Mwana CCM yoyote akinijibu hili nahamia CCM

Mwana CCM yoyote akinijibu hili nahamia CCM

Kwanza twambie wewe una umri gani? maana isijekuwa una miaka 18 unauliza mambo ya miaka 52 iliyopita!! tutwambia ingia darasani usome historia ya kabla na baada ya Uhuru.
Bora wewe umewaeleza maana watoto wa siku hizi ni kila kitu kugoma na kuandamana wakishakaribishwa Ikulu basi wanatulia kwa kahawa na Juice.
Mwl Nyerere (RIP) alishasema ukishindwa kuweka viraka vyako katika suruali utaanza kuilamu Serikali
Leo wanataka kila kitu na iko siku wasipoenda choo watadai ni Serikali ya CCM
Wangefuatilia simulizi za kitabu cha Odinga alivyotoka Nairobi - Dsm masaa 24 kwa mabasi ya baba yake (OTC) kuja Dsm kupata passport ili akasome tu Ujerumani leo kutoka Nairobi - Namanga - Arusha - Segera - Chalinze - Dsm ni masaa 10 tu
Hayo hawayaoni kuwa ni mabadiliko baada ya miaka 50
 
1.barabara ya lami kutoka mtwara kupitia dar hadi mwanza, kutoka tarakea - rombo arusha mombo tanga hadi dar, kutoka tunduma mbeya kupitia iringa moro hadi dar.
2. Elimu kuanzia chekechea, shule za sekondari kila kata nchi nzima hadi chuo kikuu (kila mkoa sasa una chuo kikuu sngalau kimoja, tunaelekea kuwa na vyuo vikuu vya wilaya
3.upatikanaji wa habari kupitia njia mbalimbali za upashanaji hususan mitandaoni km vile jf, televisheni zisizopungua 10, magazeti zaidi ya 20, redio nk. Hadi baadhi ta watu km nyie mnafikia kuitumia kutukana.
4. Hospitli za rufaa kia mkoa.

Yaani nyie kwa kukurupuka kha! Kweli Ndalichako ana kazi kwa hali hii!!
Mleta mada hajauliza mafanikio. Ameuliza huduma muhimu ya msingi ya kijamii tokea uhuru hadi leo ambayo ccm imeweza kuitekeleza na kuisimamia
 
Ccm inapendwa na watz kwa sababu inawahakikishia huduma bora za kijamii
 
Hilo ndio swali la msingi la kuuliza. Wewe na mimi tusaidiane mawazo tena ikiwezekana uanzishe na thread nyingine tulijadili hili.

hawataki ukweli mkuu nifanyeje sijui?
hata wakiona thread yenye kuwagusa basi woote wanakimbia
 
Hili ni swali zuri sana lakini sikulazimishi kuniamini kuwa hata mkuu wa kaya hawezi kulijibu.....na tafsiri yake ni kwamba wewe hutohamia ccm kwasababu swali haliwezi kupata majibu...
 
unazungumzia mashule yasiyo na facilities na walimu?hospitali zisizo na madawa na madaktari?India mwaenda kutali?

hakuna lolote la kujivunia,kama wilaya nyingi hazina maji ya uhakika huko vijijini je? elimu ndo hiyo ya wanafunzi kufaulu hawajui kusoma na kuandika,huku magu shule zaidi ya 4 zimefungwa kwa kukosa vyoo tu,umeme ndo kama tunavyojua.barabara nyingi ziko hoi na mifano ipo,huduma ya reli na ATC kila mmoja anajua.MAGAMBA TUAMBIENI,NI NINI MNACHOJIVUNIA?
 
Kwa kuwa hili swali limekosa majibu, basi litatumika kwenye kampeni za uchaguzi 2015, kila mgombea udiwani, ubunge na mgombea Urais kwenye kila mkutano swali hili litaulizwa na wananchi watajibu kwa mahali walipo!!!!
 
1.barabara ya lami kutoka mtwara kupitia dar hadi mwanza, kutoka tarakea - rombo arusha mombo tanga hadi dar, kutoka tunduma mbeya kupitia iringa moro hadi dar.
2. Elimu kuanzia chekechea, shule za sekondari kila kata nchi nzima hadi chuo kikuu (kila mkoa sasa una chuo kikuu sngalau kimoja, tunaelekea kuwa na vyuo vikuu vya wilaya
3.upatikanaji wa habari kupitia njia mbalimbali za upashanaji hususan mitandaoni km vile jf, televisheni zisizopungua 10, magazeti zaidi ya 20, redio nk. Hadi baadhi ta watu km nyie mnafikia kuitumia kutukana.
4. Hospitli za rufaa kia mkoa.

