Mwanakijiji apendekeza mabadiliko ya Mfumo wa Uongozi CHADEMA

Gurti

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
211
59
Nimesoma makala ndefu ya Mwanakijiji ilikuwa ni makala nzuri sana.

Ninaomba niweke moja ya hoja yake ambayo ni kama pendekezo lake kwa Chadema ili waweze kupambana na CCM inayojivua gamba. Anashauri kuwa viongozi wa Chadema ambao ni wabunge na wenye majukumu mengi ya kibunge, wanaweza kuzidiwa na CCM inayojipanga vizuri. Yeye akashauri kuwa ni vizuri Chadema ikafuata system ya Marekani ambayo Marais wao si viongozi wa Vyama vyao.

Yaani kwa ufupi ni kwamba, Viongozi wote ambao ni wabunge wachague moja. Aidha uwe mbunge au uwe kiongozi wa Chama. Kwa mantiki hiyo, Viongozi wa Chadema kama Mbowe, Zitto, Said Arfi ( Vice chairman) , Mnyika nk ambao ni wabunge wachague moja. Ama wawe wabunge au wawe viongozi wa CHADEMA.

Kwa maelezo yake 2010, Chadema ilishindwa kufanya mambo mengi kutokana na viongozi wake wengi kuwa wagombea. Slaa akawa peke yake.

My take; Mimi nimeshawishika kwa sehemu kubwa na ushauri huu, wadau naomba maoni yenu.

Kumbuka:
Chadema wanapenda viongozi wao wote wawe wabunge kama namna ya kupunguza gharama ya kutunza viongozi wao kwa kuwa fedha za kuwalipa mishahara hawana. Dr Slaa peke yake anawezeshwa. Wengine ambao ni wabuge hawalipwi kabisa.
 
My take; Mimi nimeshawishika kwa sehemu kubwa na ushauri huu, wadau naomba maoni yenu.

Kumbuka; Chadema wanapenda viongozi wao wote wawe wabunge kama namna ya kupunguza gharama ya kutunza viongozi wao kwa kuwa fedha za kuwalipa mishahara hawana. Dr Slaa peke yake anawezeshwa. Wengine ambao ni wabuge hawalipwi kabisa.[/QUOTE]

Mungu wabariki viongozi wetu kwa kujitolea kwenu!
 
WAzo zuri ila inabidi kufanyiwa detailed analysis kuona positive na negative impacts kwa chama kama wataamua kufuata pendekezo la hoja ya Mwanakijiji
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ni ushauri mzuri kimsingi!...
Lakini kwa mtizamo wangu si suala la kusema lifanyiwe kazi that immediate, maana sasa hivi kwa maneno mengine ni kuwaambia waachie nafasi zile zingine tofauti na ubunge!...
We could take your idea onboard for the Next season elections, lakini kwa sasa tutajikanganya!..acha wamalize salama ubunge wao, then wazo hili litapitia kwenye chekecho la vikao vya chama na kupimwa applicability yake!
Ni challenge nzuri sana
!!
 
hoja yako ni nzuri,lakini si mwafaka kwa kipindi hiki. Acha wabunge wawe pia viongozi wa chama hadi CDM itakapokomboa nchi ndipo mgawanyo wa ki madaraka (CHAMA + SERIAKALI) utakapojipambanua
 
hii ni mipango ya muda mrefu kwakweli maana inabidi kujua source ya fund kwa CHADEMA na bajeti zao mapato na matumizi then kinachobaki unajua kumhudumia mwenyekiti na sekretariet yake inahitaji gharama kubwa sana itabidi CHADEMA wajipange kwanza kwa hilo!
 
Nape=mkuu wa wilaya, Makamba=alikuwa m'bunge, Chiligati na Mkuchika=wabunge na mawaziri.
 
hii ni mipango ya muda mrefu kwakweli maana inabidi kujua source ya fund kwa CHADEMA na bajeti zao mapato na matumizi then kinachobaki unajua kumhudumia mwenyekiti na sekretariet yake inahitaji gharama kubwa sana itabidi CHADEMA wajipange kwanza kwa hilo!

Anza na CCM avatar yako haiendani na unayoandika
 
Mawazo mazuri lakini yanahitaji kujadiliwa na kufikiriwa kwa kina.
 
Wakuu
Nami pia nilisoma makala ya Mwanakijiji ilikuwa mtandaoni kwenye gazeti la Tanzania Daima. Nilivutiwa na jinsi Mzee Mwanakijiji alivyochambua huku kujivua gamba kwa ccm na mwelekeo wa chadema kama chama cha upinzani. Nilichopenda zaidi sio tu kwamba alitoa madhaifu ya chadema kwa mtindo/aina ya uongozi ilio nao sasa bali alienda mbali zaidi kwa kutoa suluhisho kwa kutenganisha uongozi wa chama na vyeo kama Ubunge na Uraisi. Nakubaliana nae kwamba imefika wakati hizi siasa za mapokeo tuachane nazo, nani alisema mgombea U-raisi lazima awe mwenyekiti wa chama? Kama ccm wanafanya hivyo haina ulazima na chadema wafanye hivyo hivyo. Ni vizuri wakawa na njia mbadala na hii ndo itawapa wananchi mwanya wa kuilewa vizuri chadema kwamba maslahi ya nchi ni zaidi kuliko Uongozi wa chama. Chama bado nikichanga na kinaitaji watu wakujitolea kufanya kazi ya kukikuza, sasa unapogawa mda wa mbunge, bungeni na chamani ni wazi kwamba majukumu yatamzidi na midhani inaweza kuwa bungeni zaidi kuliko kwenye shughuli za chama. Sasa tuwape watu wengine jukumu la kuendesha chama kila siku huku majemedali wetu wakitupigania bungeni.
Mwanakijiji kama utasoma ujumbe wangu, nikushukuru kwa makala yako yenye ufafanuzi na uchambuzi wa kina.
 
