Vunja agano na mchumba uliyeachana naye(kutoka kwa Peter Mabula)

Showio

JF-Expert Member
May 16, 2019
255
481
VUNJA AGANO NA MCHUMBA ULIYEACHANA NAYE.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Jifunze kitu kwenye ujumbe huu.
Baadhi ya Vijana na mabinti hupata wachumba kisha baada ya muda wanaachana kabla ya ndoa.
Baadhi ya wanawake single na wanaume single hupata wachumba kisha kabla ya ndoa wanaachana.

Sasa katika ujumbe huu jifunze wewe uliyewahi kuwa na mchumba kisha mkaachana.
Hata Kama kwa sasa uko katika ndoa lakini kama kabla hujaingia katika ndoa uliwahi kuwa na mchumba kisha mkaachana basi jifunze kitu.
Hata Kama uko kwenye ndoa ya miaka 30 ila kabla ya ndoa uliwahi kuwa na mchunba kisha mkaachana nisikilize itakusaidia.

Sitaki leo kuzungumzia sana chanzo cha wewe kuachana na mchumba huyo maana inawezekana ni kwa sababu ya matatizo yake yeye, au uligundua ana tabia mbaya au tabia chafu, au ni wakala wa shetani wa siri au labda tatizo ni wewe n.k.
Ninachotaka kusema ni kwamba kuachana na mchumba huyo sio tatizo lakini tatizo linaweza kuwa ni agano uliloingia na mtu huyo, ndugu hakikisha kwa maombi unavunja agano hilo kati yako na yeye, hata kama alishaingia kwenye ndoa sasa.
Hakikisha unafuta agano kati yako na yeye.

Agano ni nini?

Agano ni mapatano kati ya pande mbili au kati ya watu wawili.

Hivyo vile vilivyopatana naye, mkaapiana, mkaingia mikataba ya maneno vinaweza kuwa agano baya kwenye ulimwengu wa roho na agano hilo likakutesa hata kama mlishaachana miaka mingi sana iliyopita.
Watu wengi wanateswa na maagano ya mahusiano ya zamani.
Isaya 57:8 "Na nyuma ya milango na miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua nafsi yako kwa ajili ya mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua kitanda chako, nawe umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo ulipokiona."

Agano huwa linaishi hadi siku linafutwa, agano lisipofutwa litendelea kuishi na kufanya kazi, kama ni agano halihitajiki litakusumbua sana.

Hata Kama ni agano la kibinadamu na ni la kawaida tu, hili agano bila damu ya YESU KRISTO huwezi kulifuta, hivyo linaweza kukutesa.

Wagalatia 3:15 "Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno."

Sasa kwanini ulifute agano baya?
Ni kwa sababu hilo agano halihitajiki sasa na linaweza kukuvunjia ndoa yako ya sasa.

1 Wathesalonike 5:22 "jitengeni na ubaya wa kila namna."

Agano hili uliingiaje?
Kwa kukubaliana kutokuachana, kukubaliana kuoana, kuapiana kwamba mtakuwa pamoja daima na kila mambo mliyoyafanya mkithibitisha kwamba mtaoana au humtaachana.

Kama mliingia na katika dhambi ya uasherati hapo ndipo hatari zaidi maana hapo mliingia maagano ya kishetani mawili, agano la makubaliano na agano la dhambi chafu ya uasherati.
Warumi 6:16,18 '' Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.''
Biblia inasema jambo muhimu kwamba ni heri kuikimbia zinaa. uzinzi au uasherati ni zinaa na tukio hilo ni kuingia agano la kipepo, ni Kuwa mwili mmoja na roho chafu ya kikahaba, ni agano la kipepo linaloweza kumfuatilia mtu na kumharibia.

Ngoja nikuonyeshe baadhi tu ya madhara yanayowapata watu ambao wako kwenye ndoa sasa ambapo maagano hayo yanatokana na wachumba wa zamani na sasa maagano hayo yamewashikilia kipepo.