Mungu wangu..! kweli ccm kuna WATU. Umesahau cabbage..!
 
Ccm imeongoza nchi hii kwa zaidi ya miaka hamsini sasa, swalilangu ni hili,

Ni huduma gani yoyote ya kijamii inayopatikana hapa nchini kwa uhakika tangu mshike madaraka?.

Umasikini.
 
umeme kabla ulikua dar es salaam na makao ya mikoa michache sasa wamewekeza mtera.kidatu.pangani.na sasa gas ya songosongo umeme angalau unapatikana
afya kila mkoa na wilaya zote kuna kuna hospitali za serikali kina mama wanajifungua bure
mhimbili universty inatoa madaktari zaidi 200 kila mwaka
maji ya bomba yalikuwepo dar pekee sasa mpaka kichaka punda yanapatikana
kilimo sasa tumeanza kuondokana na jembe la mkono kwenda machine za kisasa na uzalishaji chakula umekua kiasi ya kuuza nje na tunaagiza chakula kichache sana
usafiri karibu mikoa yote sasa imeunganishwa na bara bara za lami .ambapo kabla ya uhuru barabara ilikua dar to arusha pekee
tazara m ni mradi mkubwa wa reli afrika umesaidia sana huduma rahisi za usafiri kutoka dar makambako mpaka zambia
safari za ndege nje zilikua chache sasa zipo kila siku japo ndege zetu wenywe hatujafanikiwa
elimu kabla hatukua na universiity sasa tuna uni za serikali 4 na za binafsi karibu 40 kwa pamoja zinahitimisha wanafunzi 40000 kwa mwaka huku udom ikitarajiwa kuwa chuo kikubwa zaidi afrika
michezo bado tunasua lakini tumeshawahi kuwa mabingwa wa dunia riadha na marathon na sasa tuna viwanja vizuri vya miichezo na timu kubwa kama brazil zimetembelea hapa
mawasiliano ya njia za simu yameimarika kutoka simu 20000 kabla ya uhuru mpaka simu 25m sasa hivi
radio station moja kabla sasa zaidi ya 100
hatukua na tv station kabla sasa zipo digital tv station zaid ya 20 local chanels
toka gazeti moja kwa siku mpaka daily zaidi ya 20 na weekly zaidi ya 10
viwanda sasa vipo vingi . Vya sukari pamba unga nk kabla hakuna kiwanda.
Sukari inazalishwa ya kujitosheleza nchini
huduma ya maji ni bei poa sana na imewezeshwa kwa kiasi
usalama wetu pia ni huduma moja ambayo serikali imetuhakikishia
imejenga huduma za kisasa za masoko mfano kariakoo na feri
miji yetu kama dar unaimarika kwa barabara kupanuka na sasa mradi mzuri wa kisasa wa rapid bus ni wa kujivunia.karibuni tutakuwa na fly over sehemu za ubungo na tazara
kwa mara ya kwanza huduma ya usafiri kwenda ngambo ya kigamboni itaunganishwa kwa daraja la kigamboni.usafiri baharini umeimarika kwa kujenga ferries na kule znz boti za kisasa zipo

ukweli wa mambo mengi ya msingi yamefanywa ilichobaki ni kuyaendeleza yaboreke zaidi
msingi imara tayari zimewekwa na taritibu zipo nzuri kabisa uboreshaji tu ndio jambo linalotakiwa.sheria za nchi nyingi ni kwa maslahi yetu na taifa na sasa katiba ya wana mchi wenyewe ipo kwenye mchakato
hapa bwana mkubwa kinachotakiwa kubwa ni kuacha kubweteka kudhani huduma kutoka serikalini ni bure hivo kulemaa .
Kazi ndio msingi wa maendeleo
serikali haipo kutoa free meals ukweli imejitahidi ku play their role sasa ni zamu yako na yangu kuhakisha tunapata huduma bora zaidi.huo ndio mwarubaini
mwisho nimesahau kabla hatukua na jamii forum na bloggers sasa tuna zaid ya blogs na forum 200 ambazo zinasaidia kuchangamsha serikali

hujaambiwaa utoe orodha taja huduma moja tuu iliokamilika tangu uhuru
 
Back
Top Bottom