Mwanamke, Hata wewe unayo haki ya kutoa talaka...!

Mwanamke, Hata wewe unayo haki ya kutoa talaka...!

sijidanganyi wala simdanganyi mtu yeyote hapa ninavyosema hapa ni ukweli na uhakika kwani mm ni mama paroko na nimefanya utafiti na nimeshawafanyia watu wengi canselling, na wengine niliowashauri na kuwafanyia kanselingi wameniambia na kujiweka wazi kuwa ndoa zao nyingi zilitokana kwenye vichochoro, vimtandao, na vikicheche uchwara ndo mana zimeleta shida na migogoro mingi kutokea, tofauti na ndoa zile za watu au vijana kujuana kwenye ibada hiyo ndo true mkaka acha kujifanya utambui hebu funguka uelewe zaidi na ukitaka ushauri au kufanyiwa kanselingi kwenye ndoa yako na Mama Ngina njoo kwangu nitakufunda zaidi na utakuwa imara kwenye ndoa yako
Kwa hiyo wewe ni paroko wa nchi nzima eh.....
ladyfurahia
 
Last edited by a moderator:
wala sijapotosha lara 1.
Ukweli ni kwamba wengi mnaishi kwa mazoea, na ni kwa sababu ya mfumo dume + rushwa iliyokithiri katika sekta za kudai haki mpaka kwenye taasisi za dini ndio maana mnaona ni mwanaume tu ndiye mwenye haki ya kumuacha mke.
Kama ukifuatilia kwa mujibu wa vipengele vya sheria na hata katika dini, mke ana haki ya kumuacha mume. Je anamuacha kwa njia gani hapo sasa ndipo mnapojichanganya.
Kama atakwenda mahakamani na kudai kutaka kuachana na mumewe na mahakama ikaamua hivyo, si ndio kutaliki kwenyewe huko...?
Mtambuzi kudai talaka haina maana ya kutaliki manake unadai ila mwenye kukupa ni mtu baki.
Sasa iwapo mtu baki huyo atagoma kukupa talaka je unafikiri utakuwa umefikia lengo lako??

Ninaye aunt yangu mimi leo hii ni mwaka wa 8 anadai talaka mume wa ndoa kagoma kumpa kabisa licha ya kwamba shauri liko mahakamani na bakwata. Mbaya zaid mume anadai sijawah kumfukuza mke wangu na mimi bado nampenda ila cha ajabu mke anaish tabata mume anaish mikocheni kwa miaka yote hii. Kuja kugundua kumbe mume kamuekea kauzibe tu asiolewe na mwanaume mwingine na hivyo hata akiafa leo mumewe anakwenda kumzika kama mke.

Nafikri wewe unaongelea jambo bila kujua sheria za ndoa zinasemaje. Sheria bado haimlazimish mwanaume kuandika talaka hata kama mke amedai talaka hiyo. Na sheria ya ndoa ya mwaka 2004 ikasema kabisa mwanaume ndiye mwenye majukumu ya kumlinda mke na watoto wake.
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi unapotosha umma mwanamke hawez kutoa talaka bali anauwezo wa kudai talaka basi. Kudai talaka ni tofauti na kutoa talaka. Ngoja nione nawezaje kuattach document moja hapa uisome juu ya sheria ya ndoa.
 
Last edited by a moderator:
mwanamke kudai talaka ni sawa na inawezekana. Ambalo haliwezekani ni mwanamke kumpa talaka mwenzi wake.. May be wanawake wa India ndio watakaoweza kuwapa waume zao talaka kwa sababu wao (wanawake) ndio hutoa mahari.

U a very right my dear, but the point is MWANAMKE PIA ANA UAMUZI WA KUACHANA NA MWENZA WAKE. Swala la kutoa ama kutokutoa, wote wanaseek goal moja, KUACHANA.
 
you are very wrong!!
Mahari sio ujira aliokuwa napewa baba yako wala sio hela aliyokuwa anapewa ili amuze dada yako. Mahari ni ishara ya kuunganisha familia mbili kama vile kununua ukoo.
Kiafrika mahari hutumika kama alama ya kuunganisha familia mbili na ndio sababu wengi hutaka kaupewa vitu na sio fedha.

