Mwanamke, Hata wewe unayo haki ya kutoa talaka...!

Mwanamke, Hata wewe unayo haki ya kutoa talaka...!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
slide-123.jpg

Kuna idadi kubwa ya wanawake ambao wanakaa kwenye ndoa wasizoridhika nazo, ndoa zenye kuwafuja na kuwatesa, ambazo kwao zimepoteza maana na hawana sababu ya msingi kuishi humo. Lakini wanawake hao wamejikuta wakiendelea kuishi ndani ya ndoa hizo kwa hofu tu.

Wamekuwa wakiogopa kudai talaka kwa kudhani kwamba, wao hawapaswi kuomba talaka, bali wanaume ndio wanaopaswa kufanya hivyo na pia wamekuwa wakiamini kwamba, mwanamke kuanza kuomba talaka ni aibu kwa jamii.
Lakini mbaya zaidi ni ile hofu wanayokuwa nayo kuhusu kile ambacho wanaume zao wanaweza kuwafanyia wanapoomba talaka. Huhofia kwamba, kama wanaume hawaridhiki na wao kuomba talaka, wanaweza kuwafanyia vitendo viovu baada ya talaka.

Huogopa kwamba, wanaweza kuwanyang’anya watoto, huogopa kwamba, wanaweza kuwafanyia fujo kila watakapokutana nao, huogopa kwamba, hawataweza kuwagawia mali waliyochuma pamoja na pia kuna hofu kwamba, wanaweza kuwauwa, hasa ikiwa ni juhudi ya kuzuia uwezekano wa kuja kugawana mali.

Ukweli ni kwamba, wanawake hawa wanapaswa kujua kwamba, wao hawawezi kujua vipengele vingi au vyote vya kisheria. Kwa sababu hiyo, wanapohisi kwamba, hawawezi tena kuvumilia vurugu za kindoa zinazowakabili, wanapaswa kuwaona wanasheria ili kuyaendesha mambo kisheria zaidi.

Kama hawana uwezo kifedha, siku hizi kuna taasisi zinajua namna ya kuwasaidia wanawake hawa, hata kama hawana uwezo. Taasisi kama TAWLA au WLAC zimekuwa zikifanya kazi hiyo kwa muda mrefu sasa na zimesaidia wengi.

Kwa hiyo badala ya mwanamke kuumia kwenye ndoa ya mateso kwa kutojua afanye kitu gani, anaweza kuwaona wataalamu wa sheria kutoka katika taasisi kama hizo au kutoka kwa wanasheria binafsi. Hawa wanajua hata namna ya kumfanya mwanaume mkorofi ambaye baada ya kupewa talaka anaweza kuwa kama mbweha badala ya binadamu, ajirekebishe na kufuata sheria za nchi.

Kukaa kwenye ndoa kwa sababu mwanamke anaogopa mabavu ya mwanaume ni dhana ya kale sana. Inabidi ifikie mahali ambapo mwanamke yuko huru kuanzia ndani mwake (Mawazoni na nafsini) hadi nje. Mwanamke anapaswa kujua kwamba, wakati mwingine hafungwi na mwanaume, bali hujifunga mwenyewe…….
 
Hapo hakuna Ujanja!

Either MWANAUME akupe au MAHAKAMA ndo ikupe talaka. Ila mwanamke kama mwanamke huwezi kumuandikia Mumeo Talaka 3. Hata ukijitia nunda bado hizo talaka zako sio Legally Recognized, bado ni mumeo!

Mfumo dume bado sanaaa kwenye sekta ya sheria.
 
Yeah nakubaliana na wewe lara 1, lakini kama umenisoma vizuri ninamaanisha kwamba, mwanamke anaweza kutdai talaka na kumuacha mume mkorofi kwa kufuata sheria na akamuach huyo mume na kupewa haki zake zote anazostahili ikiwapo kinga ya kutobughudhiwa na huyo mume.

Sijui umenipata..?
 
Last edited by a moderator:
Humu ndani kuna wakinadada ambao kila siku ukisoma post zao hakosi kurusha dongo kwa wanaume utafikiri Lady Jay Dee. Akitoa machozi, kesho wanaume kama mabinti, keshokutwa Yahaya .Busara ni kuishi pekee yako kama huwawezi na sio kutia sumu mioyo ya wenzenu. Kama wewe ni mvivu wa kumuomba Mungu akupe mwenzi mwema (Na wengine hata nyumba za ibada hawazijui, kila siku sehemu za kula bata na ofisini hata michango yao humu kila siku wanalaumu wanaume wasiowatoa OUT) hawatapata mume mwema yoyote zaidi ya vicheche wenzao tu.
 
kwa upande wangu naona bado mfumo dume upo na unatukandamiza sisi wanawake na tunakuwa duni kimawazo , kifikra na kunyonywa haki zetu za msingi, ndo mana tunaogopa kuomba talaka ilhali ni haki yetu pia
 
yyani umenibarikije grafani 11, kwa hoja yako ungekuwa karibu ningekupa high 5 kwani umeongea point iliyobora zaidi watu wamezidi kujichanganya hata nyumba aza ibada hawazijui unafikiri mume mwema utapata wapi kama huudhuriii kwenye nyumba za ibada? utapata vicheche vyenzako tu na mwishoe kuambulia mijeredi katika NDOA
 
Last edited by a moderator:
Hapo hakuna Ujanja!

