Upo sawa kakahoja yako ni nzuri,lakini si mwafaka kwa kipindi hiki. Acha wabunge wawe pia viongozi wa chama hadi CDM itakapokomboa nchi ndipo mgawanyo wa ki madaraka (CHAMA + SERIAKALI) utakapojipambanua
Teh teh teh baba umeuaaaaa!!!!'Ubunge ndio unawapa mshahara hivyo kuwa na nguvu ya kupigana zaidi. Jiulize kwa nini Maalim Seif aliolewa na ccm kirahisi hivyo bila hata kulipiwa mahari na tena akafika mahali akaanza kampeni kwamba uchaguzi usifanyike Zanzibar ili apate kula kidogo (hakuamini kwamba angekuja kupewa cheo cha mama wa nyumbani ikulu)
Nimesoma makala ndefu ya Mwanakijiji ktk gazeti la mwanahalisi wiki hii- ilikuwa ni makala nzuri sana. Ninaomba niweke moja ya hoja yake ambayo ni kama pendekezo lake kwa Chadema ili waweze kupambana na CCM inayojivua gamba. Anashauri kuwa viongozi wa Chadema ambao ni wabunge na wenye majukumu mengi ya kibunge, wanaweza kuzidiwa na CCM inayojipanga vizuri. Yeye akashauri kuwa ni vizuri Chadema ikafuata system ya Marekani ambayo Marais wao si viongozi wa Vyama vyao. Yaani kwa ufupi ni kwamba, Viongozi wote ambao ni wabunge wachague moja. Aidha uwe mbunge au uwe kiongozi wa Chama. Kwa mantiki hiyo, Viongozi wa Chadema kama Mbowe, Zitto, Said Arfi ( Vice chairman) , Mnyika nk ambao ni wabunge wachague moja. Ama wawe wabunge au wawe viongozi wa CHADEMA.
Kwa maelezo yake 2010, Chadema ilishindwa kufanya mambo mengi kutokana na viongozi wake wengi kuwa wagombea. Slaa akawa peke yake.
My take; Mimi nimeshawishika kwa sehemu kubwa na ushauri huu, wadau naomba maoni yenu.
Kumbuka; Chadema wanapenda viongozi wao wote wawe wabunge kama namna ya kupunguza gharama ya kutunza viongozi wao kwa kuwa fedha za kuwalipa mishahara hawana. Dr Slaa peke yake anawezeshwa. Wengine ambao ni wabuge hawalipwi kabisa.