MwanaHalisi yamshambulia Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MwanaHalisi yamshambulia Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Oct 28, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Shutuma za Sitta dhidi ya Kubenea kwamba sasa kanunuliwa na mafisadi kama alivyozitoa katika kipindi chake katika ITV zimejibiwa na na gazeti hilo wiki hii katika tahariri yake iliyoanzia ukurasa wa mbele.

  Kubenea anataka kuonekana ni jembe lisilotetereka katika kuwaumbua mafisadi na wale wanaofuatilia kwa makini stori za gazeti hilo watagundua kwamba hana marafiki, na hasa wa mafisadi, wapambe wao na wote wale manafiki wanaojifanya kuupiga vita ufisadi, kumbe wao ndiyo mafisadi wakuu.

  Soma mwenyewe hiyo tahariri hapa chini.  _____________________


  TAHARIRI: Sitta ‘kanyea kambi'


  SAMWEL Sitta ametuhumu gazeti hili, kuwa linatumiwa na watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini ili "kumchafua" yeye na wenzake.

  Alikuwa akiongea kwenye kipindi cha "Dakika 45" juzi Jumatatu, kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

  Sitta alionekana na kusikika akisema, gazeti hili lilikuwa madhubuti na imara; lakini sasa limeanza kuyumba kutokana na hatua yake ya kushambulia wale wanaopigana na ufisadi nchini, hasa yeye.

  Alikwenda mbali hata kutuhumu mtendaji mkuu wa Hali Halisi Publishers Limited (HHPL) na mchapishaji wa MwanaHALISI, Saed Kubenea, kuwa amenunuliwa na mafisadi.

  Waziri huyu wa Afrika Mashariki anajua fika kwamba gazeti la MwanaHALISI, wamiliki wake, waandishi wake, hawana mkataba naye wa kumwandika anayotaka.
  Sisi tuko kazini. Tunaangalia wale tunaowatumikia; nao ni umma wa Tanzania na jamii pana. Siyo Samwel John Sitta wa Urambo, kibarua katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

  Si gazeti, kiongozi wake wala mwandishi wa MwanaHALISI, aliye na mkataba wa kumwandika Sitta kama anavyotaka. Tuna kanuni ya kuandika yeyote na chochote kama alivyo au kilivyo na siyo kwa upendeleo.

  Kama Sitta aliwahi kuandikwa vizuri ajue; na labda akumbuke kuwa, hakuwa ametoa chochote, ameahidi chochote au amefurahisha gazeti kwa lolote lile; bali kwa kuwa alikuwa kwenye mstari wa ukweli na haki.

  Pale atakapotoka kwenye mstari; akajiingiza kwenye fikra, kauli na matendo ambayo tunaona na kuamini kuwa siyo sahihi; yanayokinzana na ukweli na haki kwa jamii tuliyomo; tutamwonyesha kwa jamii kama alivyo – bila woga wala upendeleo.

  Nani amemtuma Sitta kushiriki vita dhidi ya MwanaHALISI? Nani atamwamini kwa kauli zake ambazo hawezi kuthibitisha? Je, kwamba gazeti limeandika asichopenda au ambacho hapendi wengi wajue juu yake, huko ndiko kushirikiana na mafisadi?

  Siyo sahihi kutumia "ufisadi" kujenga urafiki au uadui. Fisadi na hata wanaowashabikia, watafahamika, hasa kwa matendo yao na mapema, kwa kauli zao. Lakini kwa Sitta kujaribu kukimbia kivuli chake, na kutafuta kuegemeza woga wake kwa MwanaHALISI; hakika ni woga uliopitiliza kwa mtu wa umri, elimu, uzoefu kazini na nafasi aliyonayo serikalini.

  Hata hivyo, Sitta siyo mwanzilishi wa "mapambano dhidi ya mafisadi" nchini. Hata kwa hatua ya Bunge kuchunguza mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond wakati yeye akiwa spika, hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuona ufahari na kujitwisha ushujaa.

  Bunge lilikuwa linafanya mwitikio tu wa mfululizo wa ripoti za vyombo vya habari jasiri ambavyo vilikuwa vikiandika, bila kukoma, ufisadi uliokuwa umefanywa nchini. Richmond ni "cha mtoto" kwa ufisadi mkuu ambao bunge lake halikushughulikia na bado liko kimya juu yake.

  Aidha, ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilichoanika orodha ya watuhumiwa 11 wa ufisadi hapo 15 Septemba 2007 kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam; wakati viongozi wa Sitta – katika chama chake na serikali wakidai kuwa "huo ni uzushi mtupu."

  Ukweli ni huu: Walioanikwa ni viongozi wakuu wa nchi wa sasa na waliopita ambao wamekuwa waajiri wa Samwel John Sitta. Bado ni waajiri wake. Hawezi kujitenga nao. Hawezi hata kuwaambia uso kwa uso kwa ukali wa mkweli na mhalifu. Anarukia MwanaHALISI!

  Gazeti hili lina rekodi ya kuwa pekee lililoripoti kwa kina na ufasaha tuhuma ya kila mmoja miongoni mwa waliotajwa kwenye orodha ya mafisadi. Mara baada ya kuchapisha taarifa za watuhumiwa na picha zao, baadhi walitishia kwenda mahakamani; lakini tulisimama imara hadi wakayeyuka.

  Hata kinachoitwa "ujasiri wa wapinga ufisadi" ndani na nje ya bunge, kilitokana na mfululizo wa uibuaji uoza serikalini. Uibuaji huo ulifanywa na baadhi ya vyombo vya habari; gazeti hili likiwemo au likiongoza.

  Bali tukubali kuwa Sitta ana matatizo na wenzake. Ni muhimu amalizane nao vizuri au vyovyote vile bila kujenga viinimacho. Kwa mfano, Sitta anataka kujinasua kutoka kwenye tuhuma za usaliti wa chama chake kwa kile kinachoitwa "kuanzisha chama ndani ya chama."

  Anatuhumiwa kuwa mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Jamii (CCJ) wakati bado ana nafasi ya juu katika uongozi wa serikali ya chama kilichoko madarakani. Hakika hili siyo tatizo la MwanaHALISI; hata pale gazeti litakapokuwa limeandika taarifa zake kwa kunukuu vyanzo ambavyo siyo rahisi kuvikanusha.

  Hapa, badala ya kutuhumu gazeti letu, ni vema akajibu madai ya "washirika wake," hasa Fred Mpendazoe, anayelalamika kuwa Sitta alimtosa. Mpendazoe ambaye wakati huo alikuwa mbunge wa Kishapu (CCM), anasema aliamua kuacha ubunge ili kuimarisha CCJ, wakati wakisubiri "Sitta na wenzake."

  Gazeti halihusiki na chochote walichoahidiana wakati huo. Halijapata ushahidi kama walidhulumiana. Halijapokea taarifa iwapo kuna ambao hawakupata mgawo wa fedha zilizochangwa na wahisani wa ndani au nje kwa ajili ya kazi ya akina Sitta na Mpendazoe.

  Tunachojua na tulichochapisha ni juu ya ujio wa CCJ, nani alikusanya fedha na kutoka kwa nani; nani alilipia kodi ya pango ya ofisi, nani alilipa mishahara ya watumishi wa mwanzo na nani alilalamika, kwamba "wenzangu wameniacha njiapanda."

  Hadi sasa waanzilishi watatu wamesema kile wanachodai wanaelewa vema na hata kwa kiapo. Hao ni Mpendazoe, Dickson Ng'hily na Daniel ole Porokwa. Katika hili, na hasa kama Sitta anadhani tunalikuza kwa kuliandika, alaumu wenzake na siyo chombo cha habari wala wanaokimiliki.

  Jingine ambalo tunahisi linaweza kuwa limemfanya Sitta aanze kushambulia MwanaHALISI, ni pale gazeti lilipomtuhumu hujuma kwa kufunga mjadala wa kashfa ya Richmond. Wakati huo alikuwa spika. Hapa tulisema bayana kwamba hatukubaliani naye. Hata sasa hatukubaliani naye.