Hata mungu mwenyewe aliamuru mahari iwepo ili ionekane kwamba familia zimeunganishwa kwa gharama. Swala la kusema dada maisha yakikushinda urudi nyumban halina uhusiano na mahari manake wapo wengi tu yalipowashinda waliondoka bila kujali swlai la mahari na mpaka leo wanaish kwa amani na furaha.

Wapo wengine kwa kujua umuhimu wa mahari walidiriki hata kuwasaidia waume zao kulipa mahari yaani binti anampa mwanaume pesa ili amlipie mahari na bado yalipowashinda walioaandoka tu.

Kwangu mimi mahari ni jambo la muhimu na halina uhusiano na amani na furaha ya wanandoa husika
gfsonwin, mahari ilikuwa na maana hiyo unayoizungumzia miaka ya 1947 na si kwa kizazi hiki cha Dot Com.
Siku hizi kwa mfumo wa mahari mwanamke anachukuliwa kama bidhaa na ndio maana baadhi ya wanaume waliolipishwa mahari nyingi hujimilikisha mwanamke kama chombo cha kumtumikia na si binadamu mwenzie mwenye haki sawa na yeye.

Hebu sikia jibu na mwanaume anayeulizwa anakwenda wapi na mkewe...
utasikia anajibiwa.. "Unaniuliza nakwenda wapi, wewe ni kama nani..."

Hiyo dhana yako ni ya kale mno, siku hizi ukichukua mahari ni sawa na kumuuza binti yako, wankwangu mie kina Ngina nitawagawa bure...

Copy to: King'asti, Kipipi, Asnam, Paloma
 
HEBU SOMA HAPA KAMA ILIVYO ANDIKWA NA ALAN KAJEMBE KISHA NITARUDI NA DOCUMENT NYINGINE.

NENO talaka linaweza kuwa mojawapo ya maneno yaliyozoeleka midomoni au masikioni mwa watu wengi katika ulimwengu wa sasa.

