Mwanamke: Kabla hajatoa tamko la kufunga ndoa usimwambie haya…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,810
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,810 2,000

Katika maisha wote tuna siri zilizotuzunguka na mambo mbalimbali ya kifamilia pengine yanayotia kinyaa ambayo huwa tunatamani yasijulikane kwa wengine au labda yafutike kabisa. Lakini inategemea unayachukuliaje mambo hayo au yanaathiri vipi mitazamo yako kuhusu wewe. Ukweli ni kwamba hatuwezi kuyabadili labda tunachoweza kufanya ni kubadili mitazamo ya wengine kuhusu yale yaliyotuzunguka…………Familia yenu ni ya vurugu tupu:
Baba yako ni mlevi kupindukia au baba yako na mama yako wote ni walevi kupindukia. Kaka zako ni mateja au dada zako wote wamezalia nyumbani au waliwahi kuolewa na kuachika, na sasa wako nyumbani tu wakichapa umalaya na pengine wanaendelea kuzalia nyumbani. Haya ni mambo ambayo hupaswi kuyazungumzia kwa mpenzi ambaye hajatoa tamko la kutaka mfunge ndoa. Kwani itamfanya mpenzi mpya atengeneze tafsiri tofauti kuhusu wewe.Uhusiano wako wa mwisho na mwenzi wako ulivunjika kwa vurugu:

Inawezekana mpenzi wako wa kwanza mliachana kwa vurugu kubwa, kwa mfano ulifikia hatua ya kufanya jaribio la kunywa sumu kutokana na kugombana kwenu kabla ya kuachana kwenu. Haya ni mambo ambayo hupaswi kuyasema kwa mpenzi wako mpya, kwani utampa maswali mengi sana ya kujiuliza juu yako.

Idadi ya wapenzi uliowahi kuwa nao:
Kuwa na idadi ndogo au kubwa ya wanaume uliowahi kuwa na uhusiano nao haimaanishi kwamba wewe ni mzuri katika mapenzi, sana sana unajidhalilisha tu.Maisha yako ya ujanani ya kujirusha:
Maisha yako ya ujanani au ulipokuwa shule ukijirusha kwenye kumbi za starehe ni ya kwako na si vyema uyapigie upatu kwa mpenzi mpya ili akujue kwamba na wewe hauko nyuma katika mambo ya starehe.
Ushawahi kuishi maisha ya kutangatanga:

Ni kumbukumbu yenye kuumiza hisia pale ukumbukapo maisha yako ya utotoni kama yalikuwa magumu na machungu. Kulelewa na wazazi wasiojali na watesaji, kuishi kwa kutangatanga kutoka nyumba moja hadi nyingine kutafuta hifadhi kutokana na kunyanyaswa. Kubakwa au kuishi maisha ya vurugu katika familia. Haya ni matukio ambayo yameshapita na hayatakiwi yatawale fikra zako tena. Umeshakua mtu mzima na maisha yanasonga mbele. Kuanza kumsimulia mpenzi mpya kuhusu aina ya maisha uliyokulia kama yalikuwa ni ya taabu kama nilivyoeleza hapo juu kutamfanya akuone kama wewe utakuwa unatonesheka kihisia haraka kutokana na kujeruhiwa kihisia utotoni. Mpenzi anaweza kukukwepa na hatimaye kukukimbia.

Nitaendelea kudadavua siku zijazo……..
 
gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
18,135
Points
2,000

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
18,135 2,000
Mtambuzi sikubaliani kabisa na wewe katika haya, kwa mtu yyte ambaye anapenda kuwa na maisha mazuri yenye heshima basi hupenda kuambiwa kila jambo liwe baya ama zuri prio to event kwani kuambiwa itakupa guts nzuri za wewe uingieje humo.

nijuavyo mm huwez kumwambia mtu ambaye bado hujui hatima yenu itakuwaje, ila unapaswa umwambie yule ambaye tayar maisha yameshakuwa defined.

nikigundua ulinificha jambo u gonna pay for that esp, aina ya familia, na past life yako
 
Last edited by a moderator:

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,810
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,810 2,000
Mtambuzi sikubaliani kabisa na wewe katika haya, kwa mtu yyte ambaye anapenda kuwa na maisha mazuri yenye heshima basi hupenda kuambiwa kila jambo liwe baya ama zuri prio to event kwani kuambiwa itakupa guts nzuri za wewe uingieje humo.

nijuavyo mm huwez kumwambia mtu ambaye bado hujui hatima yenu itakuwaje, ila unapaswa umwambie yule ambaye tayar maisha yameshakuwa defined.

nikigundua ulinificha jambo u gonna pay for that esp, aina ya familia, na past life yako
sasa unakubaliana na mimi au unapingana na mimi?

