Nipeni ushauri kuhusu huyu mwanamke maana nipo njia panda

BIG Africa

Member
Oct 15, 2022
85
117
Habari zenu
Bila kupoteza muda Mimi naishi jijini Arusha, nimetokea kuwa katika Mahusiano na kadada kamoja hapa hapa Arusha. Mahusiano bado hayajawa deep kwani tuna muda mchache kama miezi minne. Kikubwa kilichonivutia Kwa huyu dada ni kwamba ni mpole, mkarimu pia ana hofu Sana na Mungu(huyu dada ni muslamu) Mimi ni mkristo katika kupiga naye Stori kuhusu kubadili dini dogo yupo tayari.

Kinachonishangaza Kwa huyu demu ni kwamba yeye anadai hana simu mara nyingi huwa anatumia namba za watu wake wa karibu hasa dada yake nilijaribu kupeleleza Kwa wenzake wakaniambia kuwa simu huwa wanamuona nayo. Hapa katikati nilikuja nikapewa namba yake ya simu na watu wake wa karibu (hakunipa yeye)ambayo nayo muda mwingi haipatikani lakini inapatikana Watsup tu japo pia siyo sana.

Pindi Ninapokuwa nachati nae Watsup huwa anajibu meseji sema taratibu Sana na juzi Kati huyu dada nilitoka kumuomba picha zake anitumie Watsup akasema atanitumia lakini mpaka Leo hajatuma. Muda huo bando Kwa màana ya vocha huwa namtumia (Bila kuniomba) lakini huyu demu hajawahi kusema ahsante.

Vipi kuhusu kumtumia pesa?. Mara nyingi huyu demu huwa namuambia nimtumie pesa kidogo ya kutumia lakini cha kushangaza huwa anakataa anasema "usijali" lakini pindi Ninapokuwa nae hivi ana Kwa ana nikimpa pesa anachukua Bila shida.

Usichoke tuendelee, juzi Kati nilimwona yupo online Watsup nikachat nae akajibu mtu mwingine ambaye alijitambukisha kuwa ni dada yake na laini ya simu ni yake. Pale pale nikawaza kuwa huyu demu huenda kweli hana simu kwani dada yake nilimpigia Watsup call voice alisema huyo mdogo wake hana simu na laini anayoitumia ni yake huwa Tu anamuazima dada yake Kwa muda ili achati Watsup.

Sasa kinachonishangaza Kwa sasa kuhusu huyu dada ni kwamba hajibu tena meseji zangu Watsup yaani akiwa online nikimtumia hajibu. Hapo awali kama nilivyosema niliwahi kumuomba anitumie picha zake kadhaa Watsup akadai atanitumia lakini hajawahi kunitumia lakini muda huo huo picha zake naziona akiwa anazituma kwenye status yake watsup.

Kwa mfano Jana usiku huyu dada alikuwa online Watsup akichati na kisha nikaona amposti picha zake kwenye status lakini nikimtumia meseji kibao hajajibu na meseji zinafika. Nimetafari Kwa kina zaidi kuhusu Hali hiyo nimekuja kuwa nahisi labda kwasasabu nilichati na dada yake ambaye aliniuliza kwamba kwenye laini ni yeye ni Mimi nilimwambia au kujitambulisha kwake kwamba Mimi ni rafiki wa mdogo wake na baadae nikamwambie amsalimie koz nampenda sana.

Hapo labda nahisi labda ndiyo sababu ya yeye kutokujibu meseji zangu Watsup labda alitaka iwe Siri??.Binafsi sijui.Huyu demu umri wake ni early 20s (miaka kama 20 au 21 hivi) Mimi nina miaka 30.Kuja kwenu wana jamii forums ni kuomba ushauri kwenu je huyu mwanamke anaweza kuwa mtu sahihi kwangu?

Kwa jinsi ambavyo nilivyoeleza kwani binafsi nimetokea kumpenda Kwa dhati dada huyu na sitaki kumchezea kwani nataka kumuoa kabisa lakini sasa Kwa hili kinachoendelea Mimi kinanichanganya kuhusu yeye japo huyu demu na yeye hapo awali alishawahi kuniambia kuwa ananipenda pia.Ushauri wenu jamani.Karibuni.
 