1. Mara kwa mara unaota uko na mchumba wa zamani, unaota unafunga nae ndoa, unaota yeye ndio mwenzi wako sasa wakati kiuharisia mlishaachana miaka mingi iliyopita na kwa sasa yeye alishaingia kwenye ndoa yake na wewe uko kwenye ndoa yako.

Au mlishaachana muda mrefu uliopita na yeye sasa yuko katika ndoa huku wewe umebaki kumuota na amekosekana wa kufunga ndoa na wewe maana agano hilo la kipepo la zamani linawazuia watu sahihi kufunga ndoa na wewe.

Ukiona hivyo ujue agano hilo la kipepo kati yako na mtu huyo halijavunjika. Na kama likiendelea kuwepo litakuharibia ndoa yako kama uko kwenye ndoa, hata kama hauna ukaribu wala uhusiano na mchumba huyo wa zamani.

Kama hujafunga ndoa tambua kwamba huyo unayemuota ndotoni ndiye kukushikilia kipepo, hata kama yeye hajui chochote lakini lile agano yaani makubaliano kati yako na yeye, hayo makubaliano yamesimama kwenye ulimwengu wa roho kukushikilia.
Mimi Peter Mabula ni shuhuda nyingi juu ya hili ndio maana nakueleza haya leo ili ujitenge na kila agano linalokushikilia sasa linalotokana na uhusiano wa zamani.

2. Kujikuta kila mara unamuwaza mchumba wa zamani, unatamani ungefunga ndoa na yeye hata kama alikutenda vibaya na mkachana naye ndio ilikuwa heri kwako.

Hali hili inachochewa na agano la kipepo kati yako na yeye, hivyo futa agano hilo kwa maombi katika jina la YESU KRISTO.
Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."

Kama hajaingia katika ndoa unaweza kujikuta kila ukipata mchumba unamwacha ghafla bila sababu, kumbe umeshikiliwa na agano la kipepo la mchumba wa zamani.
Kama uko kwenye ndoa utajikuta unatamani ndoa yako ife, ni hatari sana.

3. Bila sababu unajikuta humpendi mwenzi wako wa sasa.

Yaani hata ukiulizwa kwanini kwa sasa unamchukia mume wako au mke wako hata hujui ni kwanini ila ukweli unamchukia sana hata unatamani muachane au unatamani hata afe ili ufunge ndoa na mwingine, unatamani kumsaliti n.k
Ndugu huko ni kushikiliwa na agano la kipepo la zamani, ni kuvamiwa na nguvu za giza kwa kiwango cha juu sana.

4. Mchumba wa zamani kumuona ni wa kipekee sana kuliko uliyenaye kwenye ndoa sasa.

Ukweli ni kwamba huyo wa zamani hana ukipekee wowote ule ila agano la kipepo kati yako na yeye ndilo limekupumbaza hata uone kwamba yeye ni mtu wa kipekee, ukikaa vibaya shetani ataivunja ndoa yako.

5. Kujikuta unatamani kuwasiliana nae kwa siri, unatamani uongee nae kwa simu, unatamani atokee na kukukumbatia.

Hiyo yote ni nguvu ya agano la kipepo kati yako na yeye, hivyo futa agano hilo la kipepo kati yako na yeye.
Kama una mawasiliano naye futa na jitenge mbali naye maana hakuhusu kwa lolote lile sasa.
wewe una maisha yako na yeye ana maisha yako hivyo achana naye.
Mpende mke wako wa ndoa au mume wako wa ndoa na umpe heshima yake stahiki.
Vunja agano la kipepo na mchumba wa zamani.
Hata kunaweza kuwepo maagano ya zamani kutoka kwa watu 20 tofauti uliowahi kuwa na mahusiano nao, vunja maagano na wote hao, vunja kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.

6. Unapomuona Mchumba wa zamani ni bora kuliko mwenzi wako wa ndoa ambaye uko naye sasa.

Hiyo ndio kazi ya shetani yaani kuharibu.
Yohana 10:10 "Mwivi(Shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; ........"