Nimesema kama ulivyosema hapo kwenye bold, kwamba kabla hajazungumzia hatma ya uhusiano wenu basi usianze kuzungumzia hayo niliyoyasema.....

dada vipi leo, au ushapata DOMPO nini?
 
Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Messages
28,263
Points
2,000

Eiyer

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2011
28,263 2,000
Kimsingi hapa kuna ukweli mkubwa sana.
Kumwambia mambo "muhimu" mtu ambae haujui mtakapoishia ni tatizo kubwa
Lakini kama kuna ndoa mmepanga ni jambo jema kuwa muwazi

Ila malezi na mazoea yanatusumbua sana,kama tukiweza kwenda kinyume na haya angalau kidogo tutawdza kuondoa "visirani" vingi sana maishani mwetu!
 
Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,810
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,810 2,000
Kimsingi hapa kuna ukweli mkubwa sana.
Kumwambia mambo "muhimu" mtu ambae haujui mtakapoishia ni tatizo kubwa
Lakini kama kuna ndoa mmepanga ni jambo jema kuwa muwazi

Ila malezi na mazoea yanatusumbua sana,kama tukiweza kwenda kinyume na haya angalau kidogo tutawdza kuondoa "visirani" vingi sana maishani mwetu!
Afadhali wewe umenielewa...

Ni vyema ikaeleweka kwamba mpenzi ambaye bado hajatamka kusudio lake ya kutaka mfunge ndoa, si vyema kuanza kusimulia hayo niliyoyaeleza pengine na mengine ambayo nitayaeleza hapo baadae kwa kadiri nitakavyopata muda.

Ni bahati mbaya sana kuna baadhi ya wanawake hudhani kwamba kwa kusimulia masaibu aliyopitia utotoni, maisha ya vurugu ya familia yao au jinsi alivyoachana na mmpenzi wake kwa vurugu kubwa kutasababisha amvute huyo mwanaume ili ampende na labda atoe tamko la kufunga ndoa mapema.

Hiyo itakuwa ngumu, wanaume wanachkua tahadhari sana kuhusu familia ya mwanamke na maisha aliyopitia....
kwa kusema hayo ni sawa na kumfukuza asirudi tena..!
 
King'asti

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
27,725
Points
2,000

King'asti

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
27,725 2,000
Mie kabla hata ya first date, wakati tunaanza kuangaliana kwa macho ya paka na thamaki (ndo maana hata samaki akaangwe hafumbi jicho kwa kumuogopa nyau), naweka yoote mezani. Yaani ajue kabisa binti mtambuzi hazimtoshi, haoneleki na ana dingi anapenda vidosho (ile siri unamtegea maza kulea usiku siitaji). Yaani kabla hajayavulia nguo lazma ajue kabisaaa. Na wala siogopi, kwa sababu nahitaji from the word go, mwanaume anaejiamini na anaejijua anaweza kuishi popote na yeyote. Kama ni mwanaume anaeogopa ulevi wa babangu hanifai, manake atashindwa hata kunishauri na kunisaidia ili nimsaidie babangu. So hata dirty family secrets (we all have them jamani, za baba mdogo kutembea na mwanae ama mkamwana wake) mie namwagaaaa! Akiniona najikaribisha lwa huyo ba mdogo si atanilindia humohumo!
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Messages
10,476
Points
1,225

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined Jul 24, 2008
10,476 1,225
Aksante Baba yangu kwa bandiko hili.

Da King'asti aksante kwa post yako. Kusema ukweli ninatamani sana kama maisha ya past au family secrets zisingekuwa na muingiliano wowote na mahusiano yetu ya wakati huu. Yaani ninatamani sana but kwa bahati mbaya haiwezekani. Mimi nilikuwa kama Da King'asti katika suala zima la ukweli na uwazi unfortunately kilichokujanitokea katika uhusiano wangu ambao ulikomaa na kufikia kiwango cha ndoa na mtoto nilikuja kujuta kwani ilipofikia wakati wa ugomvi all the family secrets zilianikwa hadharani katika vikao vya familia kama nguo mbichi juani, tena with all those statements za.......Yes aliniambia, we si ulisemaga......tena uliniapia e.t.c.......kutokana na hili kusema ukweli nimeresout to tell only few, tena zile ambazo unahisi iko siku mtakutana nazo katika maisha yenu, lakini zile za sijui Ba mdogo alimbaka au alitembea na mwanae au sijui Baba alitembea na ma mdogo nitakufa nazo aisee, kwanza najua kabisa huyo baba mdogo hatowezanibaka!
 