Habari zenu.Bila kupoteza muda Mimi naishi jijini Arusha nimetokea kuwa katika Mahusiano na kadada kamoja hapa hapa Arusha.Mahusiano bado hayajawa deep kwani tuna muda mchache kama miezi minne.Kikubwa kilichonivutia Kwa huyu dada ni kwamba ni mpole,mkarimu pia ana hofu Sana na Mungu(huyu dada ni muslamu) Mimi ni mkristo katika kupiga naye Stori kuhusu kubadili dini dogo yupo tayari.Kinachonishangaza Kwa huyu demu ni kwamba yeye anadai hana simu maranyingi huwa anatumia namba za watu wake wa karibu hasa dada yake nilijaribu kupeleleza Kwa wenzake wakaniambia kuwa simu huwa wanamuona nayo.Hapa katikati nilikuja nikapewa namba yake ya simu na watu wake wa karibu (hakunipa yeye)ambayo nayo muda mwingi haipatikani lakini inapatikana Watsup tu japo pia siyo sana.Pindi Ninapokuwa nachati nae Watsup huwa anajibu meseji sema taratibu Sana na juzi Kati huyu dada nilitoka kumuomba picha zake anitumie Watsup akasema atanitumia lakini mpaka Leo hajatuma.Muda huo bando Kwa màana ya vocha huwa namtumia (Bila kuniomba) lakini huyu demu hajawahi kusema ahsante.Vipi kuhusu kumtumia pesa?.Mara nyingi huyu demu huwa namuambia nimtumie pesa kidogo ya kutumia lakini cha kushangaza huwa anakataa anasema "usijali"lakini pindi Ninapokuwa nae hivi ana Kwa ana nikimpa pesa anachukua Bila shida.Usichoke tuendelee.Juzi Kati nilimwona yupo online Watsup nikachat nae akajibu mtu mwingine ambaye alijitambukisha kuwa ni dada yake na laini ya simu ni yake.Pale pale nikawaza kuwa huyu demu huenda kweli hana simu kwani dada yake nilimpigia Watsup call voice alisema huyo mdogo wake hana simu na laini anayoitumia ni yake huwa Tu anamuazima dada yake Kwa muda ili achati Watsup.Sasa kinachonishangaza Kwa sasa kuhusu huyu dada ni kwamba hajibu tena meseji zangu Watsup yaani akiwa online nikimtumia hajibu.Hapo awali kama nilivyosema niliwahi kumuomba anitumie picha zake kadhaa Watsup akadai atanitumia lakini hajawahi kunitumia lakini muda huo huo picha zake naziona akiwa anazituma kwenye status yake watsup.Kwa mfano Jana usiku huyu dada alikuwa online Watsup akichati na kisha nikaona amposti picha zake kwenye status lakini nikimtumia meseji kibao hajajibu na meseji zinafika. Nimetafari Kwa kina zaidi kuhusu Hali hiyo nimekuja kuwa nahisi labda kwasasabu nilichati na dada yake ambaye aliniuliza kwamba kwenye laini ni yeye ni Mimi nilimwambia au kujitambulisha kwake kwamba Mimi ni rafiki wa mdogo wake na baadae nikamwambie amsalimie koz nampenda sana.Hapo labda nahisi labda ndiyo sababu ya yeye kutokujibu meseji zangu Watsup labda alitaka iwe Siri??.Binafsi sijui.Huyu demu umri wake ni early 20s (miaka kama 20 au 21 hivi) Mimi nina miaka 30.Kuja kwenu wana jamii forums ni kuomba ushauri kwenu je huyu mwanamke anaweza kuwa mtu sahihi kwangu? Kwa jinsi ambavyo nilivyoeleza kwani binafsi nimetokea kumpenda Kwa dhati dada huyu na sitaki kumchezea kwani nataka kumuoa kabisa lakini sasa Kwa hili kinachoendelea Mimi kinanichanganya kuhusu yeye japo huyu demu na yeye hapo awali alishawahi kuniambia kuwa ananipenda pia.Ushauri wenu jamani.Karibuni.
Mnunulie simu
 
Back
Top Bottom