Sawia Mkuu! Mbona hata Manabii/Mitume etc wanatukanywa kwenye Mihadhara na Mahubiri na watu hawawashupalii kama Lissu.Nyerere ni Mungu?
ukweli nyerere walikuwa muongo na mnafiki, amedhulumu sana, sasa mkiambiwa mnaona katukanwa, mbona wengine mnawatukana kwa kukashifu .....?
Naungana na wewe, huyu mzee alijiuzulu nyazifa zake wakati wengi wetu tukiwa mashuleni, hatukujua ni nini hasa kilimpata hadi kufikia uamuzi huo, ala kumbe kosa lake kubwa ilikuwa kuhoji uhalali & mfumo wa muungano huu huu unaojadiliwa ndani ya Bunge la katiba!!Tusi kubwa alilotukana Lissu, ni kuuliza uhalali wa kumuweka kizuizini Mzee Jumbe kule Mjimwema.
Petro E. Mselewa kujua matusi ni mpaka mama yako akuambie kuwa wewe baba yako ni aliyekuwa mchunga ng'ombe wenu.
Ni vigumu mno kuutetea hoja isiyo na haki ili ipate haki stahiki na ikubalike. ni kweli ni kazi ngumu mno ndiyo maana mara wanahamia kwenye matumizi, ulinzi na jeshi, vita nkHao serikali mbili wameshindwa hoja ya kwa nini kusiwe na na serikali tatu,wana tapa tapa.Serikali tatu..Period........
Siko tayari kutukana, ila jua kua maneno aliyoyasema hakustahili kuyasema dhidi ya Nyerere.
Kuna uvumi (binafsi naziita propaganda) kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum na Wakili Msomi mwenzangu Tundu A.M.Lissu 'amemtukana' Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 'Matusi' husika yanadaiwa kuporomoshwa na Tundu Lissu alipokuwa akiwasilisha Maoni ya Wachache katika Kamati Nambari Nne ya Bunge.
Inasemwa kuwa Tundu Lissu amemtukana na kumdhalilisha Baba wa Taifa. Propaganda hizi zinazosambaa haraka na kwa kishindo zimemkumba hadi Mzee Edwin Mtei ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA. Nikumbukacho ni kuwa Lissu alipokuwa akitetea na kufafanua Maoni ya Wachache,alitoa mifano minne akiwataja watu mbalimbali wakiwemo Mwalimu Nyerere,Profesa Issa Ghulamhussein Shivji na Dr.Harrison Mwakyembe.
Kwanza,tufahamishane hasa matusi yaliyoporomoshwa na Wakili Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere. Tukiyajua na kutambua kuwa ni matusi na dharau kweli,tuungane kumkemea Wakili Lissu na kumuonya asirudie tena. Karibuni tutaje matusi au dharau za Wakili Tundu Lissu kwa Mwalimu Nyerere. Halafu,kwanini wengine waliotajwa hawaonekani kama wametukanwa au kudhalilishwa?
......Lissu aliwahi kuzungumzia issue za majaji walioteuliwa na JK......ukisoma kw amakini utaona uchambuzi wake ulikuwa una walakini fulani.......washabiki wa siasa wakabaki kushangilia!!........nakubaliana na wewe kuwa ni muhimu tuwe makini na maneno yatolewayo na watu mbali mbali..........
Moja ya jambo ambalo limeijengea Sifa sana JF ni kutokana na baadhi ya wanachama wake kuwa na uchambuzi mahiri........Umaarufu wa JF....Ni utamaduni wa kuchambua.......siku hizi kumetokea wanasiasa wengi wanataka kuivuruga JF yetu hapa....i.e. hapa pumba zinawekwa mchana kweupe na mchele vivyo hivyo.....
Ndipo tunapokosa direction kama taifa iwapo sifa ya kisiasa ni kumwaga matusi tu.
Maneno ni upanga wenye ncha mbili zinayokata pande zote. Maneno yako yanaweza kukufanya uwe na hatia na vile vile yanaweza kukuondoa kwenye tuhuma za hatia. Yote inategemea na jinsi unavyotumia maneno yako.
Sidhani kama Lisu alitumia maneno yake vizuri, na ndiyo maana nimekuwa na wasiwasi na uhakika wa maneno yote aliyowahi kutuambia kuhusu Zitto na Kitila huko nyuma.
Mama kumbe una mitusi ya nguoni sikuamini tena
Siko tayari kutukana, ila jua kua maneno aliyoyasema hakustahili kuyasema dhidi ya Nyerere.
Kwa akili zenu, na u CDM wenu bado mnaona kabisa Lissu alikuwa sahihi kutumia lugha zile na kumwita Mwalimu Nyerere mwongo! Kwa hiyo unataka kuwaambia watanzania kuwa mwasisi wenu wa CDM ni bongo lala kwa kuwa Lissu hakutoa tusi lolote? Kweli CDM sasa siasa zimewashinda!