Unamuona mchumba wa zamani ni bora kuliko mume wako au mke wako wakati ukweli ni kwamba kwa sasa upo na mtu bora zaidi ila agano la kipepo kati yako na mchumba wa zamani ndilo linakuharibia.

Nimewahi kuongea na watu wengi sana ambao walikuwa wanahitaji msaada wa maombi, wengi wao nikigundua maagano ya kwanza kwenye mahusiano ya uchumba uliokufa ndio yanawatesa.
Dada mmoja kila akipata mchumba uchumba unaishia njiani, lakini ndoto zake kila mara anaota anaolewa na mchumba wa zamani ambaye kwa sasa ana mke na watoto.
Dada huyu hakujua maana ya ndoto hiyo kumbe agano la kipepo kati yake na mwanaume huyo ndilo linamshikilia hivyo tulipofuta agano hilo ndipo akapata mume na kuolewa.

Mama mmoja siku moja alinipigia simu akiniambia kwamba mume wake ni tajiri na mwanaume huyo anamuonyeshe upendo wa ajabu mama huyo lakini mama huyo akili yake iko kwa mchumba wa zamani waliyeachana zamani sana na huyo mchumba ana mke na watoto.

Dada mmoja alipata mchumba, mara ya kwanza alifurahi na mahari akatolewa lakini siku chache kabla ya kufunga ndoa yeye mwenyewe akawaambia wazazi wake na Kanisa kwamba hataki kuolewa, watu wote walimshangaa na hata alipoulizwa kama wamekosana na mchumba wake akasema hakuna, wakamuuliza kama amepata siri yeyote mbaya kuhusu mchumba wake au familia akasema hamna. Wazazi wake waliumia na kumtukana sana maana walikasilika huu ya yaliyotokea siku chache sana kabla ya ndoa.
Binti huyo aliwaambia warudishe mahari waliopokea, Kamati ya harusi ilishanunua hadi vitu lakini kamati hiyo inatakiwa ivunjwe maana Bibi harusi ghafla tu hataki kuolewa.
Familia zote mbili walikataa vikao vingi ili kumbadili huyo binti lakini ilishindikana, hata yeye akiulizwa kwanini anavunja uchumba huo katika mazingira ya mwisho ili kufunga ndoa hakuwa na jibu.
Wazazi walimwambia "Si ni wewe ulikuja kumtambulisha kwetu kijana huyu mbona unabadilika wakati ndoa imefika? " Binti alisema hata yeye hajui ila hataki tu kufunga ndoa.

Binti huyo kila mtu alishangaa kuanzia wazazi, wakwe, watumishi wa MUNGU, Kanisa, Ndugu, majirani na jamii nzima.
Yeye akabaki akilia tu.
Alinipigia simu akisema "Mtumishi Mabula nisaidie maana mchumba wangu nampenda sana na kila kitu kiko tayari kwa ajili ya kufunga ndoa, hakuna tatizo lolote ila ghafla tu mimi sitaki kufunga ndoa" Nilimshauri kwa uchungu na ukali lakini nikagungua agano la kipepo kati yake na mchumba wa zamani ndilo limemshikilia kipepo, waliapiana kwamba hawajaachana kamwe na binti alimwambia mwanaume yule kwamba hataolewa na mwanamume mwingine yeyote nje na kijana huyo, kumbe lilikuwa agano la kipepo.
Ndugu, leo kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO vunja maagano yote mabaya kati yako na uliowahi kuwa na uhusiano nao wa kimapenzi au kiuchumba.

Kama mlikutana hadi kimwili na mchumba wa zamani ndio hatari zaidi.
Futa maagano ya kimakubaliano kati yako na yeye na futa pia agano la dhambi ya uasherati mliofanya.
Mithali 6:32-33 ''Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. ''

Biblia inasema anayezini hana akili kabisa yaani hana akili zote, hana akili hata moja.

Unaweza kuwa wewe sasa ni mama mtu Mzima lakini mume wako hajatulia katika ndoa yenu kwa sababu yuko kwenye agano la kipepo na wanawake wengine.

