MwanaHalisi yamshambulia Sitta

MwanaHalisi yamshambulia Sitta

Kwanza kabisa nakwambia spade shall never be a spoon. Wewe umetumwa tu kumchafua Said Kubenea, nami najitokeza wazi kabisa kukwambia kwamba huna ubavu wowote wa kuita spade kuwa spoon. Kubenea na mwanahalisi litabakia kuwa gaziti la umma, na litasomwasana mpaka ulie.

Kwanza nikupe kitu cha ajabu sana ambacho ni cha pekee kwa mwanahalisi. Ukifanya jambo zuri kwa taifa wanakutunuku, na wewe huyo huyo utakapoharibu wanakukosoa. Hii ina maana gani? Hawana usabiki, ila huandika habari yakinifu, tofauti na uhuru na mzalendo. Hiyo ya kununuliwa inakuhusu wewe na kununuliwa kwako kumchafua Kubenea.

Kwanza hauna hata consistency katika hoja zako, mtu aliyenunuliwa anaweza akageuka na kuandika habari kame hii? Hebu angalia habari za uhuru na mzalendo.
"Mzimu wa Ricmond wamwandama Lowassa" katika toleo la jana huku akimpachika Jacob Daffi jukumu la kuiandika taarifa hiyo.

MY TAKE;
Kubenea hamchukii aliyekuwa, kama mtu binafsi, na huenda hana tatizi nae, yeye anazungumzia suala la Richmond. Anazungumza unafiki katika kupooza suala hilo kana kwamba ni mkuu pekeyake ndio alihusika. Kwanini mswada ulikufa haraka haraka, kama sio unafiki wa Ndioooo. Mwacheni. Hata yule nanihii alisema kuna mengi hatujasema, kasome hansadi.

Tutasoma sana Mwanahalisi.
watake wasitake MWANAHALISI KILA WIKI TUTASOMA NA HABARI ZAKE TUTAENDELEA KUZIAMINI
KUNA UBAYA GANI MWANAHALISI KUANDIKA SITTA ALIUZIMA MJADALA WA DOWANS?????????
 
Hizi siasa zingine ni mufilisi sana...hivi wangapi hapa tunaomchukia Lowasa tukikutana na katika level hiyo (pesronal) tutaacha kumsalimia na pengine kutabasabu kidogo? Hili litakuwa na maana tunakubali madudu aliyoyafanya? Sidhanii hivyo.
 
The evidence ni kitendo chake cha kuwashambulia vinara wa vita dhidi ya ufisadi. Kila mtu anauheshimu mchango wa Sita na Mwakyembe katika kupingana na rushwa nchi hii.

Ndugu yangu Mwita mpambanaji wa kweli wa vita dhidi ya ufisadi ni lazima atambue kwanza jambo muhimu ni kubadilisha mfumo wa utawala tulionao. Bila hivyo watu wataingia madarakani ni wasafi,baada ya muda watachafuka mfano mzuri Mkapa. Sijawahi sikia akina Sitta wanaongelea kubadili mfumo. Maadui zao ni RA,AC na EL. Sasa Kubenea anapowafungua bongo wasomaji wake kwamba hawa jamaa hawana kitu ni mafisadi tu kama wenzao,baadhi yetu tunasema jamaa kanunuliwa. Mpambanaji wa kweli atapendekeza tubadilli mfumo,Katiba mpya,atapinga matendo yote ya uonevu wanayowafinyiwa wananchi,ataungana hata na vyama vya upinzani na taasisi za kiraia kupinga uonevu dhidi ya wanasiasa wa upinzani na wananchi wanaopambana na maovu ktk jamii.
 
Kubenea kanunuliwa siku nyingi na mafisadi, ndio mabwana zake wapya. Hapo anamsalimia fisadi Lowassa kwa unyenyekevu kama mke amsalimiapo mume wake. Habari yenyewe ya wiki hii yenye kuhusu Richmond kumwandama Lowassa ni ya kinafiki. Ni danganya toto eti kutaka watu wadhani kuwa bado anaendelea kumgonga Lowassa, ndani ya habari yenyewe kaandika utumbo mtupu kuwa eti serikali nzima ndio iliyohusika na Richmond badala ya kusema ukweli kuwa wahusika wakuu wa rushwa hii ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Nazir Karamagi.

