Mwanafunzi Mtanzania kakutwa amekufa/ameuawa Bangalore India

Kwa wale watakao penda na kupata nafasi wanaweza kuja hapa Russian culture karibu na agakani.. unakutana kwa ajili ya kukusanya michango ya kusafirisha Mwili wa mapendwa wetu IMRAN.. kikao kinaendelea hivi niandikavyo nadhani tutakuwa hapo mapaka saa mbili

Asante Mzee Malecela kwa kuandaa mkutano huu
 
Poleni wafiwa.........

Kwa wale wanaoifahamu familia ya Iddi Simba, marehemu ni mtoto wa dada mdogo wa Mama Iddi Simba.

Tupo pamoja.
 
Poleni wafiwa.........

Kwa wale wanaoifahamu familia ya Iddi Simba, marehemu ni mtoto wa dada mdogo wa Mama Iddi Simba.

Tupo pamoja.

ina maana mama wa Saida Kilumanga sio??? sad nashindwa kudigest hili tukio la kikatili kwa huyu mtoto jamani!!!!!!!!!
 
dah, inasikitisha sana...rip...yaani mtu anamchinja mwenzake kabisaaa, mmmmh...
 
Mimi nasubiri kuona jinsi Ubalozi wetu India pamoja na Foreign office jinsi watakavyo re-handle hili saga. Haiwezekani kila uchwao watanzania wauawe kikatili kwenye nchi ambazo siku zote raia wao wanapewa protection wanapokuwa Tanzania.
 
Mimi sidhani kama wahindi ni racist, labda nationalist ila ni watu wanaojali mali mno. Wakisikia wewe unatoka Africa wanajua kama utakua mlala hoi. Wanadharau wahindi wenzao wanaotoka Afrika pia(same race). My 2 cents. RIP Imrani
 
Si wa Afrika hwpendani, bali watanzania zaidi, manake wabongo wengi tabia zetu ni mbaya kuliko tukiwa ughaibuni pengine kuliko hata mapopo (Nigerians), wapo wengi wetu ambao hawataki kabisa kujulikana kama wao ni wa Tz (visa na sababu nyingi!).

Hao wahindi unkienda kila mahali wana ushirikiana utazani mchwa hata kwenye maovu wapo pamoja!

Sad news, kama upo India saidia mzee Ben...

R. I. P Imran
 
Mimi nasubiri kuona jinsi Ubalozi wetu India pamoja na Foreign office jinsi watakavyo re-handle hili saga. Haiwezekani kila uchwao watanzania wauawe kikatili kwenye nchi ambazo siku zote raia wao wanapewa protection wanapokuwa Tanzania.

Forget about Ubalozi, siyo mara kwanza jambo la namna hiyo kutokea. In fact nikiwa kule masomoni tulipatwa na misiba miwili (mji niliyokuwa) niliyohusika hatua zote. Msiba mmoja tulisafirisha na mmoja tulizika kulekule. Msiba wa kwanza ulisababishwa na ajari, jamaa wa Ubalozi alikuja na alishia kuchukua PDM zake. Na msiba wa pili hatukuweza kujua chanzo cha kifo, maana jamaa report iliyotolewa ni natural death.

Ninachotaka kusema, msitarajie lolote kwa hao jamaa.
 
Kama hali ni hii bas haina haja ya kuwepo na Ubalozi inaudhi sana
 
Anaitwa IMRAN MTUI nirafiki yangu wa karibu... it is soo sad indeed.. amakutwa amekatwa mikono na miguu inasemekana baada ya kuuawa alitupwa relini na train ikampitia so kichwa kimesagika...

inaonekana wahindi wameanza vita rasmi ya kuwauwa watanzania kama (sio waafrica wasomao huko) kwa tz huyu ni mwanafunzi wa tatu kwa muda mfupi sana

Jioni ya kifo chake alimuaga rafikie wanae isha nae wote pale Saski Manshion, Gopal Reddy Layout, 1st Main (kwa wale waishio india msiba uko hapo) kuwa natoka akarudi badae ingawa hakuingia ndani akaacha pikipiki yake na mlinzi anasema alikuwa ameongozana na muhindi mmoja..so kesho yake asbuhi rafikie akapata taarifa ya kifo chake

RIP IMRAN you will be missed

He's one of the coolest people i've ever met,alikuwa mtu fresh sana,pia mpenzi mkubwa sana wa Reggae na culture ya Rastafarianism....Nakumbuka alikuwa akipenda poem za Mutabaruka,aliniambia kuhusu kipande kimoja cha poem hiyo kinachokwenda hivi, "I am da black man coming from da black womb entering in da black world,doing everything in black" Niliyapenda sana maneno hayo kutoka kwenye poem hiyo ya Mutabaruka na kila wakati nilikuwa nikimkumbuka,very sad indeed.
Rest in Peace Imran,we will miss you.
 