WAzo zuri ila inabidi kufanyiwa detailed analysis kuona positive na negative impacts kwa chama kama wataamua kufuata pendekezo la hoja ya Mwanakijiji

Its too early to do that chama bado kichanga hii iwe dhana tu huku wakijiandaa kufanya hivyo lakini for the time being its going to cost them a lot. Mwanzo wa kitu kunahitaji kukifungamanisha kwanza na baadaye ndiyo ufanye de centralization. Kumbuka CCM ni imara kwa sababu walianza na chama kushika hatamu lakini hatari ni kuwa democracy inavyozidi kuwa huo mfumo unakuwa out dated na hivyo utakufa kama CCM hajiandai ku work on competitive basis na decentralization. Lakini CHADEMA inatakiwa iwe opposite ya CCM mpaka iwe consolidated na inapofikia imejenga coherence ndipo hapo ianze kutengamanisha hizo kofia. So far kama wame mwacha mmoja nje ambaye ni senior its enough baadaye wanaendelea kui de associate mpaka itafikia optimal level.
 
Nimesoma makala ndefu ya Mwanakijiji ktk gazeti la mwanahalisi wiki hii- ilikuwa ni makala nzuri sana. Ninaomba niweke moja ya hoja yake ambayo ni kama pendekezo lake kwa Chadema ili waweze kupambana na CCM inayojivua gamba. Anashauri kuwa viongozi wa Chadema ambao ni wabunge na wenye majukumu mengi ya kibunge, wanaweza kuzidiwa na CCM inayojipanga vizuri. Yeye akashauri kuwa ni vizuri Chadema ikafuata system ya Marekani ambayo Marais wao si viongozi wa Vyama vyao. Yaani kwa ufupi ni kwamba, Viongozi wote ambao ni wabunge wachague moja. Aidha uwe mbunge au uwe kiongozi wa Chama. Kwa mantiki hiyo, Viongozi wa Chadema kama Mbowe, Zitto, Said Arfi ( Vice chairman) , Mnyika nk ambao ni wabunge wachague moja. Ama wawe wabunge au wawe viongozi wa CHADEMA.
Kwa maelezo yake 2010, Chadema ilishindwa kufanya mambo mengi kutokana na viongozi wake wengi kuwa wagombea. Slaa akawa peke yake.
My take; Mimi nimeshawishika kwa sehemu kubwa na ushauri huu, wadau naomba maoni yenu.

Kumbuka; Chadema wanapenda viongozi wao wote wawe wabunge kama namna ya kupunguza gharama ya kutunza viongozi wao kwa kuwa fedha za kuwalipa mishahara hawana. Dr Slaa peke yake anawezeshwa. Wengine ambao ni wabuge hawalipwi kabisa.


He he heeeee kweli mfa maji haishi kutapa tapa, mkifuata tu huo ushauri mmejimaliza , na hivi chama kiko under liquidation
 
Ubunge ndio unawapa mshahara hivyo kuwa na nguvu ya kupigana zaidi. Jiulize kwa nini Maalim Seif aliolewa na ccm kirahisi hivyo bila hata kulipiwa mahari na tena akafika mahali akaanza kampeni kwamba uchaguzi usifanyike Zanzibar ili apate kula kidogo (hakuamini kwamba angekuja kupewa cheo cha mama wa nyumbani ikulu)
 
wazo baya,sio lazima tuige,sisi tunautaratibu wetu na ndio huo tunaoutumia,siwezi kurisign kokote
 
Nimekuwa nikishauri hivi kwa muda mrefu katika post zangu zote huko nyuma. Chadema wakiingia kwenye mtego wa CCM wa serikali na chama kuwa "convoluted into one thing" watakuwa wamekosea na muda si mrefu Inertia ya Serikali wavuta wote watajikuta wameshatumbukia. Zitto tayari alishazama.

Kwa mfumo kama huu chadema ikichukua serikali, hakuna chama! Pale makao makuu itabaki kama jumba la makumbusho kama ilivyo Rumumba. Wanaharakati wote watageuka watendaji wa serikali na inertia ya serikali itawazamisha wote halafu huku makao makuu hakuna mtu wa kuwarudisha kwenye msitari, itakuwa worse than CCM nakuambia.

Kwa sasa hivi Chadema haina serikali, ila ina wabunge ambao focus yao ni kwenye uwakilishi. Hawa inatakiwa wapunguziwe majukumu ya Kichama, wachukue wengine (ila wawe wanaharakati bora kabisa). Chama kibaki kuwa unit ambayo iko focused kwenye siasa na kukitawanya chama huko vijijini walipo wananchi.

Utekelezaji wake unaweza usiwe wa mara moja, lakini that has to be a direction. Chama na serikali in one is always a recipe for disaster. All communism systems had this formula and it has almost always failed!!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom