Mwanamke huyu ni "Stalker" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke huyu ni "Stalker"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by bitimkongwe, May 22, 2010.

 1. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Tafadhali naomba ushauri kwa jirani yangu huyu.

  Kuna mwanamke anamtaka kimapenzi lakini yeye hana interest naye kabisa. Lakini mwanamke huyu anamsumbua sana mpaka imekuwa kero. Mchana na usiku ni message tu za kumpenda na kumwomba waoane. Huyu mwanamke wala hajali kama yule jamaa ana mke au la. Saa kumi alfajiri anapiga simu. Ameshachoka kumwonya lakini ni kama akili zimefyatuka, hajali.

  Mimi nimeshauri asijibu hizo message yeye huwa hajibu lakini bado ndio kwanza kama amewashiwa moto.

  Jee munashauri afanye nini ili kuepukana na balaa hili? Maana amechoka kabisa. Anamfuata ofisini ikabidi aweke tahadhari kwa walinzi wakimwona wasimruhusu kabisa.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Aendelee hivyo hivyo. Ipo siku mwanamke atachoka tu.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mwambie akupigie pande wewe ujidawasco
   
 4. T

  Tall JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.wanapendana hao.wasikuzuge,hadi ofisini wameonyeshana.
  2. Asubiri mwenyewe pressure itashuka taratibu asiwe na haraka wala hasira.
  3.haiwezekani,azuiwe ofisini na walinzi halafu bado aendelee kumpigia simu?
  4.Nadhani kagundua jamaa yupo peke yake ndio maana spidi kali.
  5.Je kuwa na mwanamke anaempenda na kuwa na yule anaempenda sana sana bora yupi?........abadili mawazo amchukue huyu anaempenda sana sana..
  6.Kuna kitu amemwahidi,si bule,muulize vizuri jamaa yako.
  7.Labda jamaa ni kimwaga,ATM...........NDIO MAANA bibie hataki kumwacha.
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Kwani wewe ndo ulimleta huyo jamaa yako mjini au alikuja na mbio za mwenge? Mambo ya mapenzi bana hayahitaji ushabiki. We mkataze, afu ndo aje kuwa shemeji yako! Utakuwa unaona aibu kunywa juice kwake!
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  King'asti umesema kweli! Kaa pembeni!
   
 7. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ukimya ni mzuri kwa mtu kama huyo
   
 8. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Asanteni kwa ushauri, lakini kwa mara ya kwanza huyu mama alikutana na huyu jirani yangu ofisini kwa shughuli ya kazi, yaani ni kama vile unakwenda ofisini una shida halafu unaambiwa kamwone fulani. Katika kufuatilia baadhi ya wakati unampa mtu namba yako ya simu, na sio kwa lengo lo lote la ziada. Ndio yaliyomfika huyu jamaa.

  Kwa kweli hata kama anao mabibi wengine (hilo siwezi kujua) lakini at least kwa hapo nyumbani kwake anaonekana ni mtu mwenye heshima kwa familia yake. Sasa hiyo ndiyo inayomsumbua.

  Fidel80, kujidawasco ndio nini?
   
 9. JM Aristotle

  JM Aristotle Senior Member

  #9
  May 22, 2010
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee yaani believe me, na-'feel', huyo jamaa anachopitia...
  But, from experience; njia pekee ni kuendelea kukaa kimya tu, kwasababu hata kama ukimkataza, ataendelea tu...
  Siku moja ataona kwamba hafiki popote, na ataamua kuacha tu...
  (Mpe pole sana...)
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  safi sana, absolutely true and very good advice
   
Loading...