Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%

Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%

Hawa walimu ni kati ya viumbe wa ajabu kabisa.

Haiwezekani mtu alilie haki ya kuwafanyia ukatili wanafunzi.

Sidhani kama kuna hiyo haki kwenye katiba ya nchi yoyote duniani.

Haki ya kuchapa!!! Haha..

Sent using Jamii Forums mobile app
Fimbo siyo ukatili.Ukatili unatokana na Hali ya mtoa adhabu.Akitoa adhabu kikatili na Bila kuzingatia Sheria na Hali ya mtoto na kosa ndiyo inakuwa ukatili.Lkn kusema fimbo ni ukatili Basi hata mkuu asingeruhusiwa kufanya ukatili.Mimi ningependa fimbo zisiwepo kabisa.Lakini tuweke kitu mbadala wa kurekebisha tabia za watoto.Bila kuweka kitu mbadala Basi nadhani tutakuwa hatuna Nia njema ni kizazi kijacho.Pia mazingira ya shule yaboreshwe.Shule Sasa hivi zimedharaulika.Shule nyingi zipo kama mazizi ya Ng'ombe.Shule za Sekondari zenye sakafu ya sementi nadhani huenda hazifiki hata asilimia 10.
Shule ambazo matundu ya vyoo yanatosheleza hazifiki hata asilimia kumi.Shule ambazo vyumba vya madarasa vinatosha huenda hazifiki hata asilimia kumi.Idadi ya walimu ni changamoto pia.
Mazingira ya shule yamefanya watoto waone kama shule hazina maana yeyote.Wanaona ni kijiwe tu.
Serikali Kila siku wanakimbilia kutafuta wa kumpa lawama.Na wananchi tunaimba mashairi ya serikali Bila kujijua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna mwalimu mwenye njaa ya kutandika viboko nadhani ndiye atalilia kutandika watoto. Hakuna mwalim mwenye njaa ya kutandika mitoto yenu. Ila, miaka 2 tu ijayo, wewe unayedhihaki humu, ndio utakuwa wa kwanza kuja lialia humu humu. Acheni dhihaka kwa waalimu. Mtu aliyekutoa tongo tongo ukajua kuumba herufi a leo unamdhihaki?? Laana zingine zitatupatia hapa hapa.
Nazidi kusisitiza kwamba; Hakuna mwalimu mwenye njaa ya kutandika mtoto wa mtu fimbo. Ila, anatamani mwanao awe raia mzuri na mwenye utaalam
Shida ni kuwa Kila mtu anadhani ualimu ni kazi ya Kila mtu.Hata yeye anajiona.mwalimu.Yaani anakufundisha wewe uliyesomea ualimu.Mtu kama huyu mwenye mtizamo huu angewashauri serikali kuwa walimu usisomewe Ila yeyote tu afundishe.
Walimu tufanye Kwa kadili ya uwezo wetu Ila Yale yaliyo nje ya uwezo wetu nadhani hatutakiwi kuhangaika Nayo.Mie nina Darasa langu Lina wanafunzi karibu 200 nimechagua wanafunzi 30 wenye discipline ambao hawasukumwi Hawa Kila siku nipo nao.Huwa nahakikisha napata muda wa ziada wa kuwapa home work wanafanya na ninawasahishia.Siwezi jitesa na wanafunzi wote wakati almost 170 ni wakorofi sitaki kutumia muda mwingi kufanya counselling Kwa mtu ambaye ukiongea naye unajua kabisa toka Nyumbani Kwao wamemtuma shule akafeli na akasababishe wengine wafeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wa kufa atakufa tu mkuu.! Mwl isiwe kisingizio wangapi ulio wahi wasikia wameuwawa na walimu?
Mwalimu aweza kuwa mzazi kuliko hata wewe mwalimu anakaa na mwanao kwa miaka saba na huenda zaidi ya masaa nane kila siku anamfahamu mwanao mara elfu kadhaa.
Binti anavunja ungo kwa mara ya kwanza anayejua hilo ni mwalimu wake, kijana ana barehe anayelitambua hilo mwanzo ni mwalimu wake, leo hii unamuona muuaji ila wewe na visaa viwili vyako ndio mzazi na mlezi mwema.. muwe na shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko Iringa abiria katwangwa risasi na Polisi nasubiri tamko la Waziri kuwa polisi wasitembee na bunduki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote uliyoyaeleza hpo hayampi uhalali mwalimu wa kushika gongo na kumpiga mwanafunzi kichwani mpaka kumuua!! Naona unachukulia kifo simpo sana angekuwa mwanao ndyo ameuliwa kwa staili hyo ungeandika hyo comment km ulivyoiandika!!?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mwalimu Huwa anashika gongo na kumpiga mtoto kichwani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ni kuwa Kila mtu anadhani ualimu ni kazi ya Kila mtu.Hata yeye anajiona.mwalimu.Yaani anakufundisha wewe uliyesomea ualimu.Mtu kama huyu mwenye mtizamo huu angewashauri serikali kuwa walimu usisomewe Ila yeyote tu afundishe.
Walimu tufanye Kwa kadili ya uwezo wetu Ila Yale yaliyo nje ya uwezo wetu nadhani hatutakiwi kuhangaika Nayo.Mie nina Darasa langu Lina wanafunzi karibu 200 nimechagua wanafunzi 30 wenye discipline ambao hawasukumwi Hawa Kila siku nipo nao.Huwa nahakikisha napata muda wa ziada wa kuwapa home work wanafanya na ninawasahishia.Siwezi jitesa na wanafunzi wote wakati almost 170 ni wakorofi sitaki kutumia muda mwingi kufanya counselling Kwa mtu ambaye ukiongea naye unajua kabisa toka Nyumbani Kwao wamemtuma shule akafeli na akasababishe wengine wafeli

