Mwana CCM yoyote akinijibu hili nahamia CCM

Mwana CCM yoyote akinijibu hili nahamia CCM

Ccm imeongoza nchi hii kwa zaidi ya miaka hamsini sasa, swalilangu ni hili, Ni huduma gani yoyote ya kijamii inayopatikana hapa nchini kwa uhakika tangu mshike madaraka?.
si kosa lako, swali ni zuli sana ila uwezo wako wa kuelewa ndio mdogo, nakukumbuka sana kwa kitendochako cha kuwatenganisha wazazi wako kisa baba yako ni mlevi na mgonvi? dhambi hiyo bado inakutafuna. jalibu kuimage tanzania ya miaka 20 iliyopita na sasa kisha ujijibu na kukaa kimya.
 
Huduma ya kuongoza nchi hii kwa ulaghai na hila. Wamefanikiwa sana kwenye hii huduma ya kijamii.
 
Huduma ya UFISADI ndio huduma ya uhakika kabisa ambayo at least CCM wanaweza kutembea kifua mbele na kusema.."Tumethubutu na tumeweza..." kwa kweli tutakuwa wanafiki sana kama hatutawapongeza kuiboresha hii ya UFISADI.Una swali lingine@PISTILO?
 
mimi naweza kujibu nikiwa kama raia wa nchi hii.
CCM pamoja na kukopa hela nyingi nje wamejitahidi sana kwenye barabara za LAMI.
mengine zero!
wamejitahidi??????! kwahiyo huna uhakika
 
Hata Marekani hawawezi kutimiza kila kitu

Mbona swali rahisi sana, mkuu kama ulifaulu mitihani basi ulidesa, taja huduma ya kijamii, tena moja tu, ambayo CCM wamefanya ipatikane kwa uhakika kwa miaka hamsini mliyoko madarakani.

Msamehe bure tu,kuna thread hapa kuwa asilimia 77 wanaomuunga mkono mkuu ni mbumbumbu(wasiokuwa na elimu),pengine Chris Lukosi ni mmoja wao!
 
Last edited by a moderator:
Kwanza twambie wewe una umri gani? maana isijekuwa una miaka 18 unauliza mambo ya miaka 52 iliyopita!! tutwambia ingia darasani usome historia ya kabla na baada ya Uhuru.
jibu swali wewe sijakuambia uniulize swali.
 
Hata Marekani hawawezi kutimiza kila kitu
Wewe umeulizwa swali, Tutajie hata moja tu kama hakuna ni bora uandike hakuna utaeleweka sio kutuletea mambo ya Marekani kwani wenzetu yapo waliyoyamudu inagwa sio yote.
 
wamejitahidi??????! kwahiyo huna uhakika

kutokana na hali aliyoikuta JK na sasa hali ilivyo kwa kweli kwenye barabara nampa JK 75% ya utendaji mzuri wa kujenga barabara mimi ni Cdm na kadi ninayo!
ila huduma zingine hovyo hovyo kabisaaa!
 
Back
Top Bottom