Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,328
Mwanaharakati Marcosy Albanie ametoweka nyumbani kwake baada ya kufuatiliwa na watu wasio julikana kwa kipindi cha siku kadhaa.
Mtakumbuka mara ya mwisho Bwana huyu alionekana kwenye kipindi cha kipima joto kilicho rushwa kwenye runinga ya ITV kikimshirikisha yeye, mbunge wa Singida mashariki Mh Tundu Lissu pamoja na naibu spika Mh Job Ndugai.
Chanzo: Mabadiliko.
NB. Marcosy anajishughulisha na taasisi ya kiraia inayo fuatilia mwenendo wa shughuli za bunge pamoja na masuala mengine katika jamii.
Kutoka kwenye gazeti la Mwananchi ijumaa, Machi 15, 2013. Uk 8.
Akizungumza- jana kutoka alikokimbilia,- Marcossy alisema ameamua kuikimbia nyumba yake kwa ajili ya usalama na kubainisha kuwa taarifa ya vitisho vyake aliwasilisha kwa Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRD-Coalition,) Onesmo Olengurumwa.

Na Frederick Katulanda | Mwananchi | Ijumaa, Marchi 15 2013
Mwanaharakati Albanie Marcossy, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Civil and Political Right Watch (CPW) ameondoka nyumbani kwake Kimara Dar es Slaam akidai kilichomwondoa ni kupokea vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana.
Marcossy, awali aliwahi kufanya kazi kwenye Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) ambako alikuwa mmoja wa waliopeleka mashtaka kwenye Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Septemba 28, 2012 dhidi ya serikali kutokana na mauaji yenye utata ya watu 23 akiwamo Mwandishi wa habari Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.
Akizungumza jana kutoka alikokimbilia, Marcossy alisema ameamua kuikimbia nyumba yake kwa ajili ya usalama na kubainisha kuwa taarifa ya vitisho vyake aliwasilisha kwa Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRD-Coalition,) Onesmo Olengurumwa.
Olengurumwa alithibitisha kupokea taarifa hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alipoulizwa jana alisema polisi hawana taarifa kuhusiana na kutoweka kwa mwanaharakati huyo wala kutishiwa kutokana na kutopokea taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo