Mwanafunzi wa Feza ashangaa wanaofeli mtihani wa NECTA

Dogo yupo sahihi
 
Nimecheka sana wallahi. Maelezo uliyoweka hapo na picha husika ya tukio vimeshindwa kulandana

Picha inaashiria kuwa Betting ni adhabu inayomkabili St Kayumba
 
Hao ni vilaza, wachawi, wenye wivu na husda. Pia wapewe kombe au kama vipi serikali ianzishe tuzo ya maskini bora wawe wanashindana maana haiwezekani binadamu mwenye akili timamu ajivunie shida na umaskini. Ni punguani tu atajisifia ujinga na kumponda aliyefanikiwa.

Hapa angekuwa wa mwisho na kupata dungu hao wangekuja kumpongeza, akili zao ziko reverse.
Kwanza huyo dogo hapo alipo tiyari anawazidi akili na uzee wao. Katoa ushauri, maoni na kajibu maswali ila wanamkasirikia kama vile kaweka sheria.
1. Kasema wanafunzi wajipime na mitihani mingine maana NECTA ni rahisi. Kama mtu unaona ni upuuzi sio kesi, kawaazishie wanao ligi ya singeli na kucheza rede wasubiri NECTA.

2. Kasema NECTA ni rahisi. Ni maoni yake, kama unapinga mwambie mwanao NECTA ni ngumu akiingia kwenye mtihani azimie.

3. Kashangaa wanaofeli. Ajabu iko wapi? Mbona humu kuna watu mnashangaa wanaofaulu kama yeye, tena yeye hajawatafutia visingizio waliofeli ila nyinyi mnataja mara umaskini, mara yeye kisa wana hela.

Au serikali ianzishe tuzo ya umaskini maana watu wanaupenda sana. Ndio maana mwanasiasa akijiita mnyonge raia wanajigaragaza mtaani, wakati familia yake haijui shida.
 
Simshangai huyo mtoto.Mimi mwenyewe nilipokuwa mdogo nilikuwa nashangaa mtu anafeli vipi.Mpaka namaliza chuo kikuu sikuwahi kufeli.Ila maisha yamenipiga na kitu kizito kichwani najiuliza waliotajirika wamewezaje?🤣🤣🤣
Pole mkuu
 
Sasa mzazi kutwa kufatilia mambo ya kina mondi kajala konde kiba na kwa upande wa baba kutwa kubishana mambo ya mpira [emoji1]
Mtoto atatoboa kweli

Ova
 
Sasa mzazi kutwa kufatilia mambo ya kina mondi kajala konde kiba na kwa upande wa baba kutwa kubishana mambo ya mpira [emoji1]
Mtoto atatoboa kweli

Ova
Na hili swala litaendelea kuwepo kadri siku zinavyoenda, wazazi wasipoona umuhimu wa shule, hawawezi somesha watoto wao na kuwakazania wasome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…