Hao maafisa wenyewe wameweka kindugu,hawajui uongozi na wajibu wao ni nini.hope mtakubaliana na mimi kama htjawahi kukutana na maafisa wa balozi zetu usibishe.
 
- Wakuu habari zinasikitisha sana, lakini pia bado tunahitaji all the facts I mean sioni sababu ya kutukanwa kwa ubalozi wetu huko so far wakati sioni all the facts, ingawa sio siri habari inasikitisha sana na pole wafiwa wote!

- Lakini binafsi, nitasubiri all the facts kwanza kabla ya kuhukumu Wahindi wote Duniani au Balozi zetu zote Duniani kwa kifo ambacho sina all the facts kimetokeaje na sababu zake!

Respect
.

FMEs!
 
Nawashangaa sana mnaosema watanzania hatupendani wakati wazungu na wahindi hao mnao wasifia hata kusalimiana hawasalimiani. Issue inayosumbua watanzania ni umaskini, njaa na maradhi.

Watanzania tumezoea maisha ya kistaarabu, mfano, ukienda pale kisutu na kariakoo wahindi 4-6 hulala chumba kimoja haijalishi wamelalaje lakini hili kwa mtanzania tena mwenye uwezo wakufika nchi za watu hatopenda maisha ya namna hiyo, labda wazamiaji na waliofeli maisha.

Lakini wahindi siwalaumu kwa hilo kwa sababu ni maisha wameyazoea hapa india, nimetembelea states za Delhi, Bombay, Uttarakhand, Kelara, n.k. mitaani maisha ni yale yale.

mwanamke wa kihindi na hasa wahindu hawaruhusiwi kumsalimia mwanamme yeyote kwa kushikana mikono kama siyo ndugu yake au mmewe. Sasa huko kusema wahindi wanapendana nikupi???

Kama ndugu zangu hanjaishi india msitoe comments ambazo hazina hakika. Mpaka mda huu naandika maoni haya nipo uhindini na maisha ni noma kishenzi. Kuna mhindimmoja anaishi kampala na tayari kaoa myarwanda tumekutana naye hapa ktk hoteli alikuwa na ndugu zake na akaapa kwamba hawezi kurudi kuishi india kwa zababu ya utamaduni na maisha ya kishenzi ya hapa nchini kwao.

Watanzania nawaomba tujitahidi tumpambane na rushwa lakini hakuna nchi nzuri kuishi ambayo wageni wanaikimbilia kama Tanzania pamoja na umaskini wa watu wake.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
- Wakuu habari zinasikitisha sana, lakini pia bado tunahitaji all the facts I mean sioni sababu ya kutukanwa kwa ubalozi wetu huko so far wakati sioni all the facts, ingawa sio siri habari inasikitisha sana na pole wafiwa wote!

- Lakini binafsi, nitasubiri all the facts kwanza kabla ya kuhukumu Wahindi wote Duniani au Balozi zetu zote Duniani kwa kifo ambacho sina all the facts kimetokeaje na sababu zake!

Respect
.

FMEs!

Heshima nyingi mzee

Imran amekutwa hana kichwa (data nilizozipata jana msibani), kakatwa mikoni na miguu.. police india wamesema ni suicide...how!!!! mtu anaejiua anajikata kichwa na miguu na mikono????????? tufikirie tena upya.

jana hiyo hiyo muivory cost kauawa hapo hapo bangalore..waziri wao wa mabo ya nje kaenda.. sisi katumwa police wetu wa kibongo...soo sad

RIP IMRAN
 
Heshima nyingi mzee

Imran amekutwa hana kichwa (data nilizozipata jana msibani), kakatwa mikoni na miguu.. police india wamesema ni suicide...how!!!! mtu anaejiua anajikata kichwa na miguu na mikono????????? tufikirie tena upya.

jana hiyo hiyo muivory cost kauawa hapo hapo bangalore..waziri wao wa mambo ya nje kaenda.. sisi katumwa police wetu wa kibongo...soo sad

RIP IMRAN
poleni wafiwa...
 
Back
Top Bottom