Mwanamke mfupi mwembaba vs mrefu mnene

Mwanamke mfupi mwembaba vs mrefu mnene

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Kuna wakati maumbo ya miili ya binadamu yanakuwa yanachangia sana kujenga usugu au kurahisisha baadhi ya mambo kufanyika kwa urahisi au ugumu kwenye eneo fulani la maisha yake

Kwenye suala na mahusiano hasa ya kwenye ndoa ni muhimu kujua hili ili kuepuka matatizo ambayo hayana ulazima

Kuna ka utafiti kamefanyika ambako sio rasmi sana kihivyo lakini kanaweza kuwasaidia watu kupata baadhi ya majibu ya maswali waliyokuwa wanajiuliza siku nyingi

Najua kuwa yameshawahi kusemwa mengi sana kuhusiana na maumbile ya mwili lakini sidhani kama yamewahi kuongelewa kwa namna ambayo nakwenda kuzungumzia

Yaliyoongelewa nadhani ni yale ambayo yanahusu kwenye kitanda zaidi kuliko kwenye mambo mengine,mimi nitakwenda kuzungumzia kwenye mambo mengine zaidi tofauti na kitandani

Matokeo ya ka utafiti hako yanasema kuwa mwanamke ambae ni mfupu halafu mwembamba mara nyingi anakuwa na tabia zinazoweza kusababishwa na umbo lake hili

Baadhi ya tabia ambazo mwanamke anakuwa nazo mwenye umbo hilo ni kama ifuatavyo



Msemaji sana
​
Inasemekana uwa mwanamke ambae ni mfupi na mwembamba anakuwa ni mwepesi sana kwenye mdomokitendo ambacho wanaume wengi hawakipendi kwani wanaume wameumbwa kusema machache na wasingependa sana kubishiwa hasa kwa sauti kubwa

Mwanamke ambae ana umbo la namna hii inaonekana ni mwongeaji sana na sio anaekubali kushindwa mara nyingi,kitendo hicho kinamfanya aonekane mkorofi sana hivyo kumfanya asiweze kupata baadhi ya fursa nyingi

Tabia hii inaelezwa na baadhi ya wanasaikolojia kuwa inasababishwa na na kitendo cha mwanamke huyo kutokujiamini kulikosababishwa na kutokujikubali kwa namna alivyo kwani jamii nyingi zinamchukulia mwanamke mfupi kama "asiefaa" hivyo kumpa wakati mgumu sana kujikubali kitendo ambacho yeye anamuangalia kila anaejaribu kutokukubaliana nae kwenye jambo fulani kuona kama anamnyanyapaa


Mzurulaji​
Mwanamke ambae ni mfupi na mwembamba inadaiwa kuwa na ka tabia ka kupenda kutembea sana,hii nayo ni aina ya tabia ambayo baadhi ya watafiti wanasema kuwa inasababishwa na umbo la mhusika,watafiti hao wanasema kuwa mwanamke ambao ni mnene au mwenye umbo ambalo linakaribia unene ni mvivu sana kutembea na hata kuongea sana,jambo hilo linawafanya waonekane kama wanaofaa sana kuolewa lakini hilo ni tofauti kwa hawa wa umbo la ufupi na wembamba

Miili ya hawa wembamba na wafupi inaonekana kama ni sababu tosha ambayo inaweza kuwafanya wakawa na hiyo tabia japokuwa inasemwa kuwa malezi nayo yanachangia kwa kiwango kikubwa sana

Tabia hiyo imekuwa ikiwafanya wanawake hao kuonekana kama wasioweza kuwa wake wanaofaa sana kwani hakuna mwanaume atataka kuingia kwenye ndoa na mwanamke wa aina hiyo kwani haipendezi


Kwa uchache ni hizo na ngoja niishie hapo kwani mada itakuwa ndefu sana na kuwachosha wasomaji lakini kuna sifa nyingi sana ambazo zinawahusu hawa wanawake wa aina hii,sifa ambazo zinaonekana ni kikwazo kwao kwenye mahusiano ya kindoa

Lakini pamoja na hayo hii haina maana kuwa kila mwanamke mwembamba na mfupi anaingia kwenye kundi hili lakini wengi wao wako hivyo!

​
 
Utakuwa mrefu halafu mwembamba tu wewe .....

Hilo ni suala lingine bibie
Hebu tujadili kwanza hilo!

hahahaha nimeuliza tu jamani lol back to the topic watu wafupi huwa hawajiamini bila kujali jinsia na wembamba au unene wake waongeaji sana (wana gubu) hawakubali kushindwa kirahisi kuepuka dharau
afu hapo kwenye uzuralaji na kutembea sana umeaanisha kutembea kawaida au ukicheche
 
Ufupi unaouzungumzia hapa ni upi? Yaani mfupi ukiwa umemlinganisha na nani? Au unazungumzia vipimo vipi? Naomba unijibu pengine naweza kutoa ushahidi wa uliyoyasema
 
Mi najua tu mimi ni mwanamke mzuri afu mwema. Mengine mtajazia. Mara sijui ndo sony wega, miguu kama mikono, pua kama ngumi, nywele kama mbigili. Mtajipanga sana na ndo paw haniachi miaka laki nane.

cc Kongosho
 
Last edited by a moderator:
huu utafiti nauwona kama una ukwel ndan yake
 
hahahaha nimeuliza tu jamani lol back to the topic watu wafupi huwa hawajiamini bila kujali jinsia na wembamba au unene wake waongeaji sana (wana gubu) hawakubali kushindwa kirahisi kuepuka dharau
afu hapo kwenye uzuralaji na kutembea sana umeaanisha kutembea kawaida au ukicheche

Nimemaanisha kutembea kawaida!
 
Mi najua tu mimi ni mwanamke mzuri afu mwema. Mengine mtajazia. Mara sijui ndo sony wega, miguu kama mikono, pua kama ngumi, nywele kama mbigili. Mtajipanga sana na ndo paw haniachi miaka laki nane.

cc Kongosho
Habari ya siku?
Mzima lakini wewe?

Long time ujue .....!!
 
Mambo mengine yanachosha jamani. Yaani kila siku wanawake kila siku wanawake.....
 
Aisee ni kweli.sio wanawake tuu na wanaume pia.wapo kama wana inferior complex.yani wanajua kujidefend kwa maneno kama chiriku.kwa uzururaji hapo kweli.cha kuongezea pia wanawivu na mashindano kwenye kila kitu.
 
Back
Top Bottom