...Nimekwambia waulize watoto au wajukuu ili ujishangae mwenyewe....
...Kwa kuwa umejifungia kwenye kachumba kadogo kanakoitwa "Mahaba kwa Chama", hautaweza kuona zaidi ya hivyo ulivyoona, lakini ukitoka nje ya hako kachumba kalikoubana ubongo na kupelekea moyo kufanya kazi ya ubongo, utaona kumbe upo kwenye nchi nzuri Tanzania, yenye watu wazuri na yenye watu wabaya pia waliosambaa kama mchanga wa bahari kwenye makabila, dini, vyama, ngo, mitaa na vilabu tofauti tofauti...
....Utawaona mamia ya watu makini na maelfu ya watu wabovu/wezi ndani ya CCM, utawaona makumi ya watu makini na maelfu ya wabovu/wezi ndani ya Chadema, kama utakavyowaona pia makumi ya watu makini na maelfu ya wabovu/wezi ndani CUF na NCCR, na list inaendelea...