Mwanafunzi afa akitoa mimba ya mwalimu

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
740
Hebo oneni haya mambo jamani, sijui jamii yetu inaelekea wapi? Halafu eti biti wa miaka 19 kidato cha kwanza!

Mwanafunzi afa akitoa mimba ya mwalimu
na Suleiman Abeid na Zuhura Waziri, Shinyanga

MWANAFUNZI mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa akisoma kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya Katente wilayani Bukombe mkoani Shinyanga amekufa baada ya kutoa mimba ya miezi saba ambayo inadaiwa alipachikwa na mwalimu wa shule ya msingi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, amemtaja mwanafunzi aliyekufa kuwa ni Shukuru Edward na kwamba tukio hilo lilitokea Agosti 12, mwaka huu saa 8 usiku wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya serikali wilayani Bukombe.

Kufuatia kifo hicho, Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia wazazi wawili wa mwanafunzi huyo waliotajwa kwa majina ya Bw. Edward Shamba (52) na Bi. Anastazia Edward (48) pamoja na Bw. Anthony Edward (34) ambaye ni mwalimu anayedaiwa kumpa mimba hiyo.

Wengine waliokamatwa wakituhumiwa kusaidia utoaji wa mimba hiyo ni Bw. Robert Mashuku “Bujilima” (36) ambaye ni Daktari, Bw. Julius Maganga (45) mhudumu wa chumba cha maiti katika hospitali ya serikali wilayani Bukombe na Bi. Maria Andrew (26) dada wa marehemu.

Akifafanua, Kamanda Ibrahimu alisema baada ya kubainika kuwa mwanafunzi huyo ana mimba, mtuhumiwa Bw. Anthony akishirikina na Bi. Maria walijaribu kutoa mimba hiyo kwa kutumia dawa za kienyeji lakini ilishindikana na kusababisha kichanga kilichokuwa tumboni kuoza.

Hali hiyo ilimsababishia maumivu makali mwanafunzi huyo ambapo alianza kutokwa usaha katika sehemu za siri, hivyo kulazimika akimbizwe katika hospitali ya serikali Bukombe Agosti 11, mwaka huu baada ya hali kuwa mbaya zaidi.

Hata hivyo baada ya kufikishwa hospitalini hapo, mwalimu Anthony alitumia kadi yake ya Bima ya Afya kumtibia mwanafunzi huyo huku akiwa ameandika jina la uongo katika kadi za wagonjwa.

Ili kuficha ukweli wa kubainika kuwa mgonjwa huyo ni mwanafunzi, aliamua kuandikisha jina la uongo la Catherine Shamba badala ya Shukuru Edward, maarufu kwa jina la ‘Shamba.’

Kamanda Ibrahimu alisema akiwa hospitalini hapo, mwalimu Anthony alishirikiana na Daktari Mashuku kutoa kwa siri mimba hiyo lakini hata hivyo mwanafunzi huyo alifariki usiku wa Agosti 12, mwaka huu.

Baada ya kufariki mwanafunzi huyo, Dkt. Mashuku akishirikiana na watuhumiwa wengine walimfanyia upasuaji ambapo walitoa kichanga kilichokuwa tumboni chenye jinsi ya kiume kikiwa na umri wa miezi saba na kwenda kukificha katika jokofu la hospitali hiyo bila kuitaarifu Polisi kwa nia ya kuharibu ushahidi.

Hata hivyo baadhi ya raia wema walitoa taarifa Polisi ambao walifika hospitalini hapo na kukuta tayari mwili wa mwanafunzi huyo umechukuliwa na kupelekwa kijijini kwao Imalagigo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

Kutokana na hali hiyo Polisi waliwahi katika kijiji hicho kabla ya mazishi na kufanikiwa kuuchukua mwili huo na kuurejesha hospitalini kwa ajili uchunguzi wa kitaalamu.

Wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, walishangaa kukuta mwili wa kichanga ukiwa umefichwa katika moja ya majokofu yaliyokuwa ndani ya chumba hicho na ilipochunguzwa, ilibainika kuwa ndicho kilichotolewa tumboni mwa marehemu.

