Mke ni msaidizi tukumbuke
ila siku hizi wababa loh sio wa kusaidiwa tena ..ni mizigo
umenikumbusha siku za nyuma kidogo,( niliolewa wkt nasoma chuo), nilipopata kazi mume wangu aliacha kutoa matumizi ya nyumbani ( japo yy alikuwa na kazi nzuri zaidi na yenye kipato kikubwa kuliko mimi)..
miezi kadhaa ya kwanza nilijitahidi kuhudumia familia kwa kila k2(chakula,nk)..kila nilpomuuliza pesa ya chakula/matumizi alitoa visingizio (ilimradi hana hela) siku moja alisafiri safari ya km wiki moja hivi na akaondoka bila kuacha hata senti...na hapo nyumbani tulikuwa na wtt wetu 2 wadogo(under 5 years) na ndugu zake 3 watu wazima pamoja na msichana wa kazi..
nilichokifanya, nikahakikisha chakula cha wtt wangu kipo(uji, mtori n.k)halaafu nikamnunulia dada mkate nikamwambia sina hela ya chakula kwa hivo ataishi na mkate..(nilifanya hivi ili dada wa kazi asiondoke awalee watt alikuwa dd mzuri) (nilificha akiba kdg ili ht mtt akiumwa niweze kwenda hosp)
kwa kifupi nyumbani kukawa hakupikwi k2, kwa wk nzima, hakukuwa na chochote cha kupikwa, umeme nao uliisha kwa hivo tukawa tunaishi na mishumaa.. siku hiyo mr akarudi ktk safari, ilikuwa usiku, akakuta giza, akauliza mbona giza? hakujibiwa, akaenda kununua umeme, taa ikawaka..
tukalala bila kula chochote(hakukupikwa)..asb tukaamka tukaenda kazini, jioni tukarudi nyumbani, tukalala tena kavu kavu, (hakukupikwa).. tulipofika kitandani akaniuliza hivi hii nyumba siku hizi wa2 hawali chakula? tangu nimekuja sijaona msosi wowote! nikamuuliza, unakumbuka mara mwisho wewe ulitoa pesa ya matumizi (chakula n.k) mwaka gani? swali hilo lilimuingia barabara kwani hakunijibu..
kesho yake nilipotoka kazini, nilikuta friji imejaa vyakula hadi haifungi..mchele umenunuliwa kg 100, n.k ilimradi nyumba ilijaa vyakula kila kona..
nikasema kimoyomyo kumbe unajua kuhudumia familia ee, na kuanzia hapo akajua majukumu yake km baba..
kwa hivo ni kweli mwanamke akishakuwa na kipato, mume anajitahidi kukwepa majukumu yake na kuyahamisha kwa mke au kumtegea..