Last edited by a moderator:

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,214
Points
2,000

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,214 2,000
Mtambuzi usemayo ni kweli kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaa nakuunga kichwa mikono hadi miguu loh.......

my dear King'asti hizo siri ndo zitakuwa fimbo yako ya kukuchapia........
Mie kabla hata ya first date, wakati tunaanza kuangaliana kwa macho ya paka na thamaki (ndo maana hata samaki akaangwe hafumbi jicho kwa kumuogopa nyau), naweka yoote mezani. Yaani ajue kabisa binti mtambuzi hazimtoshi, haoneleki na ana dingi anapenda vidosho (ile siri unamtegea maza kulea usiku siitaji). Yaani kabla hajayavulia nguo lazma ajue kabisaaa. Na wala siogopi, kwa sababu nahitaji from the word go, mwanaume anaejiamini na anaejijua anaweza kuishi popote na yeyote. Kama ni mwanaume anaeogopa ulevi wa babangu hanifai, manake atashindwa hata kunishauri na kunisaidia ili nimsaidie babangu. So hata dirty family secrets (we all have them jamani, za baba mdogo kutembea na mwanae ama mkamwana wake) mie namwagaaaa! Akiniona najikaribisha lwa huyo ba mdogo si atanilindia humohumo!

MwanajamiiOne, natumaini King'asti atakusoma na kukuelewa hapa, mara nyingi hawa wapenzi wakikujua ndani nje wanazitumia siri hizi kama njia ya kukucontrol au kukuumizia, boyfiriend sijui mchumba hapaswi kujua madudu ya ajabu ajabu, anapaswa awaone wote kama malaika loh....

Aksante Baba yangu kwa bandiko hili.

Da King'asti aksante kwa post yako. Kusema ukweli ninatamani sana kama maisha ya past au family secrets zisingekuwa na muingiliano wowote na mahusiano yetu ya wakati huu. Yaani ninatamani sana but kwa bahati mbaya haiwezekani. Mimi nilikuwa kama Da King'asti katika suala zima la ukweli na uwazi unfortunately kilichokujanitokea katika uhusiano wangu ambao ulikomaa na kufikia kiwango cha ndoa na mtoto nilikuja kujuta kwani ilipofikia wakati wa ugomvi all the family secrets zilianikwa hadharani katika vikao vya familia kama nguo mbichi juani, tena with all those statements za.......Yes aliniambia, we si ulisemaga......tena uliniapia e.t.c.......kutokana na hili kusema ukweli nimeresout to tell only few, tena zile ambazo unahisi iko siku mtakutana nazo katika maisha yenu, lakini zile za sijui Ba mdogo alimbaka au alitembea na mwanae au sijui Baba alitembea na ma mdogo nitakufa nazo aisee, kwanza najua kabisa huyo baba mdogo hatowezanibaka!
mume mwenyewe kuna vingine humwambii..... na kuna mengine kuhusu kwao wala sitaki kuyachimba na kuyajua.....imagine unamwambia mpenzio" mpenzi wangu alopita tuliwahi fanya threesome"

uwiiiiiiiiiiiiiiii

chinekeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

na ndoa inaota mabawa...
 
Last edited by a moderator:

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Messages
10,476
Points
1,225

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined Jul 24, 2008
10,476 1,225
Mtambuzi usemayo ni kweli kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaa nakuunga kichwa mikono hadi miguu loh.......

my dear King'asti hizo siri ndo zitakuwa fimbo yako ya kukuchapia........MwanajamiiOne, natumaini King'asti atakusoma na kukuelewa hapa, mara nyingi hawa wapenzi wakikujua ndani nje wanazitumia siri hizi kama njia ya kukucontrol au kukuumizia, boyfiriend sijui mchumba hapaswi kujua madudu ya ajabu ajabu, anapaswa awaone wote kama malaika loh....mume mwenyewe kuna vingine humwambii..... na kuna mengine kuhusu kwao wala sitaki kuyachimba na kuyajua.....imagine unamwambia mpenzio" mpenzi wangu alopita tuliwahi fanya threesome"

uwiiiiiiiiiiiiiiii

chinekeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

na ndoa inaota mabawa...
Aksante BADILI TABIA
Mimi nimejifunza thro a hard way na somo limeniingia vizuri BUT Tukirejea kwenye mada ya Baba Mtambuzi nadhani yuko sawa kwa sababu kwa jinsi anavyosema kwa mwanaume asithubutu kuyasimulia haya na ni kweli wapo wanaume ambao hata iweje ya kwao hasimulii aisee........tena siku ukijakutana nalo la kwao hata kama mmeshaoana ukiuliza anawezakukujibu kuwa hajui au akakushut kabisa kuwa hayakuhusu nawe unabaki una-question maana ya kuwa kitu kimoja! Mimi nilishakutana na hiyo ambayo kwao kulikuwa na ugomvi wa hali ya juu ambao ulipelekea kifo cha mtu mmoja wa karibu sana nasi lakini mwenzangu aligoma kabisa kuelezea kilichojiri!!

So ni kweli kuna vya kuelezea na vya kumezea
 
Last edited by a moderator:

lara 1

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2012
Messages
15,645
Points
2,000

lara 1

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2012
15,645 2,000
Thubuuuuuuuuuuuuutu!!!!!!! Let the gones be by gones!!!!!!!!!! Siwezi kujiaanga mwenyewe kwa kitubio hata robo sekunde!!!!!!!!! Hell to the No!!!!!!!!

The past dsnt determine the present neither the future! ILL TAKE MY CHANCES THAT YOU MAY NOT FIND OUT!!!!!!! And even if you do ILL DENY ALL CHARGES uso mkavu, hapo lazima a guy abaki 50/50 huenda kweli, huenda uongo.

Never under estimate power of comfession!!!!!!!!! Yaani umekiri kwa kinywa chako na utashi wako WHAT IS THERE LEFT TO DOUBT!!!!!

WHAT HE DOESNT KNOW CANT KILL HIM!!!!!!!!!! Can it?
 
MadameX

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2009
Messages
7,831
Points
1,225

MadameX

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2009
7,831 1,225
Aisee Habari ambazo zinanitoa raha huwa simuelezi na ikiwa atauliza naweza hata kumwambia live kuwa its something I can't not share at the moment. Labda mbeleni, lakini mwanzo mwanzo :nono: :nono:
 
Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,810
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,810 2,000
Mie kabla hata ya first date, wakati tunaanza kuangaliana kwa macho ya paka na thamaki (ndo maana hata samaki akaangwe hafumbi jicho kwa kumuogopa nyau), naweka yoote mezani. Yaani ajue kabisa binti mtambuzi hazimtoshi, haoneleki na ana dingi anapenda vidosho (ile siri unamtegea maza kulea usiku siitaji). Yaani kabla hajayavulia nguo lazma ajue kabisaaa. Na wala siogopi, kwa sababu nahitaji from the word go, mwanaume anaejiamini na anaejijua anaweza kuishi popote na yeyote. Kama ni mwanaume anaeogopa ulevi wa babangu hanifai, manake atashindwa hata kunishauri na kunisaidia ili nimsaidie babangu. So hata dirty family secrets (we all have them jamani, za baba mdogo kutembea na mwanae ama mkamwana wake) mie namwagaaaa! Akiniona najikaribisha lwa huyo ba mdogo si atanilindia humohumo!
King'asti usiwaponze wenzio, wewe siri zako ni nyepesi sana, maana MIMI BABA YAKO MZEE MTAMBUZI NI MTU MTAKATIFU SANA, kwa hiyo familia yako haina jambo la fedheha zaiidi ya zile kesi zangu za ujanani kabla sijawowa na kuwazaa wewe na ndugu zako, kwa mfano yale mambo ya ndoa za mkeka Ununio, yale mambo ya trial marriage, au yale mambo ya Kuibiwa wallet na machangu kule viwanja vya Maeda, yote zilikuwa ni mbilinge za ujanani ambazo zinaonyesha kwamba mimi nilikuwa rijali na jandoni nimehudhuria.....

Lakini kuna wenzio humu hawatamani hata kuzifikiria siri za familia walimozaliwa na kwa bahati mbaya sana sisi hatuna uwezo mwa kuchagua familia ya kuzaliwamo, tumejikuta tu tumezaliwa na wazazi ambao yawezekana ni wapagani, wakristo, waislamu au waganga wa maruhani na matapeli wakutupwa. tunafinyangwa katika malezi ambayo yaweza kuwa ni mazuri au mabaya kulingana na familia ulimozaliwa....