Kubenea ana roho nyepesi kama kuku, ndio maana kanunuliwa na mafisadi na sasa anaelekea kufilisika.
 
Kubenea ni jembe lililowafunuwa Watz na kuwafanya chupi za mijizi ya CCM kuwaka moto. Wanavyomuandama, ni sababu tosha kabisa kwamba kwashika pabaya sana, kuanzia top wao JK kwenda chini.

Wanahaha hovyo hawajui wasemalo, wala wafanyalo. haya tena madudu mengine ya TIB haya hela zilizorejeshwa zachotwa. Kubenea alilianzisha hili kwa kuwataja wezi hawa katika gazeti lake mwaka 2007 orodha ya wezi 11 kuanzia JK. hakuna gazeti jingine lilikuwa na balls la kutraja majina hayo.

Kubenea ni mkombozi wa wanyonge -- HONGEERA SAANA. ENDELEA NA NYUNDO ZAKO!
 
Kubenea kawekwa mfukono na mafisadi. Watu makini wamebaini jambo hilo miezi kadhaa sasa. Kwa msiomjua Kubenea, siyo shujaa hata kidogo mnaodhani. Kubenea ndio amenyea kambi ya wapambanaji wa ufisadi na kuhamia kwa mabwana zake wapya Edward Lowasa na Rostam Aziz.
Wapambanaji wa ufisadi Samuel Sitta na Reginald Mengi wanafahamu fika kuwa Kubenea hayuko nao tena, ana roho nyepesi kama kuku na amepakatwa na mafisadi.

Sitta kama kawaida yake ya kusema ukweli daima na kutokuwa mnafiki, ndio maana akaamua kumsema live kubenea kwenye TV kuwa ameshanunuliwa. Sote tunajua kuwa Kubenea kanunuliwa. Anatia aibu!!!
 
Mafisadi wanaamini kuwa everybody has a price. Kumbe kwa kujitutumua kote huko siku zote hizi bei ya Kubenea ni rahisi kama kuku na sasa anawatumikia kina Lowasa, Rostam na Chenge kama Absalom Kibanda wa Tanzania Daima.
 
Kubenea kanunuliwa siku nyingi na mafisadi, ndio mabwana zake wapya. Hapo anamsalimia fisadi Lowassa kwa unyenyekevu kama mke amsalimiapo mume wake. Habari yenyewe ya wiki hii yenye kuhusu Richmond kumwandama Lowassa ni ya kinafiki. Ni danganya toto eti kutaka watu wadhani kuwa bado anaendelea kumgonga Lowassa, ndani ya habari yenyewe kaandika utumbo mtupu kuwa eti serikali nzima ndio iliyohusika na Richmond badala ya kusema ukweli kuwa wahusika wakuu wa rushwa hii ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Nazir Karamagi.

Kubenea ana roho nyepesi kama kuku, ndio maana kanunuliwa na mafisadi na sasa anaelekea kufilisika.

Mkuu Fareed umesema ukweli mtupu! Kubenea is no more...
 
Hivi watu wanashindana kwa hoja au Nguvu?ina maana mkitofautiana mawazo nyie ndio maadui kwenye mawazo mengine?haiitaji kwenda shule ujue kuwa picha hiyo ilikuwa katika msiba, dressing ya Kubenea ni kielelezo tosha,

Bado Kubenea anaandika kwa weledi wa taaluma kwa ku balance habari zake na sio lazima ukiandikwa vizuri kwa jema la leo ndio tiketi ya kuandikwa vizuri daima ukikosea unachanwa tuu

Mkapa alisha sema tuache uvivu wa kike
 
Waberoya na The Romantic..........................! Mimi hapa sitasema tena

Ila nilishangaa na bado naendelea kushangaa jinsi ambavyo watanzania wanachezewa Olympic ya Kisiasa

Nitumie nafasi hii,niendelee kuwapa moyo Raia Mwema....Watanzania wanawaamini sana msije mkaingia kwenye mtego wa kuwahujumu wananchi na kuminya demokrasia.Jenerali Ulimwengu na timu yako,endeleeni kuwapa watanzania kile wanachostahili.Msije mkageuka kuwa gazeti la udaku wa kisiasa,watanzania makini hawhitaji hilo
 
Hivi Ofisi ya Spika iliyoko Urambo nani anaitumia sasa. Hiki Kibabu kilidhani kitakuwa Spika wa Milele, Kimrithishe Mke wake, Mtoto wake na wajukuu zake. Huyu hana Tofauti na Gadafi aliyeamua Kujenga Makao Makuu ya AU kwao Siirte
 
kanunuliwa kwa shiling ngapi?kupigwa picha anapeana mkono na lowasa sio solid evidence,hata mbowe anapeana mkono na jk,.tuletee ushahidi wa maana sio hiyo picha.