Kwa lugha nyepesi, talaka ni kitendo cha wanandoa kuachana na mahusiano ya kindoa yaliyokuwa baina yao.
Lakini kisheria, ingawa maana ya talaka inaakisiwa na maana hii ya Kiswahili, lakini katika maana ya sheria kuna mambo mengine zaidi ya kuzingatia.
Tafsiri ya sheria ya ndoa ya Tanzania, sura ya 29 ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2002, talaka ni kitendo cha mahakama yenye mamlaka katika shauri linalohusika, kutoa tamko la kuivunja ndoa iliyokuwapo,kwa sababu mbalimbali.
Hivyo, tukiangalia kwa mtazamo wa kihistoria, ndoa kwa mujibu wa sheria ya Kiingereza (common law) ambayo imeakisiwa sana na sheria ya ndoa ya Tanzania, ilikuwa haitambui sababu ya aina yeyote katika kuivunja ndoa kwa msingi wa talaka.
Lakini baada ya miaka mingi kupita, sheria ya talaka ilianza kutumika nchini Uingereza baada ya sababu kadhaa za kisheria za kuvunja ndoa kwa talaka kuanzishwa.
Sheria ya Talaka (The Divorce Act) ya mwaka 1969 ilianzishwa nchini Uingereza kufuatia ripoti ya askofu Kent wa nchini humo.
Mwaka mmoja baadaye yaani mwaka 1969 serikali ya Tanzania kupitia tamko la serikali (Government Notice) namba 1 ya mwaka huo, iljuyolikana kama White Paper ilichukua msimamo na mtazamo huu wa sheria ya Kiingereza juu ya talaka.
Hadi mwaka 1971 tulipochukua msimamo huu wa sheria ya Uingereza juu ya talaka, mabadiliko makubwa ya kimsingi ya sheria juu ya talaka yalitokea katika sheria yetu hapa nchini nayo ni pamoja na kuwa na sababu moja tu inayoweza kuifanya ndoa kuvunjwa na mahakama kwa tamko la talaka, sababu hiyo ni kuwa mahakama itakapothibitisha kwamba ndoa hiyo imevunjika kabisa na haiwezi kurekebishika kutokana na kasoro zisizo weza kurekebishika.
Hivyo, sheria ya Tanzania katika hili nayo ikachukua sababu moja inayoweza kuifanya ndoa kuvunjwa na talaka.
Hata hivyo, wakati tunaangalia sheria hii, tunatakiwa kujua kwamba sababu moja ya kuivunja ndoa kwa talaka ipo Tanzania bara pekee.
Baadhi ya watu wanadhani sababu za kuvunja ndoa ni zile zinazoelezewa na sheria hii kama hali au mazingira ya kuthibitisha kwamba ndoa hiyo ina tofauti zisizorekebishika.
Sababu hizo ni pamoja na uzinifu nje ya ndoa, ukatili pamoja na kumkimbia/kumtelekeza mwanandoa mwezako.
Uzinifu ni mojawapo ya sababu zinazoipa mahakama mamlaka kisheria kuivunja ndoa yoyote.
Hata hivyo, unatakiwa kujua uzinifu una maana nyingi kutegemea na eneo husika.
Kimsingi uzinifu ni kitendo cha mwanandoa mmoja kufanya ngono nje ya mahusiano yake ya ndoa iliyo halalishwa.
Hapa katika kuondokana na wasiawasi wa kuweza kushindwa kuthibitisha uzinifu, sheria imetoa dhana kwamba pale tu itakapokutwa mume na mke wamelala pamoja na wako watupu, basi dhana hapa ni kwamba wametoka au wanataka kufanya ngono.
Dhana hii kama ilivyoanzishwa na mahakama katika shauri la Denise dhidi ya Denise, Jaji Single anasisitiza kwamba dhana hii ni ngumu kuipinga isipokuwa kama itathibitika kwamba mwanaume aliyekutwa ni ------- au mwanamke huyo ni bikira.
Na uthibitisho wa uzinifu nje ya ndoa ni kama uthibitisho wa katika kesi ya jinai ambapo anayelalamika anatakiwa kuithibitishia mahakama pasi na shaka kwamba uzinifu umetokea.
Kwa upande wa Uingereza, kama itathibitika kwamba kulikuwa na uzinifu na kwamba mtoto alizaliwa nje ya ndoa, pia atahesabika ni mtoto haramu na hivyo kukosa haki zake zote kwa mzazi wake wa pili.
Hata hivyo, mara nyingi uzinifu unaweza kuthibitishwa na ushahidi wa mazingira kama vile mmoja wa wanandoa kuwa na ugonjwa wa zinaa na kadhalika.
Kifungu cha 170(2) cha sheria ya ndoa ya Tanzania, kinatoa maelekezo juu ya ushahidi wa aina hii.
Hata hivyo, uzinifu si lazima uwe sababu ya mahakama kutoa talaka. Mahakama kwa kuzingatia mazingira ya kesi husika inaweza kuamuru mtu aliyefanya uzinifu na mmoja wa wanandoa kumlipa fidia muathirika wa uzinifu huo.
Ukatili pia ni sababu mojawapo ya sababu zinazoweza kuithibitishia mahakama kwamba ndoa hii ina kasoro zisizoweza kurekebishika.
 
gfsonwin, mahari ilikuwa na maana hiyo unayoizungumzia miaka ya 1947 na si kwa kizazi hiki cha Dot Com.
Siku hizi kwa mfumo wa mahari mwanamke anachukuliwa kama bidhaa na ndio maana baadhi ya wanaume waliolipishwa mahari nyingi hujimilikisha mwanamke kama chombo cha kumtumikia na si binadamu mwenzie mwenye haki sawa na yeye.

Hebu sikia jibu na mwanaume anayeulizwa anakwenda wapi na mkewe...
utasikia anajibiwa.. "Unaniuliza nakwenda wapi, wewe ni kama nani..."