  Ni kunyenyekea kwake kwa serikali au kutafuta "mwafaka" wa haraka kwa maslahi binafsi ambako kulimfanya azime mjadala muhimu kwa taifa. Bado tunapinga hili. Tunalipinga kwa kuwa linaathiri vibaya hata kauli zake za sasa za kutaka kampuni ya kufua umeme ya Dowans isilipwe zionekana kama mzaha.

  Kama kwa msimamo wetu huo anaona ndio tunashirikiana na mafisadi kumchafua, basi amefikia ukingoni. Sharti arudi nyuma au abomoe ngome ya kiza kilichomfunika macho na akili.

  Na nani amempa Sitta madaraka ya kuamua kuwa hiki ndiyo ufisadi na kile siyo ufisadi? Kama angekuwa mkweli na safi, asingekuwa anatumikia ambao tayari wamethibitika kuwa mafisadi – kwa kauli, vitendo na kisheria.

  Gazeti hili haliwajibiki kuomba ruhusa kwa Sitta ili lirekodi kuyumba au kupotoka na hata kutetereka kwake. Tuna haki ya kuona, kuchambua, kutolea maoni na hata kuchapisha kile tunachoona na kusadiki juu yake na juu ya yeyote na chochote kile.

  Atakayejaribu kutunyang'anya haki na uhuru wetu huo, kwa kutuita washirika wa "mafisadi," tutampinga. Tutaomba wadau wa habari kumpinga. Lakini pia tutamwita fisadi mkuu anayejaribu kutunyang'anya haki ya kufikiri, kuandika ukweli na kutoa kauli.

  Sitta ananyea kambi.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nishaisoma hii juzi, ngoja nipite kwanza, nitarejea. Sitta anahangaika tu.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sitta ashukuru utawala wa kulindana wa JK -- angekuwa ameshatimuliwa kwa usaliti wake. CCM ni chama cha ajabu sana duniani -- kuna mafisadi, wezi, manafiki, wasaliti, macowboy (wanaotembea na silaha viunoni, wazinzi -- lakini bado iko tu madarakani!

  In this country we have sheep for human beings!
   
 4. j

  jigoku JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Nina choamini mimi Sitta ni mnafiki na wala simuamini hata kidogo na wala sipendi awe kiongozi wangu hata siku
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwanza hajajibu kwa nini alijenga ofisi ya Spika kule Urambo -- Jee aliahidiwa kuwa Spika milele? Eti halafu JK ndiye alikwebnda kuifungua!
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  1.Clean out of CCM but dirty when in?

  2. Nani mwanzilishi wa vita dhidi ya ufisadi? SERIKALI, CHADEMA AU VYOMBO VYA HABARI?

  3. Je wote Mpendazoe na Sitta ni wanafiki?

  4. Kumbe kuna vyama vinakusanya pesa toka ndani na nje kwa ajili ya kujiendesha? Watarudishaje hizo pesa kwa wafadhili?. Niimemkumbuka sana Nyerere baba yangu.

  Siasa za tanzania kumbe feki. Kila siku kelele majukwaani, kumbe ndani yake, unafiki, ubinafsi,chuki na pressure toka nje. Kumbe tuna vibaraka hapa tanzania. Nilikuwa nashangaa why? Vyombo vya dola vinasema maandamano no, Wanajitokeza vibaraka waliokwisha pewa pesa wanataka kulazimisha. ninyi AN, Mzee wa viwanja sana na wewe Yero tumewashtukia.
   
 7. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Sita na Mwakyembe wanaimarisha fikra na mtazamo wangu binafsi kuwa... TAIFA HALIJAPATA NA HALITAPATA SHUJAA NDANI YA CCM TANGU ZAMA HIZI ZA VYAMA VINGI. Sita na Mwakyembe ni wachumia tumbo ambao taifa hili halijawahi kushuhudia.
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  CCM is a flop!
   