Nasisitiza jamani msimsikilize huyu binti yangu atawapotezaaaa.................LOL
 
Last edited by a moderator:

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2008
Messages
10,569
Points
1,250

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2008
10,569 1,250
Ah wapi King'asti si rahisi kihivyo kama unavyoandika hapa. Mambo ya familia yako hasa mabaya si mepesi kutajwa tajwa. Yale mazuri ndio hutanguliwa kusemwa, na hata wakati mwingine watu hudanganya ili familia zao zionekane bora mbele ya macho ya wapenzi wao. Huo ubaya utakuja kujulikana baadae mbele ya safari.

Mie kabla hata ya first date, wakati tunaanza kuangaliana kwa macho ya paka na thamaki (ndo maana hata samaki akaangwe hafumbi jicho kwa kumuogopa nyau), naweka yoote mezani. Yaani ajue kabisa binti mtambuzi hazimtoshi, haoneleki na ana dingi anapenda vidosho (ile siri unamtegea maza kulea usiku siitaji). Yaani kabla hajayavulia nguo lazma ajue kabisaaa. Na wala siogopi, kwa sababu nahitaji from the word go, mwanaume anaejiamini na anaejijua anaweza kuishi popote na yeyote. Kama ni mwanaume anaeogopa ulevi wa babangu hanifai, manake atashindwa hata kunishauri na kunisaidia ili nimsaidie babangu. So hata dirty family secrets (we all have them jamani, za baba mdogo kutembea na mwanae ama mkamwana wake) mie namwagaaaa! Akiniona najikaribisha lwa huyo ba mdogo si atanilindia humohumo!
 
Last edited by a moderator:

Neylu

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Messages
2,823
Points
1,500

Neylu

JF-Expert Member
Joined May 28, 2012
2,823 1,500
Aaah.. Hawa wanaume bwana hawaeleweki!!

Habari za kujinyenyekesha kwa mtu na kumu ungamia makosa yako yote na kumpa kila ukweli wooote wakati huna hakika na huko mbele kama atakuoa au lah! Huu mchezo siwezi fanya kamwe!!

Unajisemesha masiri yako yote na kumsimulia maisha ya familia na ukoo wenu mzima huku yeye anakuchora tuuu..!!

Mwisho wa siku mambo yasipoenda vizuri utalia na mengi.! Hii biashara kwangu haipo kabisaaa..!!
 
King'asti

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
27,725
Points
2,000

King'asti

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
27,725 2,000
Mwita Maranya, BADILI TABIA na MwanajamiiOne, naona mdingi kanielewesha vizuri hapa. Pengine labda secrets zangu mie ni nyepesi ndo maana inakuwa rahisi. Ila on a serious note, labda naangalia pia akili ya mtu kabla ya kuwa close friend (i cant date mtu ambae sio close friend wangu). By the way, si naye nahakikisha ananipa ma family secrets? So ataanzia wapi kumwaga ugali? Na niseme nimekuwa lucky tu kwenye relationships, thank God, ila mie hadi mtu mwenye tuhuma ya uchawi namtaja waziii. Kesho tukigombana akasema ndo maana uncle wako mchawi namuambia acha ukalumekenge, si ulijua hilo before kunipenda?
MwanajamiiOne, mie nikuhurumie tu kwa sababu umekuwa mwanamke muafrika hadi unashindwa kujitetea. Issue ni moja, tuna mgogoro wa ndoa, tumekaa hapa kuelezana siri za moyoni, au tumekaa kujadili ndoa? Kwani wewe ulikuwa na siri ngapi za kwao, za kushuhudia na kusimuliwa? Ntamuambia hapo hapo usije ukasahau kuwaambia na wewe issues zako, unazimikiaga kati kati ya mlima na umepindia juu eeh. Manake kama unalala na mtu unaemuogopa, sasa lile kovu la kwenye kalio (ilimpata dada mmoja tukiwa sec, kakutana na player jamaa akahadithia hilo kovu dar nzima hadi kisarawe nadhani!).

mie si act up, kama ni kukutuma maji jikoni nakutuma live, lol. True colours from day one, im still that naughty gal you saw on the corridor 10 yrs ago.
 
Last edited by a moderator:

King'asti

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
27,725
Points
2,000

King'asti

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
27,725 2,000
Afu ungejua wewe unaniona bhange, wakati mwenzio wanajipanga kuomba ushauri hapa,lol. Kweli nabii hasifiki nyumbani kwao.
King'asti usiwaponze wenzio, wewe siri zako nyepesi.

Nasisitiza jamani msimsikilize huyu binti yangu atawapotezaaaa.................LOL
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,392,874
Members 528,740
Posts 34,120,676
Top