Kamanda Ibrahimu alisema baada ya uchunguzi wa kitaalamu, mwili wa mwanafunzi pamoja na kichanga chake vilikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Alisema katika mahojiano ya awali na mtuhumiwa Bw. Anthony, alikiri kumpa mimba mwanafunzi huyo ambaye sasa ni marehemu na kwamba yeye pamoja na watuhumiwa wenzake wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni baada ya uchunguzi kukamilika.

SOURCE: Majira
 
Maadili yameshuka sana siku hizi, hapa dar ukipita mitaa mingi wakati wa usiku utaona watoto wadogo wanakutongoza bila kujali hadhi yako.
Nafikiri sheria zinazotungwa zisilenge wabakaji na wanaowapa mimba wanafunzi bali zilenge vilevile kuimarisha au kusimamia maadili katika jamii.
 
Wakuu lakini na hawa wakusoma vjivazi vyao vinatia utata sana hasa si mnajua na walimu wa sasa ni wa 80's.....nakumbuka nilikuwa nafundisha binti fulani jirani yetu jioni bure....lakini alipokuwa anakuja masomoni ni kama alikuwa kwenye maonyesho ya mavazi....
kitopu si kitopu basi mgongo wote uko wazi huko chini ndio wanaita vile vipedo....ananukia uturi wa kimahaba.....na mimi ni rijali na binadamu ati

sasa nilitaka kusema kuwa 19yrs mi mtu mzima iam sure alikuwa anajua anachokifanya na mwalimu......so tuangalie pande zoote.....mistake wamefanya kuichomoa mimba otherwise...
 
Kuzini Ni Dhambi Lkn Kutoa Mimba Ni Dhambi Zaidi...

Nafikiri Abeid Karume Alikuwa Na Principle Nzuri Za Kudhibiti Uzinifu Zanzibar, Ila Sasa Naona Karume Junior Ameshindwa!!! Kwa Mainland Hali Ni Mbaya, Na Watawala Wameshindwa Kudhibiti Hali...
 
Haya ni matokeo ya unafik uliokithiri katika jamii yetu! Mwanamke wa miaka kumi na tisa anaogopa kuzaa? Tusingekuwa na sheria za kigandamizi kulinda unafik wetu, huyu binti angekuwa hai. Tunawalaumu mabint kwa kututamanisha lakini nenda katika sehemu za starehe uone jinsi vibabu wanavyowachangamkia wafanya kazi ambao bila shaka wana umri wa vijukuu vyao! Hatuoni aibu kutumia lugha zinazokaribia matusi kuwazungumzia wasichana/wanawake tunaowaona wana mvuto, tena kwa sauti kubwa ili jamii itutambue kuwa sisi ni wanaume kweli.

Hatuwezi kulazimisha maadili ambayo hata hapo kale hayakuwepo. Tunasahau kuwa hapo kale, binti akishavunja ungo aliozeshwa kwa sababu walitambua na kukubali kuwa kuna mabiliko katika maumbile na hormones zake. Leo, anaenda shule lakini mabiliko hayo bado yapo pale pale. Kwavile tunaelewa umuhimu wa elimu kwa jamii ni lazima tukubali ku'accomodate' mabadiliko haya katika mabinti wetu. Ni lazima tuwafundishe namna ya kujikinga na pale wanapoteleza tusiwahukumu bali tuwape uwezo wa kuendelea na maisha yao.

Kwa unafik huu tutaendelea kuzika mabinti zetu. Mungu awalaze mahali pema peponi marehemu hawa.
 
Kuzini Ni Dhambi Lkn Kutoa Mimba Ni Dhambi Zaidi...

Nafikiri Abeid Karume Alikuwa Na Principle Nzuri Za Kudhibiti Uzinifu Zanzibar, Ila Sasa Naona Karume Junior Ameshindwa!!! Kwa Mainland Hali Ni Mbaya, Na Watawala Wameshindwa Kudhibiti Hali...

