke mwenye rangi nyeupe hutolewa mahali kubwa kuliko mweusi, Na pia ukubwa wa mahali unategemeana na elimu ya mwanamke, kama mwanamke amesoma sana basi mahali yake itakuwa kubwa zaidi zaidi ya ambaye hajasoma Sana au hajasoma kabisa”.
Na mchambuzi wa maswala ya kijamii kutoka Tanzania, Betty Masanja anasema, “Suala zima limegeuzwa na kumfanya mwanamke kuwa chombo au bidhaa tu”. Wazazi wametuzaa na kutulea sawa hatukatai lakini haiwapi wao mamlaka ya kutumia sisi watoto wao hasa watoto wa kike kama mitaji ya wao kujipatia pesa. Ya kwamba watampa mtoto wao kwa mwanaume yeyote atakaye weza kutoa mahali waitakayo.
Najua Kuna watu ambao bado watakuwa kinyume na mimi kuhusu hili swala la mahali, hasa wanawake, ambao huamini kuwa mahali huwapa wao thamani, na kadri mahali inavyokuwa kubwa ndio mwanamke huonekana kuwa na thamini kubwa, kitu ambacho sio kweli. Kwa wanosema kuwa mahali Ni nzuri kwa mwanamke naomba ujiulize haya maswali mawili
Kwanini mahali ipangwe? Tena ipangwe na familia ya mwanamke ? Kama mahali Ni zawadi tu amabayo inatolewa na mwanaume kwa familia ya mwanamke kama shukrani, kwanini ipangwe na familia ya mwanamke? Kwasababu kama shukrani inatakiwa familia ya mwanaume ndio iandae, wajipange wenyewe waone ni kiasi gani walicho na uwezo nacho au watoe samani gani. Sasa kwanini ipangwe?
Kwanini ilipwe na upande mmoja? Na kama mahali Ni shukrani kwanini familia ya upande wa wanaume tu ndio unalazimishwa kutoa? Kwani familia ya mwanamke haitakiwi kushukuru familia ya mwanaume kwa kumlea mwanaume huyo ambaye anaenda kumuoa binti yao?
Nadhani utakuwa umepata mwanga kidogo kuhusu Jambo hili baada ya kujiuliza swali. Najua kaka zangu mtakuwa mnaona kuwa hili sio tatizo lenu, naomba niwaambie kuwa hili tatizo Ni la kwenu pia na tena nadhani hili tatizo huwaumiza wanaume sana kuliko hata wanawake.
Ebu fikiria wewe kijana umebarikiwa kupata mwenza wako na mkaamua mfunge ndoa , Sasa kijana mdogo anaambiwa na familia ya mwanamke atoe mahali ya shilingi laki moja au milioni atazitoa wapi. Na kwa nyakati hizi vijana wengi wanakuwa bado wanatafuta maisha, hawana nyumba wala, mali nyingi, kitendo cha kumwambia atoe pesa ili apate mke unakuwa unamwonea na kumuumiza Sana. Na ndio maana vijana wengi wanaamua wasioe, wanaamua tu kuishi pamoja .
Sasa huoni kuwa tunakuwa tunasababisha vijana wengi kufanya uzinzi? Kwasababu kufanya tendo la ndoa bila kuwa katika ndoa ni nini Kama sio uzinzi?
Ukiachana na kushusha hadhi ya mwanamke, hili tatizo la mahali linachochea kama sio kuwa chanzo cha tatizo la wanaume kupiga wake zao: unajua mtu ukitoa pesa kupata kitu unakuwa na mamlaka nacho na uchungu nacho sana, na ndivyo inavyokuwa kwenye ndoa mwanaume anapotoa mahali.
Mwanaume anamtolea mwanamke mahali alafu wakiwa katika ndoa mwanamke anakuwa hamsikilizi au anapingana na kile anachokisema na akienda kutoa kwa taarifa kwa wazazi hapati msaada wowote , unategemea nini kitakachofuata hapo Kama sio kipigo? Sio kwamba ninai halalisha hii tabia la hasha. Mimi ninaichukie na kuipinga vikali, lakini kama tunataka hili tatizo la kupiga wanawake liishe, tuache kuwaumiza hawa wanaume kwa kuwalazimisha watoe mahali.
Wanawake naomba tutambue kuwa tunathamani sana, na thamani hiyo haiwezi kupimwa au kulinganishwa na pesa yeyote ile. Wewe unathamani kuliko mamilioni au mabilioni ya pesa hivyo usikubali kulinganishwa hivyo. Tusikubali kutolewa mahali kwa maana hii inatushusha thamani yetu sisi Kama wanawake. Tupate muda tukae na wazazi wetu kuongea nae ilituone jinsi mtazamo wao ulivyo na kwa upendo tuweze kuwaeleza upande wetu.
Natumaini kama wazazi ambao wameelimika na kutupenda watatuelewa. Na ili hili tatizo liweze kutatuliwa inabidi watu wa jinsia zote mbili watambue kwanza kuwa hili ni tatizo la wote na sio la wanawake tu. Na kwa pamoja tukiungana tunaweza kulitatua hili tatizo.