Mwana FA: Tulilipwa Bilioni mbili na milioni mia moja hamsini na tano baada ya kushinda kesi

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Msanii Hamis Mwinjuma aka mwanafa ameweka wazi kiasi cha pesa walicholipwa na kampuni ya simu iliyokuwa ikitumia nyimbo zao bila ridhaa.

Msanii Mwanafa na AY waliishitaki kampeni hiyo ya simu mahakamani mwaka 2011 na baada ya miaka 7 ya purukushani za mahakamani hatimaye mwaka 2018 walifanikiwa kupata amri ya mahakama ya kuattach akaunti ya benki ya kampuni hiyo na kufanikiwa kupata kiasi cha pesa 2.185 bilioni.

Mwanafa akihojiwa na mtangazaji Salama Jabir amesema pesa hizo zilitolewa kwenye akaunti ya benki ya kampuni hiyo ya simu na kuingizwa kwenye akaunti ya mwanasheria wao kabla ya wao kugawana fedha hizo.

Mwanafa amesema alitumia sehemu ya fedha hizo kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo perfume yake ya falsafa.

Mwanafa hakusita kuelezea historia ya maisha yake jinsi alivyolelewa kwa tabu kwa maisha ya kutanga tanga. Mwanafa amesimulia kuwa mara baada ya mama yake kupata ujauzito wake kulitokea sintofahamu kati mama yake na baba yake. Hali hiyo ilipelekea babu yake mzaa baba kuingilia kati na kumchukua mama yake na mwanafa na kuishi naye mpaka alipojifungua. Baada ya kujifungua babu yake alimrudisha shule mama yake na hivyo yeye (babu mzaa baba) kuendelea kulea kichanga hicho akishirikiana na bibi yake mwanafa wa kufikia (maana bibi yake mzaa baba alikuwa ameshatengana na babu yake hivyo babu yake akaoa mke mwingine).

Mwanafa akiwa na miaka 3 babu yake mzaa baba alifariki hivyo mwanafa akalazimika kwenda kuishi na mama yake aliyekuwa ameolewa jijini Dar es salaam. Akiwa na umri wa miaka 5 mama yake aliachika na kuamua kuolewa tena huku safari hii akiwa na watoto wawili mwanafa na mtoto mwingine mdogo. Kwa kuogopa kwenda kwenye ndoa na mzigo mkubwa ilibidi mwanafa arudishwa Muheza Tanga safari hii kwa Bibi yake mzaa baba na si bibi wa kufikia tena. Ameishi na kusoma muheza na sasa ni mgombea ubunge wa Jimbo la Muheza kupitia CCM.

Sikiliza zaidi

 
Harmy B alipata sh ngapi?

Unaweza ukakuta Harmy kapigwa,wakati ile promo ilitumia biti yake.Maproducer sijui watamka lini kutetea haki zao,wasanii hawa heshimu kabisa ubunifu wao.
Sidhani Kama harmy B alitoka mtupu kwa jinsi alivyoshibana na hao jamaa .

Unaweza kuwa aliwauzia biti Ila jamaa watakuwa walitoa Muungwana tu maana Ni mchizi wao sana .

Kwenye huo mpungu hata msando kaonja hela
 
Sidhani Kama harmy B alitoka mtupu kwa jinsi alivyoshibana na hao jamaa .

Unaweza kuwa aliwauzia biti Ila jamaa watakuwa walitoa Muungwana tu maana Ni mchizi wao sana .

Kwenye huo mpungu hata msando kaonja hela
Kama walifanya hivyo basi ni jambo zuri.

Maproducer wana hali mbaya,Zest yule katengeneza karibia 80% ya hit songs za Aslay office yake ipo Tabata karibu na Remnant school,ila ukimtizama kachoka yaani sasa hivi ukimnunulia mzinga wa konyagi ana kunyongea biti.

C9 nimetizama intvw yake na wasafi,sasa hivi ameamua afungue duka lake la mitumba,uproducer haumlipi kafikia hatua ya kuzuia nyimbo za Isha Mashauzi na wasanii wengine.
 
Haya majamaa yana akili nyingi sana,wamekausha kwa kipindi chote hicho sasa hv ndio wanafunguka mpunga waliouingiza baada ya kuutumia wote,nadhani walijua fika kuwa wangeropoka kipindi kile mizinga ingekuwa mingi sana kutoka kwa ndugu na jamaa
 
Back
Top Bottom