Unaweza kuwa wewe ni Baba na ndoa yako ina miaka zaidi ya 20 lakini usiku na mchana mke wako akili yake iko kwa mchumba wa zamani, upendo kwako hana hata kidogo ila huwa anajilazimisha tu.
Kumbe yuko katika agano la kipepo na mtu wake wa zamani na agano hilo limeleta hadi agano lingine na majini mahaba, ni hatari sana maana ndio inaweza kujikuta kwenye migogoro ya kudumu.

Inawezekana wewe hakuna anayetaka kufunga ndoa na wewe kwa sababu umeshikiliwa na agano la kipepo kati yako na mtu wako wa zamani.
Unaweza ukaachana na mtu na ukawa huna mawasiliano naye lakini kama agano kati yako na yeye hujafuta ujue kubaliano hilo litakutesa.

Nini ufanye?

1. Tubu kwa makosa yako ya kuingia makubaliano yeyote kati yako na mchumba wa zamani au wachumba wa zamani Mlioachana.

Zaburi 51:1-2 " Ee MUNGU, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima."

2. Kwa maombi futa kila agano la kimahusiano nje na mwenzi wako wa ndoa.

Isaya 28:18 "Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo."

3. Vunja uhusiano wowote kati yako na mchumba wa zamani maana sasa hakuhusu tena, futa namba yake ya simu na kama ni yeye anakupigia mpe mkeo au mumeo apokee simu hiyo.

Zaburi 1:1 "Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha."

4. Ongeza upendo kwa mwenzi wako wa ndoa ambaye uko naye maana ni huyo tu MUNGU amekupa.

Waefeso 5:22-25 " Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii BWANA wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama KRISTO naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo KRISTO vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama KRISTO naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;"

5. Futa madai yote ya nguvu za giza kuhusu ndoa yako.

Warumi 8:33 "Ni nani atakayewashitaki wateule wa MUNGU? MUNGU ndiye mwenye kuwahesabia haki."

6. Jiombee kibali kwa mwenzi wako wa ndoa na muombee na yeye apate kibali cha kudumu moyoni mwako.

Mithali 18:22 "Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA."

7. Iombee ndoa yako ili idumu.

Zaburi 140:4 "Ee BWANA, unilinde na mikono ya mtu asiye haki; Unihifadhi na mtu wa jeuri; Waliowaza kuzipotosha hatua zangu."

8. Kama umefungwa na nguvu za giza jifungue kwa maombi katika jina la YESU KRISTO, kama ni mwenzi wako pia mfungue kwa maombi.

Mathayo 7:8 "kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."

9. Itolee sadaka ndoa yako na ikabidhi kwa MUNGU.

Zaburi 50:5 "Nikusanyieni wacha MUNGU wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu."

10. Kama una tabia mbaya au una mawazo mabaya acha tabia hiyo na futa mawazo mabaya, Muombee pia na mwenzi wako ili aache tabia mbaya na yafute mawazo machafu ndani yake, iheshimuni ndoa yenu.

''Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu-Waebrania 13:4''

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.

Bwana YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.

Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.

Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.

Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.

Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
 
We upendi kupasha kiporo?kula maisha we bado kijana mdogo unajipa majukumu yasiyo yako Kula bata kula mali ponda totoz
 
Kumbe maagano ya mdomoni ya nguvu kiasi hiki? Yesu wangu nirehemu, navunja maagano hote nnayoyakumbuka na nisio yakumbuka
Maneno ni hatari sana huumba nakudumu kumbuka hata Dunia Mungu aliiumba kwa kutamka maneno tu
 
Nimesoma yote. Ubarikiwe mtumishi. Swali langu je naweza kuvunja maagano yakale hali yakuwa nipo nampenzi mwingine ila sio mke?
 
Ukishaona Waebrania,Waefeso,Walawi,etc etc etc...jua..

Huyo jamaa anaitwa Mungu has fvcked up all your brains!

Huyo jamaa Mungu kujenga hivi vitabu na kuweka namba kibaoo,is causing alot of trouble in this world!
 
Back
Top Bottom