Hiyo dhana yako ni ya kale mno, siku hizi ukichukua mahari ni sawa na kumuuza binti yako, wankwangu mie kina Ngina nitawagawa bure...

Copy to: King'asti, Kipipi, Asnam, Paloma

acha kuish kwa stori zakimtaani bana, twende kweye uhalisia.
je wataka kuniambia wewe baba yako alitaka mahari ki dot com??
je sheria inasemaje juu ya mahari??

tatizo wewe unayachukulia maisha kwa namna ya kidot com na wala husimami kwenye principles zilizopo na hivyo itatupeleka kukuza kizazi kisicho kuwa na utash wa mambo ya msingi kabisa kweye maisha yao.

so far binti wa kutolewa bure anaweza kuteswa sana na huyo mume manake atamwabia WEWE BABA YAKO MWENYWE ALIKUWA NATAFUTA WA KUMGAWIA NDO MANA ALIMGAWA KWANGU BURE HUNA THAMANI YYTE SI KWANGU TU HATA KW AWAZAZI WAKO
 
Mtambuzi kudai talaka haina maana ya kutaliki manake unadai ila mwenye kukupa ni mtu baki.
Sasa iwapo mtu baki huyo atagoma kukupa talaka je unafikiri utakuwa umefikia lengo lako??

Ninaye aunt yangu mimi leo hii ni mwaka wa 8 anadai talaka mume wa ndoa kagoma kumpa kabisa licha ya kwamba shauri liko mahakamani na bakwata. Mbaya zaid mume anadai sijawah kumfukuza mke wangu na mimi bado nampenda ila cha ajabu mke anaish tabata mume anaish mikocheni kwa miaka yote hii. Kuja kugundua kumbe mume kamuekea kauzibe tu asiolewe na mwanaume mwingine na hivyo hata akiafa leo mumewe anakwenda kumzika kama mke.

Nafikri wewe unaongelea jambo bila kujua sheria za ndoa zinasemaje. Sheria bado haimlazimish mwanaume kuandika talaka hata kama mke amedai talaka hiyo. Na sheria ya ndoa ya mwaka 2004 ikasema kabisa mwanaume ndiye mwenye majukumu ya kumlinda mke na watoto wake.
gfsonwin, swala hapa ni mfumo wa kudai haki ndio mbovu na umekithiri kwa rushwa lakini haubadili haki ya mwanamke kumuacha mume mkorofi...
Labda nyie mnatatizwa na neno TALAKA, hivi ningesema mke anayo haki ya kumuacha mume, kungeibuka haya maswali mnayouliza hivi sasa.....?
 
Last edited by a moderator:
Wala sijapotosha lara 1.
Ukweli ni kwamba wengi mnaishi kwa mazoea, na ni kwa sababu ya mfumo dume + rushwa iliyokithiri katika sekta za kudai haki mpaka kwenye taasisi za dini ndio maana mnaona ni mwanaume tu ndiye mwenye haki ya kumuacha mke.
Kama ukifuatilia kwa mujibu wa vipengele vya sheria na hata katika dini, mke ana haki ya kumuacha mume. Je anamuacha kwa njia gani hapo sasa ndipo mnapojichanganya.
Kama atakwenda mahakamani na kudai kutaka kuachana na mumewe na mahakama ikaamua hivyo, si ndio kutaliki kwenyewe huko...?

Kwenda Mahakamani ni CONTINGENT ACT! Its all about chances! YOU MAY WIN OR MAY NOT!!!!!!!!! Sasa usiposhinda kesi na UKANYIMWA talaka umetoaje talaka hapo sasa?

Rejea KAMUSI! Neoa TOA na DAI hayana maana wala mantiki sawa !!!!!

