Mwalimu wa madrasa ahukumiwa miaka 80 jela kwa kumbaka binti wa miaka 15

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Mahakama ya mkoa Mwera imemhukumu Mussa Nassibu Ismail (21) ambaye ni Mwalimu wa madrasa Kiboje wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unguja kutumikia miaka 80 jela na faini ya shilingi milioni 3 kwa kosa la kushindwa kujizuia matamanio yake na kumbaka na kumtorosha mtoto wa kike mwenye miaka 15.

Akitolea ufafanuzi wa kesi hiyo Hakimu wa Mahakama hiyo Said Hemed Khalfan chini ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali Shumbana Mbwana, amesema kuwa mtuhumiwa alifanya makosa ya kumbaka na kumtorosha mtoto huyo kwa siku mbili tofauti kati ya Oktoba 18, 2019 na Novemba 2 mwaka huo huo majira ya saa 3:00 asubuhi na saa 9:00 alasiri wakati mtoto huyo akiwa katika mazingira ya madrasa huko Kiboje.

Akisoma hukumu hiyo kwa mtuhumiwa Hakimu Khalfan amesema kuwa mtuhumiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka manne, ambapo mashtaka mawili yalikuwa ni ya kubaka na mengine ni ya utoroshaji.

Baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka Hakimu amesema kufuatia adhabu namba 6 ya mwaka 2004 ya sheria ya Zanzibar, mtuhumiwa amehukumiwa kutumikia miaka 30 kwa kila kesi moja ya kubaka na katika kesi mbili za kutorosha atatumikia miaka kumi kwa kila kesi na zote atazitumikia kwa pamoja!

Chanzo: EATV
 
miaka 15 sio mdogo, kwahiyo possibly jamaa haja baka yalikuwepo makubaliano ila kwa mujibu wa sheria huyo mtoto yupo under age kwahiyo inaonekana kama amebaka tu ..
Halafu sheria ya ndoa inaruhusu mtoto Wa miaka 15 kuolewa endapo wazazi wa pande zote wamekubaliana
 
miaka 15 sio mdogo, kwahiyo possibly jamaa haja baka yalikuwepo makubaliano ila kwa mujibu wa sheria huyo mtoto yupo under age kwahiyo inaonekana kama amebaka tu ..
Mbona hoja yako haina msimamo unaktaa na kukipinga mwenyewe
 
Mada iliyopo mezani ni ya Mwalimu wa Madrasa! Hizo habari za Mapadri na Wachungaji, zikiletwa humu jukwaani nazo tutachangia.

Ila kwa sasa habari ya mjini ni Mwalimu wa Madrasa Al Ustaadh Mussa Nassib Bin Ismail, kumbaka mtoto wa miaka 15, na kuhukumiwa kifungo cha miaka 80 jela!
😀😀😀
 
Kaonewa sababu ya tamaduni za kuletewa na wazungu, miaka 15 kiafrika ni msichana aliefikia umri wa kupatiwa mume amuhifadhi, pia miaka 80 ni mingi sana tunataka kujua sharia law inasemaje kuhusu scenario kama hiyo? sharia law tunaitumia kwenye mirathi sasa kwa nn isitumike pia kwenye kesi kama hii?
 
Kwa tz ni ngumu padri kufungwa kwa hizi kesi, hata akifungwa lazima atatoroshwa tu, sasahivi kuna padri kule moshi kakitia mimba kitoto cha form two lakini yupo kitaa anadunda tu
Ila vipi ikitokea kwa Mwalimu wa Madrasa!! 👳
 
Kwa tz ni ngumu padri kufungwa kwa hizi kesi, hata akifungwa lazima atatoroshwa tu, sasahivi kuna padri kule moshi kakitia mimba kitoto cha form two lakini yupo kitaa anadunda tu
, ikithibitishwa ana kesi ya kujibu, lkn Kama Ni fununu TU za kitaa bila hatua yoyote kuchukuliwa atazidi kudunda TU kitaa!
 
hapa ndio napochoka na mambo ya dini !

sasa mwalimu wa madrasa si umesoma dini na umeishika vizuri kiasi cha kuwafundisha wengine kabisa ?

sasa inakuaje tena ?

sisi tujifunze nini kwako ?

aya sisi ambao tuna elimu za kawaida za dini ?

NDIO MAANA NASEMAGA MBINGU NI NGUMU SANA
 
Back
Top Bottom