Mkuu, hakuna taifa wala jamii iliyoweza kudhibiti uzinifu. Kinachofanyika ni kuzuia matokeo ya uzinifu (uja uzito) yasionekane. Hata Saudi na Iran watu bado wanazini pamoja na sheria za kikatili dhidi ya wadhinifu. Hata wakati wa Abeid Karume watu waliendelea kuzini. Haipendezi, lakini ni ubinadamu na ni lazima tukubali hilo.
 
jamani kwa binafsi nimesikitishwa sana na hiki kitendo cha utoaji mimba yaani we mwalimu ulichokuwa unafanya na huyu marehemu hukujua kitatokea nini nitamaa hizo wengine wanatafuta watoto wengine mwaua watoto Mungu awasamehe sana.
 
Siku moja nilikuwa namtania mwalimu mmoja kijana kwamba aangalie asije akawa ameenda kufundisha kwa kuwa anataka kuharibu mabinti. Mwalimu huyo alinijibu kuwa zamani waalimu walikuwa wanawatongoza wanafunzi lakini siku hizi nitofauti kwa kuwa wanafunzi ndio hutongoza walimu.

Kwa kauli hiyo ya mwalimu niliona kuwa kuna mazingira mabaya sana kwa walimu mashuleni na hasa pale walimu wa kiume wanapofundisha jinsia tofauti.

Mwalimu mmoja alikuwa anafundisha Jangwani alisema kuwa wanafunzi wake wa biologia walikuwa wanapenda sana somo la reproduction, na hapo walikuwa wakiuliza maswali ya kimtego kwa mwalimu na wanakuwa serious kuliko topic zingine.

ni kwa nini sasa shauku ya kuelewe kwa wanafunzi iwe kubwa kwenye reproduction zaidi ya topic zingine?

Maadili kwa watoto wa kike na kiume ni ya muhimu mno kama tunataka kulinusuru Taifa juu ya matatizo yanayolikabili.
 
Ndg Watanzania,nadhani kikubwa ni kumrudia Mungu.Haya yote yatokeayo yanachangiwa na huu Utandawazi ambao nashawishika kuamini kuwa unatuburuza.Kumomonyoka kwa maadili ktk jamii ni zao la huu utandawazi licha ya kuwa kuna mambo mengne yanayochangia.Lakini kuendelea kupga kelele kuwa maadili yanamomonyoka bila kuwa na mipango madhubuti ya kukabiliana.So wat we do to counteract the effects of this globalization?I think this should be the new direction of this thread.I ll be back with my points/opinions on this.
 
Siku moja nilikuwa namtania mwalimu mmoja kijana kwamba aangalie asije akawa ameenda kufundisha kwa kuwa anataka kuharibu mabinti. Mwalimu huyo alinijibu kuwa zamani waalimu walikuwa wanawatongoza wanafunzi lakini siku hizi nitofauti kwa kuwa wanafunzi ndio hutongoza walimu.

Kwa kauli hiyo ya mwalimu niliona kuwa kuna mazingira mabaya sana kwa walimu mashuleni na hasa pale walimu wa kiume wanapofundisha jinsia tofauti.

Mwalimu mmoja alikuwa anafundisha Jangwani alisema kuwa wanafunzi wake wa biologia walikuwa wanapenda sana somo la reproduction, na hapo walikuwa wakiuliza maswali ya kimtego kwa mwalimu na wanakuwa serious kuliko topic zingine.

ni kwa nini sasa shauku ya kuelewe kwa wanafunzi iwe kubwa kwenye reproduction zaidi ya topic zingine?

Maadili kwa watoto wa kike na kiume ni ya muhimu mno kama tunataka kulinusuru Taifa juu ya matatizo yanayolikabili.

Mbona hata sisi tulikuwa na shauku sana na somo la reproduction! Hii inatokana na kupata nafasi kuzungumzia kitu kinachotuhusu sana lakini kilichofanywa mwiko. Ni maswali gani ya mtego anayoweza kuulizwa mwalimu?

Wajibu ni kwa sisi tulio watu wazima na tuliopitia huko ambako vijana wetu wapo kuelewa na kuto ku take advantage of the situation. Badala ya kujifanya kuwa sote tulikuwa malaika, tuwe humble na kukubali udhaifu wetu.

Hizi draconian laws hazitasaidia lolote. Watu wanapigwa mawe lakini bado wanaendelea kuzini kama kazi!
 
Back
Top Bottom