Either MWANAUME akupe au MAHAKAMA ndo ikupe talaka. Ila mwanamke kama mwanamke huwezi kumuandikia Mumeo Talaka 3. Hata ukijitia nunda bado hizo talaka zako sio Legally Recognized, bado ni mumeo!

Mfumo dume bado sanaaa kwenye sekta ya sheria.
lara 1 mdogo wangu mwanamke anahaki ya kudai talaka lkn sio kutoa talaka nafikiri ndicho alichomaanisha Mtambuzi.

lakini pia kwa experience yangu wanawake wengi waliodai talaka zao hasa kwa wale niliowashudia wengi ambao ni waislamu walikutana na pigo kubwa sana la mume kukataa kumpa talaka na hii kwao imekuwa ni adhabu kali sana manake asipokupa talaka huwez kuolewa tena hivyo utabaki tu kuwa mtaliki lkn usiye rasmi.

kifungu hiki na chenyewe bado kina mnyima mwanamke haki yake ya msingi ya kupata maisha ya amani na furaha anayotakiwa kuyapata. mwanamUME anapokataa kutoa talaka hawez kulazimishwa na mahakama atoe talaka na akisema huyu bado nampenda hata kama ni ya uongo hakuna jins ambavyo mahakama inaweza kutengua kauli hii hivyo badala ya kuwa na unafuu kwa mwanamke imekuwa ni adhabu tena mbaya sana.

IKUMBUKWE KWAMBA TALAKA SIO DHABU ILA KUKATAA KUTALIKI NI ADHABU TENA MBAYA SANA KWA MWANAMKE
 
lara 1 mdogo wangu mwanamke anahaki ya kudai talaka lkn sio kutoa talaka nafikiri ndicho alichomaanisha Mtambuzi.

lakini pia kwa experience yangu wanawake wengi waliodai talaka zao hasa kwa wale niliowashudia wengi ambao ni waislamu walikutana na pigo kubwa sana la mume kukataa kumpa talaka na hii kwao imekuwa ni adhabu kali sana manake asipokupa talaka huwez kuolewa tena hivyo utabaki tu kuwa mtaliki lkn usiye rasmi.

kifungu hiki na chenyewe bado kina mnyima mwanamke haki yake ya msingi ya kupata maisha ya amani na furaha anayotakiwa kuyapata. mwanamke anapokataa kutoa talaka hawez kulazimishwa na mahakama atoe talaka na akisema huyu bado nampenda hata kama ni ya uongo hakuna jins ambavyo mahakama inaweza kutengua kauli hii hivyo badala ya kuwa na unafuu kwa mwanamke imekuwa ni adhabu tena mbaya sana.

IKUMBUKWE KWAMBA TALAKA SIO DHABU ILA KUKATAA KUTALIKI NI ADHABU TENA MBAYA SANA KWA MWANAMKE
gfsonwin hebu rudi kwanza.
Hapo kwenye RED ulikuwa unamaanisha MWANAMKE AU MWANAUME...?
 
Last edited by a moderator:
Binafsi nadhani mlolongo mzima huu wa talaka huwa mgumu kutokana na mfumo mzima wa ndoa...

Kuanzia siku ya kwanza, muanzilishi wa safari ya ndoa huwa ni mwanaume na jamii nzima imempa mamlaka hayo...

Kumbukeni kuwa mwanaume ndiye wa kuanza kutongoza, kutoa mahari na wakati mwingine kuandaa sherehe ya harusi...

Sasa kwa mfumo huo jinsi ulivyo unaweza kuona ni kwa kiasi gani mwanamke anatengenezewa mazingira ya kutojiamini...