Hapo umesema mkuu! We need critical evidence.
 
please over please mod, tuanze kupewa mtihani hapa JF kuna watu vilaza sana, aisee si mshaambiwa hatujadili picha bali tunajadili jinsi kubenea alivyoshuka kiwango kwenye uandishi kiasi kwamba anatujengea imani kuwa amefichwa kwenye kwapa za mafisadi.
 
Unakumbuka Baada ya CCM kutangaza kujivua Gamba na Nape kutembelea Media House zote za Tanzania? Matokeo ya Visiting ile ni

A. Magazeti yafuatayo yalikataa kuimba Wimbo wa kujivua Gamba na sasa yamekua ni Maadui wa CCM-Sitta
1. Mwanahalisi
2. Mwananchi
3. Tanzania Daima

B. Magazeti yafuatayo yaliamua Kucheza Ngoma ya Kujivua Gamba ya akina nape
1. Raia Mwema ( Siku hizi nimeacha kulinunua)
2. Uhuru
3. Nipashe

Kwa Hiyo Kundi A limekuwa ni Adui mkubwa wa CCM-Sitta
Sawa KAKA kubenea
 
Watanzania bwana, watu wamekubuhu kwa uwongo. Ni kwa sababu, taifa halina maadili.

Mtu mzima anaandika Kubenea kanunuliwa kwa sababu, eti amekutwa akisalimiana na Lowassa?

Mimi nilikuwapo siku ambayo picha hii imepigwa. Ilikuwa ni kwenye msiba wa Dany Mwakiteleko, ambapo Kubenea aliingia hapo na kumkuta Lowassa akiwa amefika kuhani. Sasa ulitaka asiende kumsalimia? Hata kama kuna ugomvi kiasi gani, kulikuwa hakuna njia ya kutoenda kumsalimia.

Huyu jamaa alivyokubuhu kwa uwongo, anamtaja Ngurumo kwamba anamjua vema Kubenea, kwamba hakwenda shule. Lakini hasemi amesoma kwa kiwango gani.

Lakini hata kama hakwenda shule kwa kiwango cha Chuo Kikuu, lakini anachokifanyia taifa ni kikubwa kuliko hao waliopata elimu – waliohesabu madarasa.

Kisha mtoa mada anasema ‘Kubenea anatoka Mafia.” Ana uhakika na hilo? Mimi najua wapo watu humu ndani, kazi yao kuchafua wenzao. Ndiyo hao waliowahi kuandika humu ndani Kubenea kwenda kugombea ubunge Mafia.

Uchaguzi umekwisha hakuoenekana na mpaka leo hajaonekana huko.

Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Kubenea ni mmoja wa vijana wachache waliofanikiwa kuanzisha gazeti na kuleta mabadiliko nchini…

Pesa SIO sabuni ya roho.....pesa ni kitendea kazi mkuu!!! Na ndio maana WHITE HAIR (aka Sungura Mweupe!!!) kaitumia kama silaha ya kutekeleza mpango wake wa kujisafisha!!!!
Pesa sabuni ya roho!
 
Kubenea kanunuliwa siku nyingi na mafisadi, ndio mabwana zake wapya. Hapo anamsalimia fisadi Lowassa kwa unyenyekevu kama mke amsalimiapo mume wake. Habari yenyewe ya wiki hii yenye kuhusu Richmond kumwandama Lowassa ni ya kinafiki. Ni danganya toto eti kutaka watu wadhani kuwa bado anaendelea kumgonga Lowassa, ndani ya habari yenyewe kaandika utumbo mtupu kuwa eti serikali nzima ndio iliyohusika na Richmond badala ya kusema ukweli kuwa wahusika wakuu wa rushwa hii ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Nazir Karamagi.

Kubenea ana roho nyepesi kama kuku, ndio maana kanunuliwa na mafisadi na sasa anaelekea kufilisika.
wewe una akili za kuku kama huoni makosa ya SITTA
 
Back
Top Bottom