Mwamposa ajitetea kuwakamua waumini 'sadaka ya kujimaliza', atoa ufafanuzi mujarabu

Tulia. Hujawahi kumsikia akitoa ufafanuzi. Ina maana huu ufafanuzi aliotoa amejichanganya mwenyewe? Wewe ni nani hadi uupinge ufafanuzi wa Mwamposa? Acha ujuaji uchwara mkuu.
Kama hujawahi kwenda kusali Kawe Kwa Mwamposa na kutoa hiyo sadaka ya kujimaliza basi wewe ndio utulie na uache ujuaji uchwara, na uache kupotosha umma.
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Mtume Boneface Mwamposa (Bulldozer) amefafanua kwa ufasaha maana ya "sadaka ya kujimaliza" inayotolewa na waumini wa kanisa lake baada ya kupokea shutuma mbalimbali kutoka kwa wananchi kwamba amekuwa akiwakamua waumini hela zote hadi wanakosa nauli ya kurudia majumbani kwao.

Ufafanuzi uliotoka ni kwamba kutoa sadaka ya kujimaliza sio kutoa fedha zote ambazo mtu amekwenda nazo kanisani. La hasha! Maana ya sadaka ya kujimaliza ni kutoa fedha zako zote ulizonazo benki na kuziwasilisha kwa mtume kama sadaka. Kwa mfano, kama una akaunti 5 kwenye benki tofauti, komba pesa zote zilizomo kwenye akaunti hizo umtolee Mungu wako. Hii ndio maana halisi ya sadaka ya kujimaliza. Yaani unajimaliza kabisa na kuanza upya!

Mtume amesema hayo zikiwa zimesalia siku chache kabla ya mkesha wa mwaka mpya unaoenda kwa kaulimbiu ya "vuka na chako" utakaofanyika kanisani kwake katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.

MAONI YANGU
Binafsi nimewahi kusimuliwa na muumini mmoja aliyetoa sadaka fedha zote alizokuwa nazo hadi nauli lakini wakati anaondoka kwa miguu kuelekea kwake Gongolamboto akitokea Kawe, mtume akamfanyia muujiza akaokota noti ya Tsh 5000 akaitumia kama nauli, yeye na wanawe wawili aliokuwa ameandamana nao.

Afadhali sasa ufafanuzi umewekwa wazi kwani waumini na wananchi walikuwa hasa hawafahamu maana ya sadaka ya kujimaliza. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mungu wa Mwamposa hajawahi kushindwa.

Nawasilisha.

Pia soma >
Sadaka ya kujimaliza ya kwa Mwamposa inatia watu umasikini
Tapeli kama matapeli wengine tu.
 
Kama hujawahi kwenda kusali Kawe Kwa Mwamposa na kutoa hiyo sadaka ya kujimaliza basi wewe ndio utulie na uache ujuaji uchwara, na uache kupotosha umma.
Mwamposa mwenyewe katoa ufafanuzi, wewe ni nani hadi upinge? Wewe ni Mwamposa?
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Mtume Boneface Mwamposa (Bulldozer) amefafanua kwa ufasaha maana ya "sadaka ya kujimaliza" inayotolewa na waumini wa kanisa lake baada ya kupokea shutuma mbalimbali kutoka kwa wananchi kwamba amekuwa akiwakamua waumini hela zote hadi wanakosa nauli ya kurudia majumbani kwao.

Ufafanuzi uliotoka ni kwamba kutoa sadaka ya kujimaliza sio kutoa fedha zote ambazo mtu amekwenda nazo kanisani. La hasha! Maana ya sadaka ya kujimaliza ni kutoa fedha zako zote ulizonazo benki na kuziwasilisha kwa mtume kama sadaka. Kwa mfano, kama una akaunti 5 kwenye benki tofauti, komba pesa zote zilizomo kwenye akaunti hizo umtolee Mungu wako. Hii ndio maana halisi ya sadaka ya kujimaliza. Yaani unajimaliza kabisa na kuanza upya!

Mtume amesema hayo zikiwa zimesalia siku chache kabla ya mkesha wa mwaka mpya unaoenda kwa kaulimbiu ya "vuka na chako" utakaofanyika kanisani kwake katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.

MAONI YANGU
Binafsi nimewahi kusimuliwa na muumini mmoja aliyetoa sadaka fedha zote alizokuwa nazo hadi nauli lakini wakati anaondoka kwa miguu kuelekea kwake Gongolamboto akitokea Kawe, mtume akamfanyia muujiza akaokota noti ya Tsh 5000 akaitumia kama nauli, yeye na wanawe wawili aliokuwa ameandamana nao.

Afadhali sasa ufafanuzi umewekwa wazi kwani waumini na wananchi walikuwa hasa hawafahamu maana ya sadaka ya kujimaliza. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mungu wa Mwamposa hajawahi kushindwa.

Nawasilisha.

Pia soma >
Sadaka ya kujimaliza ya kwa Mwamposa inatia watu umasikini
Nyie wezi tu kama vibaka wengine, tofauti mnaiba huku mmevaa suti na mmeharibu ubongo wa mnaowaibia. We kwa akili yako mtu kufunga bank accounts zote na hela kukuleteeni nyie ,fedha ambazo mtu amesevu kwa miaka kibao, na ana familia inamuhitaji, mnaona ni jambo la kawaida??? Mbona yeye Mwamposa hafungi accounts zake na azitoe kama sadaka?? Au ye hataki kwenda mbinguni? Acheni wizi.
 
Fungua uzi wa kunipinga. Vingivevyo, ukae kimya uache kupotosha umma.

Kama Mwamposa mwenyewe kasema wewe unampinga kama nani?
Uzi sifungui na kama hutaki watu wachangie basi waambieni moderator waupige pin
Vinginevyo utapokea mawazo tofauti na yako na kimya sikai mkuu,ukikasirika pasuka.

Kichwa chako itakuwa kiliyumba hukumuelewa,wafuasi wa Mwamposa waulize watakupa majibu sahihi...Kawe hujafika ila upo unapotosha watu huku mtandaoni.

Mimi siyo muumini wa Mwamposa ila hiki unachojaribu kuongea ni uongo.
 
Nyie wezi tu kama vibaka wengine, tofauti mnaiba huku mmevaa suti na mmeharibu ubongo wa mnaowaibia. We kwa akili yako mtu kufunga bank accounts zote na hela kukuleteeni nyie ,fedha ambazo mtu amesevu kwa miaka kibao, na ana familia inamuhitaji, mnaona ni jambo la kawaida??? Mbona yeye Mwamposa hafungi accounts zake na azitoe kama sadaka?? Au ye hataki kwenda mbinguni? Acheni wizi.
Mwambie huyo aelewe apunguze povu humu ndani.
 
Waafrika bado tunaamini sana miujiza.
Matatizo yako ( yetu) hayatoondoka kwa miujiza. Kaa chini umiza kichwa

Mwamposa matatizo yake yashaisha kakaa chini kaumiza kichwa.
 
Back
Top Bottom