Ismailsimba
Member
- May 10, 2012
- 88
- 12
Are you a Mwana FA fan what is your favorite song? Mine is 'lakini alikufa kwa ngoma'
1. Ungeniambia
2. Demu wangu wa kwanza
3. Binamu
4. Hawajui
5. Alikufa kwa ngoma
6. Mamba
Da Acha Mwana Fa alikua zamani bwana ingawa bado yupo ila namkubali na mapini ya zamani
1.Ingekua Vp
2.Mabinti
3.Tuliza Ball
4.Wanapendana
5.Binamu 100% commercial
Ninachomkubali akiamua kujisifia anajisifia hadi balaa wimbo kama 'binamu' na 'msiache kuongea', (inspekta H toka alivyojibiwa kimya hadi leo) Na akiamua kuponda ndo usiseme kama 'ungeniambia', 'bado nipo nipo'
Tafuta wimbo wa 'demu wangu wa kwanza' kama haujawahi kusikiliza jamaa alivyolalamika hm
binafsi ni mshabiki mfurukutwa na mfiligiswa wa juma mohamed mchopanga almaarufu kama jay moe toka kundi la wateule.
Ila kwa kuwa hapa anazungumziwa mwana fa na ngoma zake basi nami niseme wazi kuwa jamaa ngoma yake nayoikubali ni wanapendana akimshirikisha mtoto wa dar dully sykes.
Anaanza kwa kusema:...
Napenda vitovu ila naogopa shanga
labda bado mtoto ama labda bado mshamba
wote wanavyaa vikuku ili kuleta picha ya ngono
we subiri ipigwe ragga uone wanavyokata mauno...
nenda club siku za mabinti bure
washkaji huwa kibao utadhani wameambiwa wasilale
wote wanakwenda gym ili body zifutie warembo ukidhani una mbinu mabinti wana mitego
usiamini kuwa hawataki, ila wanaelewa kwa mikogo
wanatamani kuaproach ila wanaogopa kuitwa milupo...
DULLY...
Oooh no ona maajabu ya jana
Jack na Alice Biduka ndani ya Club walipigana eti sababu yangu mbele za watu wanazozana
Bado nasisitiza karne hii wanapendana...
FA...
Wamechizika marijali wanapenda ila mabinti wanazimika
Imeshageuka, sio kutongoza tu warembo pia hulea wakikupenda na umechoka si unanielewa...
Acha vicheche kadhaa vinavyokomalia watu
Vyenye mapenzi ya mikwanja au majina na umaarufu ambavyo ukiwa chata tu vinaonyesha udhaifu
Wapo wanaotongoza na bado ni waaminifu...
1. Ungeniambia
2. Demu wangu wa kwanza
3. Binamu
4. Hawajui
5. Alikufa kwa ngoma
6. Mamba
mi na mademu damu damu,hawajui na unanitega
We jamaa umepotelea wapi?Mimi na mademu damu damu ndo wimbo gani wa FA?wewe subiri watu wakumbuke nyimbo za zamani za kalikawe au jah kimbute ndo uchangie!
Kuna wimbo kamshirikisha LadyJay Dee unazungumzia Kifo kama sikosei title ya wimbo wenyewe inaitwa "Siku nitakapozama"Da Acha Mwana Fa alikua zamani bwana ingawa bado yupo ila namkubali na mapini ya zamani
1.Ingekua Vp
2.Mabinti
3.Tuliza Ball
4.Wanapendana
5.Binamu 100% commercial