Mwalimu Nyerere Wamlipua Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu Nyerere Wamlipua Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rugemeleza, Dec 2, 2009.

 1. R

  Rugemeleza Verified User

  #1
  Dec 2, 2009
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu
  Nimeona habari hii katika Gazeti la Raia Mwema nikaona niwajuze.
  Rugemeleza
  Mwalimu Nyerere wamlipua Kikwete
  Mwandishi Wetu
  Disemba 2, 2009


  [​IMG]Siri za uteuzi wa mgombea urais CCM zaanikwa
  [​IMG]Butiku asema wafanyabiashara wamembana Rais
  [​IMG]Kilaini asema nchi 'inatembea bila nguo'

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) ambacho hivi karibuni kupitia Halmashauri Kuu (NEC) yake kiliunda kamati ya Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, kutafuta suluhu ya mpasuko miongoni mwa wabunge wake, kimeongezewa ukurasa mpya kwa kutangazwa kwa siri za kikao cha Halmashauri kuu (NEC) cha mwaka 1995, kilichopitisha wagombea watatu wa urais.

  Siri hiyo ilitangazwa juzi Jumatatu, kwenye kongamano la Miaka 10 ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam lililowashirikisha viongozi wa dini, wanasiasa, wanaharakati na baadhi ya wahadhiri waliotoa kauli kali ambazo zinamgusa moja kwa moja Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, aliyeanza mbio za urais mwaka 1995.

  Kwa mujibu wa siri za kikao hicho (NEC-CCM) kilichopitisha majina ya Benjamin Mkapa, Cleopa Msuya na Kikwete ili mmojawapo achaguliwe kuwa mgombea urais wa chama hicho, Mwenyekiti wa kikao, wakati huo Rais Ali Hassan Mwinyi, alizidiwa nguvu kikaoni, akazomewa katika kitendo cha utovu wa maadili kwa baadhi ya wajumbe ambao inadaiwa walikuwa wamehongwa fedha.

  Kutokana na Mwinyi kuzidiwa kikaoni baada ya kuibuka zogo wakati akielezea sababu za baadhi ya wagombea kukatwa majina yao, Mwalimu Julius Nyerere alilazimika kuingilia kati, akitoa vitisho dhidi ya waliokuwa na jazba zinazodaiwa kuchochewa na kuhongwa fedha na kuwapo kwa mtandao mahsusi wa vijana.

  Siri hizi zilivujishwa Jumatatu na aliyekuwa mjumbe katika NEC hiyo, Joseph Butiku, ambaye sasa ameweka bayana kuwa tatizo la msingi CCM na serikalini ni mtandao ambao amedai umekuwa pingamizi kwa baadhi ya viongozi waadilifu kupewa madaraka.

  "Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi Nyerere hakuwa Rais wala Mwenyekiti wa CCM, alikuwa ni Mwinyi (Ali Hassan Mwinyi). Mtandao umeanzia pale, wengi waliokuwamo serikalini sasa ni sehemu ya mtandao. Wakati ule, niliwafuata wana-CCM wawili mmoja mgombea na mwingine mgawa fedha.

  "Nilimfuata huyu mgawa fedha nikamuuliza akakataa kukiri lakini nikamwambia hizi fedha unazogawa kwa nini usiwawezeshe tu vijana kwenye miradi yao na badala yake mnazitumia kupata uongozi…hakuwa na jibu na hadi leo ananikwepa. Mwenzake alikuwa mgombea urais.

  "Huyu nilimfuata nikamwambia wenzako wanataka uwe rais lakini tatizo lako unafukuzana sana na mali. Akasema kweli. Alikuwa na fedha nyingi zilizobainika ni kutoka nchi moja.

  Nikamuuliza hizi fedha zako umemwambia Waziri Mkuu (alikuwa David Msuya). Akasema sikumwambia. Nikamweleza kamwambie na ikibidi uzirejeshe…sijui kama alifanya hivyo.

  "Sasa kikaja kikao cha NEC; Rais Mwinyi ndiye anaongoza kikao akiwa Mwenyekiti wa CCM. Akaanza kutaja majina fulani yamekatwa, alitajwa mtu fulani nusu ya kikao wakakataa, wakaanza kuimba jina fulani, kama genge hivi. Mwalimu Nyerere ambaye alialikwa kwenye kikao hicho akaomba kuzungumza.

  "Alipokubaliwa akaanza kwa kuuliza maswali matatu kutokana na zogo hilo, kwanza akauliza, ninyi ni wahuni au viongozi? Pili, je, hivi ndivyo mnavyochagua Rais? Tatu, Watanzania kama wangewaona, je, wangeamini kuwa ninyi ni viongozi wao?

  "Baada ya maswali hayo, ndipo hali ikatulia. Ilifikia hatua ikawa ni uchaguzi kati ya uchafu unaoshabikiwa na wema, akaonya kama ni hivyo (wanashikilia msimamo) twendeni kwa wananchi. Ninyi piteni huko, nasi tupite huku tuone," alifichua Butiku huku akipewa ishara na viongozi wenzake wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Dk. Salim Ahmed Salim na Jaji Warioba pamoja na Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita, kuacha kuyarejea matukio hayo bila mafanikio.

  "Mniache niseme. Maana huu ndio wakati wake. Siwezi kukaa nayo moyoni na kufa nayo haya," alisema Butiku na kuendelea; "Sasa haya yaliyojengwa yameanza kuibuka hadharani, Umoja wa Vijana CCM wanagombea majengo (mkataba wa kinyonyaji wa ujenzi, eneo la makao makuu UVCCM Dar es Salaam).

  "Nyerere aliacha nchi ikiwa moja. Leo imekuwa nchi ya vipande. Nasema hatuwezi kuishi ndani ya takataka kwa muda mrefu. Wengine wakisema wanafukuzwa kazi. Wengine wanaambiwa walitaka urais. Mtandao katika CCM uondolewe. Mliuleta wenyewe. Mkauondoe, hasa vijana, hamna mzee humo labda Kikwete.

  "Mtandao unasema fulani asipate kazi, cheo. Salim (Dk. Salim Ahmed Salim) wewe uko NEC mkaondoe mtandao. Mkishindwa kuuondoa ili sisi tuwe na uhakika wa maisha ya wajukuu zetu, tutavaa migolole na mikwaju mje mtuondoe barabarani.

  "Tujitambue kwanza sisi ni Watanzania. Haya makundi…mitandao haina maana. Msaidieni Rais (wanamtandao) acheni majungu. Wezi waliomzunguka kama wapo msaidieni awaondoe. Hatuwezi kuwa na Rais compromised, tutamsaidia kuondokana na majungu. Hatukumchagua Rais awe mtumwa wa wafanyabiashara, wafanyabiashara wamemfanya Rais mtumwa," alisema Butiku.

  Katika mjadala huo, kutokana na wazungumzaji wengi kuonyesha hatari inayozidi kulikabili taifa kwa kutokuwa na miiko ya uongozi, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam, Methodius Kilaini, alisema; "Nashukuru kama Taifa tumeanza kutambua kuwa tunatembea bila nguo." Akimaanisha udhaifu umeanza kuzungumzwa wazi na kutafutiwa ufumbuzi na Watanzania wenyewe.

  "Tumeanza kutambua tunatembea bila nguo, mwanzo ilikuwa vigumu kuambiana. Tulikuwa tunatembea bila nguo lakini hatuambiani…vijana endeleeni kupiga kelele (dhidi ya rushwa, ufisadi na dhuluma) zitasikika kuliko hata wazee.

  "Nashukuru kusikia mapendekezo ya kurejeshwa Azimio la Arusha hata kama likiwa limekarabatiwa…hatuwezi kubaki kutokuwa na chombo kinachotoa mwongozo kwa viongozi. Siku hizi watu wenye maadili mabovu wanakuwa viongozi na wanaendeleza uchafu wao huo.

  "Nyerere alikuwa pia na viongozi wasio na maadili lakini alijaribu kuwarekebisha japokuwa si wote walirekebishika. Alikuwa na wanafunzi wake kwenye uongozi ingawa wengine wamekuwa wanafunzi wabaya.

  "Siku hizi, unakuwa na viongozi wabovu serikalini, ukijaribu kuwarekebisha hata hawarekebishiki. Kama fisadi anaingia na ufisadi wake kwenye uongozi basi anauendeleza," alisema Askofu Kilaini, ambaye mantiki kwenye kauli zake hizo zilidhihirika kuzidisha utulivu wa washiriki kumsikiliza kwa makini zaidi, na kuongeza kuwa; "Tanzania ya leo ndiyo nchi pekee mtu anaingia kama mwekezaji akiwa na dola moja lakini anaondoka na dola milioni moja.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Philip Mangula alishauri Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuanza kutoa mafunzo kwa viongozi kama ilivyo nchini China ambako viongozi wanaoteuliwa au kuchaguliwa hupewa mafunzo ya miezi mitatu ili kujua wajibu wao kwa umma, akisema hiyo ndiyo sehemu muafaka ya kupokezana kile alichoita ‘vijiti.'