 9. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Kibarua katika serikali ya JK, Kanyea kambi, APRIN kwa mamilioni, Nyumba ya spika Urambo duu? Mitambo ya mtumba then symbion, huyo aliyenyunyiza huo unga ni Mwakyembe, sitta: hapana, ni Manyanya, Sitta: hapana, ni Chenge Sitta: hahahahaha!, maboza ya maji yanalipwa na bunge kwenda kwa dada mmoja pale kinondoni, mimi ni mtumishi na Mage ni mtumishi lazima kila mmoja apate nyumba ya kununua ya serikali na bado ile ya mjengoni hataki kuhama, hayo ni machache tu niliyokutana nayo kwenye nuuz mbalimbali.

  My take: Ningekuwa Rais huyu asingekuwa waziri wangu, ningekuwa mwanaurambo huyu asingekuwa mbunge wangu. Huyu ndo anatakiwa alipe hela ya Dowans, Tanesco walisema jamani tununue hii mitambo, Zito akapiga debe jamani tununue, Idrisa akataka kuachia ngazi Sitta akakomaa, wenye mamlaka wakamuogopa leo anasema hatulipi, kivipi?

  Wa TZ tusiwe mambumbu badala ya kujifanya wajuaji na kale kakampuni kanaitwa REX Attorneys kanaendelea kulipwa mabilioni kwa kukata rufaa bado interest ya deni inaongezeka kila siku, ilikuwa kama Bil 94, leo tuko 111 bil, mpaka tunalipa inaweza kuwa imefika 130 bil. Tumeuingia mkenge na wapiga debe kina Sitta bado wanatupoteza, wanaotaka kuandamana waelekee kwa sitta. Ngeleja nenda kwa Al-Azawi yule jamaa atakusikiliza tumpoze kidogo watu wakafanye kazi, hizi siasa zenu mkapige majimboni kwenu kazi za kitaalam muwaachie wenyewe.
   
 10. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Hapo mwanahalisi wameguswa pabaya....teh teh teh thas why nimeacha kununua magazeti yao siku hizi...
   
 11. N

  Ndole JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hata mimi ila nitakwambia baadae why...
   
 12. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #12
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Asante kaka umesema ukweli! Tatizo ambaye ni Rais na wale wapiga kura wa Urambo hawayaoni hayo kuhusu Sitta! Hata kama wanayaona au kuyasikia hawayatafakari na kuchukua hatua!
   
 13. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #13
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Sina hana jipya anapiga mayowe..anabahati mbaya watz wameshtukia mapema sana
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  basi kama vipi itabidi ayazoe mwenyewe ...kwa nini alizima ule mjadala? sasa hivi ungetuka mambo yemeshaisha zamani ..kweli ccm ni mafisi
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mmm!hapa nimeshindwa kuvumilia huo ni uongo na unajua kwamba ni uongo,tuendelee na hayo mengine lakini hii yako ni uongo!!!!
   
 16. k

  kambambovu Member

  #16
  Oct 29, 2011
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku za mwizi ni arobaini, Sitta siyo mkweli, anapretend kujifanya msafi katika kundi la wachafu. Hiyo ndiyo hatima ya Mnafiki, na bora angekuwa ananyamaza kimya anvyozidi kukanusha shutuma ndiyo kwanza anakuwa kama anamwaga petrol katika moto unawowaka.
   
 17. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mzee Six anatspatapa tu. Tumhurumie jamani.
   
 18. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  magamba ndani ya ccm yako ya aina mbili njano na kijani ila yote ni magamba tu, na sasa wantumia nyumdo kupigania vichwani na jembe kizikzna ardhini Sitta ni walewale ambao wameifikisha nchi hii hapa
   
 19. F

  Fareed JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kubenea ni kweli kashanunuliwa na mafisadi siku nyingi sana. Hilo jambo linaeleweka, na MwanaHalisi limekuwa likiyumba sana. Watu wengi hatulisomi tena, ni aibu kwa Kubenea kuwa mtumwa wa kina Rostam Aziz na Edward Lowassa kwa ajili ya vipesa vidogo to. Atabaki kuwa masikini wa akili na mali milele huyu Kubenea
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Eti tumhurumie wewe nani? Wewe si mateka wa Mbowe tu..
  Sitta ni msanii kawaingiza mkenge CDM
   
Loading...