NASISITIZA, YOU ARE CHEATING BEFORE THE MASSES!!!!!!!!!!!! Mwanake katu hawezi kutoa talaka usipotoshe uma!
 
acha kuish kwa stori zakimtaani bana, twende kweye uhalisia.
je wataka kuniambia wewe baba yako alitaka mahari ki dot com??
je sheria inasemaje juu ya mahari??

tatizo wewe unayachukulia maisha kwa namna ya kidot com na wala husimami kwenye principles zilizopo na hivyo itatupeleka kukuza kizazi kisicho kuwa na utash wa mambo ya msingi kabisa kweye maisha yao.

so far binti wa kutolewa bure anaweza kuteswa sana na huyo mume manake atamwabia WEWE BABA YAKO MWENYWE ALIKUWA NATAFUTA WA KUMGAWIA NDO MANA ALIMGAWA KWANGU BURE HUNA THAMANI YYTE SI KWANGU TU HATA KW AWAZAZI WAKO
gfsonwin, dada yangu hujaelewa, baba yangu (Mungu amrehemu huko aliko) kama ilivyo wewealikuwa na mawazo hayo ya mwaka 1947 ambayo sijasema kama ni mabaya.. nielewe dada yangu..
Ubaya uko kwa hawa vijana wa Dot Com, kwamba wao wanatafsiri mahari kama kitu gani....?
 
Last edited by a moderator:
lara 1 mdogo wangu mwanamke anahaki ya kudai talaka lkn sio kutoa talaka nafikiri ndicho alichomaanisha Mtambuzi.

lakini pia kwa experience yangu wanawake wengi waliodai talaka zao hasa kwa wale niliowashudia wengi ambao ni waislamu walikutana na pigo kubwa sana la mume kukataa kumpa talaka na hii kwao imekuwa ni adhabu kali sana manake asipokupa talaka huwez kuolewa tena hivyo utabaki tu kuwa mtaliki lkn usiye rasmi.

kifungu hiki na chenyewe bado kina mnyima mwanamke haki yake ya msingi ya kupata maisha ya amani na furaha anayotakiwa kuyapata. mwanamUME anapokataa kutoa talaka hawez kulazimishwa na mahakama atoe talaka na akisema huyu bado nampenda hata kama ni ya uongo hakuna jins ambavyo mahakama inaweza kutengua kauli hii hivyo badala ya kuwa na unafuu kwa mwanamke imekuwa ni adhabu tena mbaya sana.

IKUMBUKWE KWAMBA TALAKA SIO DHABU ILA KUKATAA KUTALIKI NI ADHABU TENA MBAYA SANA KWA MWANAMKE
hapo nna wasi wasi kuwa huna taarifa sahihi wewe na hao unaowazungumzia

Nawajua Wanawake wawili wa kiislam waliochoka na waume zao wakapewa talaka na kadhi (BAKWATA) kwa sababu waume zao walikataa na sasa wote wawili wameolewa upya na wapo maisha yanasonga

Kwa hiyo nadhani tatizo kubwa kama ilivyoainishwa hapa ni ukosefu wa elimu kuhusiana na taratibu stahiki za kufikia talaka iwapo mwanamke anataka yeye talaka

Kimsingi, katika sheria za Kiislam mwanamke ana haki ya kupewa talaka mahakamani hata akisema "sina sababu ya msingi, sitaki tena tu kuwa nae"

Bila ya shaka, sheria ya msingi na utekelezaji wake kwa kwetu ni tofauti mno, lakini ukiwa na elimu ya unachokidai basi sirahisi kikosi haki yako

Na mwanamme anapokataa kutoa talaka kisheria mahakama (ya kadhi) inatakiwa kutoa badala yake

Ningeshauri watu wajifunze sheria za dini wanazozifuata ili kurahisisha kupata haki zao
 
Kwenda Mahakamani ni CONTINGENT ACT! Its all about chances! YOU MAY WIN OR MAY NOT!!!!!!!!! Sasa usiposhinda kesi na UKANYIMWA talaka umetoaje talaka hapo sasa?

Rejea KAMUSI! Neoa TOA na DAI hayana maana wala mantiki sawa !!!!!

