Nashindwa kuelewa hii ni tabia ya namna gani kwa huyu mwanamke au tuite hulka?

farfat

Senior Member
Jun 10, 2021
158
265
Ndio ni kweli nashindwa kuelewa hii ni hali ya namna gani kwa huyu mwanamke wangu tabia zake naona sio za kawaida natamani kuachana nae lkn nimeshamzoea na inakuwa viguma kiasi flani ndio maana nataka ushauri wenu wananzengo.

Nipo na huyu dada ktk mahusiano ya kimapenzi takriban miezi sita sasa ila amekuwa na tabia za kushangaza mfano ni siku ya kwanza nilipotoka nae out tulienda club fulan hivi matata hapa mjini inaitwa Warehouse ipo Masaki. Tukiwa katikati ya burudani mie vibe la kucheza lilinichosha nikaomba pause kwa mrembo wangu tupumzike ila ajabu yeye hakutaka kutulia alitaka kuendelea kucheza hivyo akaniomba acheze na mtu aliempoint yeye ktk macho yake nami nikaona sio kesi muache acheze nae lkn ilinishangaza sana aliwezaje kuwa na hali ya kutaka mwingine wakati nimeenda nae mimi! Nilihisi ni ulevi nikakausha siku ikapita.

Tabia yake nyingine inayonishangaza ni namna ambavyo anakuwa mwepesi kuzoea watu kwa haraka yani hana password kabisa huyu dada mpaka naona jau sasa.

Ila sasa tukio lililonipa mshangao mpaka kuja hapa ni kwamba majuzi bwana kulikuwa na game ya Yanga nami nikaona sio kesi ngoja nitoke na baby mama wangu aka Shangae shangae game si ikaanza bwana mara tukala chuma kila mtu akabaki amefedheheka asiamini kilichotokea lakini punde si punde mwamba Mayele akaweka kamba kimiani basi uwanja wote ukalipuka kwa furaha mara gafla baby mama akaja maungoni kwa furaha akanikumbatia nikaona kweli mtoto kafurahi mara nikaona gafla tena kamkumbatia mwamba alikuwa pembeni yangu aloooo nilishangaa wallah na vibe ikakata lakini sikuonesha hali ya makasiriko ila nilibaki kuduwaaa huyu ni mtu wa aina gani mbona kituko alooo.

Hana password kabisa why anakuwa mtu wa hivi, hii ni kawaida kweli wazee au ni namna gani mbona naona mwanamke wangu mjinga sana?
 
hakuna mwanamke hapo, piga chini hiyo malaya. Mwanamke apaswa kujiheshimu na kumheshimu mwanaume wake, sasa kama mbele ya mboni zako haoni shida kuwatomasa wanaume tena yeye ndio anawaparamia, ebo !! Usipokuwepo je ?, si ndio anatoa mpaka kijambio.
 
atakuwa alisoma shule za bweni wasichana, kipindi cha disco ( Yale ya welcome one form 1, form 5 na ya graduation)msichana mmoja anaweza kucheza na ukumbi mzima wavulana,kwa hiyo bado anafikiri hata huko club ni hivyo.
 
Ndio ni kweli nashindwa kuelewa hii ni hali ya namna gani kwa huyu mwanamke wangu tabia zake naona sio za kawaida natamani kuachana nae lkn nimeshamzoea na inakuwa viguma kiasi flani ndio maana nataka ushauri wenu wananzengo... nipo na huyu dada ktk mahusiano ya kimapenzi takribani miezi sita sasa ila amekuwa na tabia za kushangaza mfano ni siku ya kwanza nilipotoka nae out tulienda club flan ivi matata hapa mjini inaitwa warehouse ipo masaki. tukiwa katikati ya burudani mie vibe la kucheza lilinichosha nikaomba pause kwa mrembo wangu tupumzike ila ajabu yeye hakutaka kutulia alitaka kuendelea kucheza hivyo akaniomba acheze na mtu alie mpoint yeye ktk macho yake nami nikaona sio kesi muache acheze nae lkn ilinishangaza sana aliwezaje kuwa na hali ya kutaka mwingine wakati nimeenda nae mimi.. nilihisi ni ulevi nikakausha siku ikapita...
Tabia yake nyingine inayonishangaza ni namna ambavyo anakuwa mwepesi kuzoea watu kwa halaka yani hana password kabisa huyu dada mpaka naona jau sasa...
Ila sasa tukio lililonipa mshangao mpaka kuja hapa ni kwamba majuzi bwana kulikuwa na game ya yanga nami nikaona sio kesi ngoja nitoke na baby mama wangu aka Shangae shangae.. game si ikaanza bwana mara tukala chuma kila mtu akabaki amefedheheka asiamini kilichotokea lakini punde si punde mwamba mayele akaweka kamba kimian basi uwanja wote ukalipuka kwa furaha mara gafla baby mama akaja maungoni kwa furaha akanikumbatia nikaona kweli mtoto kafurahi mara nikaona gafla tena kamkumbatia mwamba alikuwa pembeni yangu aloooo nilishangaa wallah na vibe ikakata lakini sikuonesha hali ya makasiliko ila nilibaki kuduwaaa huyu ni mtu wa aina gani mbona kituko alooo. Hana password kabisa why anakuwa mtu wa hivi.. hii ni kawaida kweli wazee au ni namna gani mbona naona mwanamke wangu mjinga sana....
Huyo hafikagi kule mlimani mwisho kabisa, safari zako ukimtembeza unaishiaga humu njiani njiani. 😊
 
Back
Top Bottom