Mwanamke anayetafuta mwanaume utamjua tu

Mwanamke anayetafuta mwanaume utamjua tu

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Mchunguzi Mahiri ndani ya Kusini mwa jangwa la Sahara bado nipo na nitaendelea kuwepo huku nikiheshimu sheria zote jamiiforums.

Kuna njia nyingi sana za kumtambua mwanamke anayetafuta mwanaume lakini leo nataka kuizungumzia hii.

MWANAMKE KUTEMBEA PEKE YAKE KILA MAHALI:
Hii njia inatumiwa sana na wanawake hasa maeneo ya mijini, utakuta dada mzuri kila anapoenda anapenda kwenda peke yake yote hiyo ni kuwatengenezea mazingira ndugu watongozaji.

KWANINI WANATUMIA NJIA HII?
Kwasababu wamegundua kuwa wanaume wengi wamekuwa waoga sana wa kuwafata pindi wanapokuwa na wenzao, ni nadra sana kumkuta wanaume anaenda kumuomba namba mwanamke ambaye yupo na marafiki zake wengi huwafata wanawake ambao wapo peke yao hivyo kushinda na marafiki zao mara kwa mara huwa wanahisi wanapoteza bahati zao.

Ikitokea ametoka kazini anarudi nyumbani akiona wenzake wanaondoka basi yeye atawaambia wenzake "mimi bado nipo kuna kazi namalizia" akiwa anaenda kanisani ataiacha familia nzima iende yeye atakuwa wa mwisho au atatangulia. Wanawake wa aina hii hupenda kwenda maeneo ya mikusanyiko peke yao iwe movie, bar, restaurant au shopping wakiwa peke yao kwa kuamini maeneo hayo wanaweza kupata wanaume wa ndoto zao.

NOTE:
Si kila mwanamke anayependa kutembea peke yake anatafuta mwanaume japo uchunguzi wangu umebaini zaidi ya asilimia 80 ya wanawake wanaotembea peke yao kila mara wanakuwa wakitafuta mume.
 
Principle ni hii...Two is a company....three is a crowd...oUVeRrrr...!!
 
Nilidhani atakuwa anakata kiuno barabarani!
Sa kukaa tu mwenyewe ndo iwe mtu anataka mwanaume?
Hataaaki tu!
Period!
 
Umesahau ile ya kuanza kwenda kanisani na kushiriki mapambio.
 
Sio kila mwanamuke akienda baa anajiuza wengine waenda baa kwa kuwaona wazee wa ngwasuma, kwenye pochi zao wana hela za matumizi na usafiri wa kurudi majumbani mwao: FM Academia

ukisoma mwisho kabisa mwa thread yangu utanielewa zaidi
 
Back
Top Bottom