NASISITIZA, YOU ARE CHEATING BEFORE THE MASSES!!!!!!!!!!!! Mwanake katu hawezi kutoa talaka usipotoshe uma!
Mahakama ndio inayovunja ndoa hata kama mume au mke hataki kufanya hivyo...
 
^^
Mtambuzi
Wanawake wanaharakati wanaujua ukweli huu,,ukitaka kuthibitisha hili tazama mabinti wanang'ang'ania ndoa za kisheria ili mambo yakienda kombo mgawane mpaka sisimizi walio ndani kupitia mahakama.
^^
 
Last edited by a moderator:
Uliyoyaongea ni mambo ya msingi tu lakini naona hukugusia masuala ya imani maana kuna jamii ambayo mkishaingia kwenye ndoa ni mpaka kufa na kuzikana hili nalo sijui likoje,lakini jamii zingine hayo mambo yanawezekana tu unachotakiwa ni kuliweka suala lako kwa wahusika kisha utekelezwaji unafuata kasheshe ni hizo jamii zingine labda kama mifumo imebadilika na kuachana kupo!
 
Mila na desturi za mahali Fulani zilikubaliwa kama chimbuko la sheria kwa eneo fulani maadamu hazitakwenda kinyume na msingi wowote wa kanuni za sheria za Kiislamu: Kwa mfano mila za kindoa za mahali kuhusiana na kulipa mahari. Mahari kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, ni lazima ikubaliwe kama sehemu ya mkataba katika Nikaah lakini hapana wakati maalum uliowekwa kwa kutolewa (kulipwa). Ni desturi ya Wamisri na pia watu wengine kuwa sehemu fulani ya mahari inayoitwa Muqaddam (iliyotangulizwa) ni lazima ilipwe kabla ya sherehe za ndoa ilhali sehemu iliyobakia inayoitwa Mu'akhkhar (ilyoakhirishwa) inatakiwa tu ilipwe panapotokea kifo au talaka, kulingana na kile kinachotokea mwanzOhttp://www.alhidaaya.com/sw/node/2271#ftn3

SOMA NUKUU HII TOKA KATIKA MILA /DESTURI ZA KIISLAMU
 
Mila na desturi za mahali Fulani zilikubaliwa kama chimbuko la sheria kwa eneo fulani maadamu hazitakwenda kinyume na msingi wowote wa kanuni za sheria za Kiislamu: Kwa mfano mila za kindoa za mahali kuhusiana na kulipa mahari. Mahari kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, ni lazima ikubaliwe kama sehemu ya mkataba katika Nikaah lakini hapana wakati maalum uliowekwa kwa kutolewa (kulipwa). Ni desturi ya Wamisri na pia watu wengine kuwa sehemu fulani ya mahari inayoitwa Muqaddam (iliyotangulizwa) ni lazima ilipwe kabla ya sherehe za ndoa ilhali sehemu iliyobakia inayoitwa Mu'akhkhar (ilyoakhirishwa) inatakiwa tu ilipwe panapotokea kifo au talaka, kulingana na kile kinachotokea mwanzO

SOMA NUKUU HII TOKA KATIKA MILA /DESTURI ZA KIISLAMU

Sasa kama mie ni MPAGANI hayo maneno yako yatanisaidia nini?
Kwanza ushasema ni mila za WAMISRI, mie MMATUMBI ninaingiaje humo....?
 
usipate hasira,
hizi ni store za bongo tu grafani11
Humu ndani kuna wakinadada ambao kila siku ukisoma post zao hakosi kurusha dongo kwa wanaume utafikiri Lady Jay Dee. Akitoa machozi, kesho wanaume kama mabinti, keshokutwa Yahaya .Busara ni kuishi pekee yako kama huwawezi na sio kutia sumu mioyo ya wenzenu. Kama wewe ni mvivu wa kumuomba Mungu akupe mwenzi mwema (Na wengine hata nyumba za ibada hawazijui, kila siku sehemu za kula bata na ofisini hata michango yao humu kila siku wanalaumu wanaume wasiowatoa OUT) hawatapata mume mwema yoyote zaidi ya vicheche wenzao tu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom