......Lissu aliwahi kuzungumzia issue za majaji walioteuliwa na JK......ukisoma kw amakini utaona uchambuzi wake ulikuwa una walakini fulani.......washabiki wa siasa wakabaki kushangilia!!........nakubaliana na wewe kuwa ni muhimu tuwe makini na maneno yatolewayo na watu mbali mbali..........
Moja ya jambo ambalo limeijengea Sifa sana JF ni kutokana na baadhi ya wanachama wake kuwa na uchambuzi mahiri........Umaarufu wa JF....Ni utamaduni wa kuchambua.......siku hizi kumetokea wanasiasa wengi wanataka kuivuruga JF yetu hapa....i.e. hapa pumba zinawekwa mchana kweupe na mchele vivyo hivyo.....
Kwa akili zenu, na u CDM wenu bado mnaona kabisa Lissu alikuwa sahihi kutumia lugha zile na kumwita Mwalimu Nyerere mwongo! Kwa hiyo unataka kuwaambia watanzania kuwa mwasisi wenu wa CDM ni bongo lala kwa kuwa Lissu hakutoa tusi lolote? Kweli CDM sasa siasa zimewashinda!
Kuna uvumi (binafsi naziita propaganda) kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum na Wakili Msomi mwenzangu Tundu A.M.Lissu 'amemtukana' Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 'Matusi' husika yanadaiwa kuporomoshwa na Tundu Lissu alipokuwa akiwasilisha Maoni ya Wachache katika Kamati Nambari Nne ya Bunge.
Inasemwa kuwa Tundu Lissu amemtukana na kumdhalilisha Baba wa Taifa. Propaganda hizi zinazosambaa haraka na kwa kishindo zimemkumba hadi Mzee Edwin Mtei ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA. Nikumbukacho ni kuwa Lissu alipokuwa akitetea na kufafanua Maoni ya Wachache,alitoa mifano minne akiwataja watu mbalimbali wakiwemo Mwalimu Nyerere,Profesa Issa Ghulamhussein Shivji na Dr.Harrison Mwakyembe.
Kwanza,tufahamishane hasa matusi yaliyoporomoshwa na Wakili Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere. Tukiyajua na kutambua kuwa ni matusi na dharau kweli,tuungane kumkemea Wakili Lissu na kumuonya asirudie tena. Karibuni tutaje matusi au dharau za Wakili Tundu Lissu kwa Mwalimu Nyerere. Halafu,kwanini wengine waliotajwa hawaonekani kama wametukanwa au kudhalilishwa?
Lissu hakuwa anaiwakilisha JF bali alikuwa anawakilisha maoni wa Wachache katika kamati yake kwa hiyo waliyoyaleta hapa JF ndio wanatakiwa watuletee uchambuzi wa kina ni katika maneno yapi au maandishi yepi yanayoonyesha LISSU amemtukana Nyerere (R.I.P) tofauti na hayo mtakuwa bado mnaimba ngonjera na hamjajibu kinachotakiwa kujibiwa na mleta mada.
Hayo maneno hebu kamwambie baba au mama yako hata kama yana ukweli, kisha tuletee mrejesho juu ya reaction yao.
Nyerere alikuwa muongo kweli na Lissu kabainisha hilo.
Acha kwenda nje ya mada hebu ongelea maneno ya matusi yaliyotolewa na tundu na kwani nyerere hawezi kuwa mwongo au unadhani yale yote yaliyotolewa naye yalikuwa ya kweli.???
Thibitisha pasipo shaka hapa jukwaani, ni kweli kwamba ktk maisha ya uongozi wa mwalimu hakuwahi kusema uongo?
Nyerere alikua kiongozi mzuri, Lakini alikuwa na mapungufu jamani hakuwa Mungu alikuwa na mapungufu mengi tu ukiachana na huo uwongo,
Kwa hiyo kama alidanganya asiitwe mwongo kisa.
Alidanganya nini? Mnatakiwa kuthibitisha, siyo kuongea ongea tu kama Lissu! Yaani chuki zenu za CCM mnazifanya Lissu na CDM members hata wakiongea utumbo mnaona sawa tu! Hamna tofauti na waliomtukama Jaji Warioba! Waanasiasa watu wa ajabu sana, na nyie mnashangilia kama mazuzu kisa kaongea mtu wa CDM, au CCM walivyoshangilia kwa kuwa kaongea Kikwete! Ni Mpuuzi tu ndo anaona hii ni sawa!