Mwanamke anakuwa ni kama chombo tu kinachotafutwa, kinachowekwa ndani na hatimaye kinachomilikiwa...
 
yyani umenibarikije grafani 11, kwa hoja yako ungekuwa karibu ningekupa high 5 kwani umeongea point iliyobora zaidi watu wamezidi kujichanganya hata nyumba aza ibada hawazijui unafikiri mume mwema utapata wapi kama huudhuriii kwenye nyumba za ibada? utapata vicheche vyenzako tu na mwishoe kuambulia mijeredi katika NDOA
Mh, napata wasiwasi na huo ushauri wako, huko kwenye nyumba za ibada sidhani kuna uhakika wa 100%
Kuna wanandoa wamekutana huko kwenye nyumba za ibada lakini ndoa zao zinakwenda harijojo, na wengine wameshaachan kitambooo...

Hebu fanya kijiutafiki kidogo utaujua ukweli ladyfurahia...
 
Last edited by a moderator:
Hapo hakuna Ujanja!

Either MWANAUME akupe au MAHAKAMA ndo ikupe talaka. Ila mwanamke kama mwanamke huwezi kumuandikia Mumeo Talaka 3. Hata ukijitia nunda bado hizo talaka zako sio Legally Recognized, bado ni mumeo!

Mfumo dume bado sanaaa kwenye sekta ya sheria.

nimekupenda leo. Kumbe you have got your feminine side?
I had no clue
 
nimeshafanya utafiti wa ukweli kwa 99.9% kwenye nyumba za ibada unapata wa ukweli labda awe ameingia mtu mwenye tamaa zake na kujifanya kondoo kumbe ni mbwa mwitu hapo sawa , nionavyo mm kwenye nyumba za ibada unampata yule aliyetoka kwa Bwana si macheche wa humu jf cc
Mh, napata wasiwasi na huo ushauri wako, huko kwenye nyumba za ibada sidhani kuna uhakika wa 100%
Kuna wanandoa wamekutana huko kwenye nyumba za ibada lakini ndoa zao zinakwenda harijojo, na wengine wameshaachan kitambooo...

Hebu fanya kijiutafiki kidogo utaujua ukweli ladyfurahia...
 
Hii sasa ..............
Napita tu hapa Mtambuzi
endelea kutambuka
 
Last edited by a moderator:
Binafsi nadhani mlolongo mzima huu wa talaka huwa mgumu kutokana na mfumo mzima wa ndoa...

Kuanzia siku ya kwanza, muanzilishi wa safari ya ndoa huwa ni mwanaume na jamii nzima imempa mamlaka hayo...

Kumbukeni kuwa mwanaume ndiye wa kuanza kutongoza, kutoa mahari na wakati mwingine kuandaa sherehe ya harusi...

Sasa kwa mfumo huo jinsi ulivyo unaweza kuona ni kwa kiasi gani mwanamke anatengenezewa mazingira ya kutojiamini...

Mwanamke anakuwa ni kama chombo tu kinachotafutwa, kinachowekwa ndani na hatimaye kinachomilikiwa...

Niliwahi kuyasema haya.
Binafsi mie huwa napinga sana kuhusu swala la MAHARI. nilisimama kidete kwa dada yangu kuozehwa bila kulipiwa mahari, ingawa baba alitaka sana kuchukua hiyo mahari lakini nilimwambia toka apokee mahari kwa dada zangu waliotangulia ni kitu gani amenufaika nacho au amebadilika kimaisha kwa kiasi gani.
Alikubaliana na mimi japo kwa shingo upande.

Na nilimwambia dada yangu kama maisha ya ndoa yakimshinda ajiondokee maana hatukuchukua chochote kwa mumewe...
 
nimeshafanya utafiti wa ukweli kwa 99.9% kwenye nyumba za ibada unapata wa ukweli labda awe ameingia mtu mwenye tamaa zake na kujifanya kondoo kumbe ni mbwa mwitu hapo sawa , nionavyo mm kwenye nyumba za ibada unampata yule aliyetoka kwa Bwana si macheche wa humu jf cc
Unajidanganya ladyfurahia...
Naomba uniwie radhi kutofautiana na wewe, lakini ukweli ni kwamba unawadanganya wenzio..
 
mbona ujanitag kwenye list yako hapo chini mkuu? Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
humu ndani kuna wakinadada ambao kila siku ukisoma post zao hakosi kurusha dongo kwa wanaume utafikiri lady jay dee. Akitoa machozi, kesho wanaume kama mabinti, keshokutwa yahaya .busara ni kuishi pekee yako kama huwawezi na sio kutia sumu mioyo ya wenzenu. Kama wewe ni mvivu wa kumuomba mungu akupe mwenzi mwema (na wengine hata nyumba za ibada hawazijui, kila siku sehemu za kula bata na ofisini hata michango yao humu kila siku wanalaumu wanaume wasiowatoa out) hawatapata mume mwema yoyote zaidi ya vicheche wenzao tu.
mmh!!! Hapa umekuwa too biased aisee broda!!
 
Back
Top Bottom