  Rose-Mary Nyerere mtoto wa Mwalimu Nyerere na aliyewahi kuwa Mbunge alionyeshwa kukerwa na msamiati aliouita wa sasa hivi wa upendeleo kwa tiketi aliyoiita kuwa ni "watoto wa wakubwa" akisema wao walishiriki kukata kuni Jeshi la Kujenga Taifa na shughuli nyingine ngumu akitolea mfano licha ya kuwa na kilo 47 kwa wakati huo, aliweza kubeba mzigo wa kilo 57 akiwa JKT.

  Naye, Mwanasheria mahiri Tundu Lisu alisema viongozi wengi wanashindwa kumuenzi Mwalimu Nyerere katika kipengele cha ujasiri, akitoa mifano maeneo ambayo Nyerere alionyesha ujasiri ambayo ni kumkosoa wazi wazi Rais aliyeko madarakani, kumwita Waziri Mkuu aliyeko madarakani muhuni, kupingana na wakoloni kiasi cha kufunguliwa kesi ya uchochezi.

  "Siku hizi viongozi wanaogopa gharama za ujasiri tofauti na ilivyokuwa kwa Mwalimu Nyerere," alisema Lisu.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya bia Tanzania (TBL) Arnold Kileo alisema: " CCM imekosa maadili kiasi cha kushindwa kuwanyoshea kidole viongozi wa Serikali wasio na maadili na akashauri haja ya kutathmini mfumo wa elimu nchini na hasa mitaala ambayo hubadilika kulingana na matakwa ya kiongozi aliyepo madarakani.

  Mkutano huo wa Mwalimu Nyerere, umekuja wakati hali ya kisiasa nchini ikiwa tete kiasi cha miezi tisa tu kabla ya Uchaguzi Mguu wa mwaka 2010. Maoni ya wengi ni kwamba kuna ombwe katika uongozi wa nchi na ndani ya vyama vya siasa.

  Hali hiyo imechochewa zaidi na kuwapo kwa makundi ya wazi wazi ndani ya mfumo yaliyotokana na kuwapo kwa mfululizo wa tuhuma za ufisadi dhidi ya wanasiasa, watendaji serikalini na wafanyabiashara wengine ambao ni viongozi wa juu ndani ya chama tawala. Kipindi hiki pia kimeshuhudia viongozi wa dini wakijitokeza kuikosoa Serikali.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Duu,

  Maneno mazito ya Butiku. Tusubiri Mafisadi aka vijana wa Mtandao waje wamvue nguo na sisi Watanzania tuwashangilie. Kweli viongozi wa Tz ni reflection yetu wenyewe. Nyani Ngabu, bado uko sawa ingawa naona idadi ya wanaokerwa inazidi kuwa kubwa. Taratibu watu wanaanza kusema hadharani. Muda si mrefu ataibuka mwana mapinduzi wa kweli aje awatoe jasho Mtandao.

  Mwisho wao hasa utakuja kuwa mbaya sana. Wenzao Wahindi na Waarabu watarudi kwao na tutabaki na Mipingo. Hapo ndipo tutatoa onyo la kweli.

  Sasa hivi Tanzania ni kama enzi za Zaire ila sema Mabutu wetu wanaingia kwa pesa za mataifa ya nje na hapo tunakuwa tumeshauza nchi. Wao wanauza nchi ili kupewa uongozi na sisi tunauza nchi kwa kupewa PILAU na Tshirt za njano na kijani.
   
 3. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Inafurahisha kusoma na kuona kuwa bado kuna watu wanaokerwa na tatizo tulilonalo na kuamua kusema waziwazi. Ninaona siku zote kuwa tuna tatizo kubwa la wengi waliopo kwenye siasa kuwa hapo kwa sababu ya maslahi na maopportunists. Na wengine wote kudhani kuwa kufanikiwa ni lazima kumnyenyekea mwanasiasa ambaye ameshikwa na mfanyabiashara mwizi. Bahati mbaya hili halichagui msomi au asiyesoma, wote ni watumwa wa maslahi. Ushahidi unao!

  Sina hakika kuwa vichwa vya wanaCCM wote ni vibovu kiasi cha kuamini kuwa yanayofanywa na chama chao ni kwa masilahi ya nchi hii, lakini wengi kwa sababu ya kutetea 'status quo' zao wanashabikia.

  Hata siasa za wapinzani wengi hazionyeshi kuwa zina mwelekeo wa kwenda kutafuta suluhisho kamili la haya. Inavyoonyesha wengi wanakimbilia upinzani kwa kutafuta vyeo, ambavyo mwisho wa siku vitaleta masilahi.Wanapokosa walivyovifuata huamua kuhama sehemu moja kwenda nyingine, na wengine kuhama kutoka chama tawala pia. Hii haina maana ya wote, kuna wenye dhamira za dhati, lakini zinakwamishwa na hao ambao wapo kwa sababu maalumu.

  Kuna watu ambao wanatengeneza maisha yao kwa kuharibu ya wengine. Hii ndiyo kazi yao, hawawezi kulipwa kama hawajafanya hivyo.

  Tuna kila haja ya kutafuta suluhisho la pamoja kama taifa, la kutoendelea kuweka rehani maisha yetu na ya vizazi vijavyo kwenye mikono ya wahuni wanaofanya kila siku mbinu za wizi. strategic plan ya Tanzania tunayoitaka lazima iwe kwa manufaa ya wote, na yeyote atakayeingia madarakani anatekeleza yale tunayomwambia, siyo kila baada ya miaka kadhaa kuna mtu anakuja na sera mpya.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  same old story!!! i thought kwamba taasisi ya nyerere na kikwete wako poa
   
 5. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mambo makubwa! Inaonekana joto limezidi ndani ya CCM mana mzee Butiku jambo hilo kakaanalo mda mrefu lakini mwisho dhamira imemsukuma kuyasema.

  Nawasubiri Warioba, Salim A.S, Mzee Mnduma nao waseme ukweli mana mara nyingi tumesikia wakilalamika bila kusema ukweli, mwenzao kawasaidia, wachukue hatua.
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Sasa nadhani watu wataona kwa nini Nyerere alimpigia debe Mkapa. Mkapa might have been the wrong choice but mzee kwa wakati huo ndiyo aliona anafaa kutokana na wagombea wengine waliomzunguka. Mambo kama haya ndiyo ya kuanza kujua kabla hatujamlaumu Nyerere kuwa alimpigia debe "Mr. Clean".

  The old man tried to do what he thought was right under the circumstances. Haya hata asingeingia Mkapa hali ingekua nafuu? Mbona kaondoka Mkapa mabo bado ni yale yale? History will judge Nyerere. Say what you want to say about the man but he loved his country.
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  He loved his country yes but only believe his church members as the best people among all Tanzania to lead (mbaguzi) ndio tatizo lake..that is all
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hahahaha,

  Not to exonerate Mkapa, but...

  Unaweza kufikiria Tanzania ambayo baada ya Mwinyi angeingia Kikwete?
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  this is good one!!!
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  That is your own opinion and you are entitled to it.
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Na Mwinyi naye, aliyemlift from oblivion to the presidency of the URT, alikuwa church member mwenzake pale St. Peters?
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Sipati picha mkuu. Kwanza Mwinyi mwenyewe asinge wahi kugusa kiti cha uraisi isingekua Nyerere.
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mie kwa habari za karibu nafahamu kuwa Mwinyi alikuwa akisali sana na Nyerere pale St. Peters. Tukiwa wadogo na Tumaini tulikuwa tukiwaona wakisali wote pale. Na cha zaidi, Mwinyi alikuwa akitoka kilomita kama 8 na robo kutoka Butiama. Ukichunguza sana utaona Mwinyi pia alikuwa amechonga meno ila sema baba yake alikuja hamia Zenji wakati Mwinyi akiwa mdogo. Tumaini nasikia alibeba hadi mizigo yao wakati wakihama. Wakati huo alikuwa Punda. Alipokufa akazaliwa upya kama Tumaini.
   
 14. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Hahahaaa,

  U sick son.

  Next thing you know Mwinyi ana asili ya Mwitongo! Kule Kisarawe na Zanzibar walihemea tu!
   
 15. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kweli umepatia sana, kula tano...kumbe mchonga alikuwa anagawa U-rais kwa amtakaye mwinyi hatimaye nkapa..
   
 16. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #16
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Alikuwa ana -please tu wazenj..deep inside hakuwahi kum-uplift..muda kidogo baadye uliona alivyompinga ndio akaanza kuleta church member wake nkapa kwa kupindisha democrasia.
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Dec 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Huwa sitaki kuamini uko serious! Nimejaribu hata kumuuliza mtoto wa darasa la tano anifafanulie naye akashindwa.
  Just be serious wakati mwingine.
   
 18. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #18
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mambo makubwa hayo mtoto wa tano unamuonea sana...hata wewe kama hujishughulishi huwezi kujua
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Bwahahahahahahaha.
  Basi ngoja nikalale sasa hivi nilichopenda kukiona leo kinatosha. Bwahahahahahahahahahaha.
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  kujishughulisha na nini?
   
Loading...