Sent using Jamii Forums mobile app
safi ukiendelea hivyo utafika mbali.

acha hao waalimu wengine wasiojitambua waisome namba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafunzi bila viboko ni kitu inawezekana as long as wazazi watakua mstari wa mbele kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni pia kushirikiana na walimu ili kusaidiana katika malezi ya mtoto. Ila cha ajabu wazazi wamekua wako nyuma sana kiasi Cha kuishia kuwa watu wa lawama Tu inapotokea mtoto kafeli au kuwa na tabia zisizoendana na maadili....

ELIMU BILA ADHABU VIBOKO INAWEZEKANA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ya bila viboko inawezekana kabisa mbeya vijijini kwenye shule xxx ya private mmiliki wake kapiga marufuku viboko shleni kwake mtoto kuchapwa ni mpaka atoe ruhusa yeye na maisha yanaenda vizuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Private zilizo nyingi watoto wanatoka familia bora,au za kati,ambao kwa kiasi kikubwa wanajua umuhimu wa elimu.

Pia kwa ada wanayolipa wakiambiqa habari ya kufukuzwa shule kwa utovu wa nidhamu,wengi wanalia na kusaga meno kuomba msamaha pasipo viboko.

Shule za umma kwa sasa asilimia kubwa ya watoto wanatoka familia duni sana,wengi wao hata huo umuhimu wa shule hawauoni,wanalazimishwa kwa kiasi kikubwa na walimu wao kuhudhuria shule!

Mbaya zaidi kuna wanafunzi ambao kufukuzwa shule kwao ni fursa ya kwenda kufanya mambo yao binafsi,HAWAUMII!

Kwa ushauri alioutoa mdau hapo juu,kama kweli walimu wataamua kuutekeleza,hakika wachache walioko private (wenye uwezo kiuchumi) wataendelea kufaidi mema ya nchi,lakini walio wengi (st.kayumba) watapotea sana!!!
Wengi wanatoka familia maskini huanza kufanya juhudi binafsi na kupenda shule,wanapovuka O-level,(uelewa wao hufunguka na kutambua umuhimu wa shule)

ANDIKO HILO NI HATARI KWA TAIFA KULIKO TUNAVYOWEZA KUDHANI!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu sidhani kama kuzira ni jambo jema as long tulishachagua kuwa walimu.Tutekeleze wajibu wetu Kwa mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu.
Mimi primary nimechapwa lakini sikumbuki hata mwalimu aliyenichapa,ila moja tu ndio nakumbuka Kwa vile nilichapwa Kwa hila .
Ila kwa watoto wa Sasa walimu be careful

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Private zilizo nyingi watoto wanatoka familia bora,au za kati,ambao kwa kiasi kikubwa wanajua umuhimu wa elimu.

Pia kwa ada wanayolipa wakiambiqa habari ya kufukuzwa shule kwa utovu wa nidhamu,wengi wanalia na kusaga meno kuomba msamaha pasipo viboko.

Shule za umma kwa sasa asilimia kubwa ya watoto wanatoka familia duni sana,wengi wao hata huo umuhimu wa shule hawauoni,wanalazimishwa kwa kiasi kikubwa na walimu wao kuhudhuria shule!

Mbaya zaidi kuna wanafunzi ambao kufukuzwa shule kwao ni fursa ya kwenda kufanya mambo yao binafsi,HAWAUMII!

Kwa ushauri alioutoa mdau hapo juu,kama kweli walimu wataamua kuutekeleza,hakika wachache walioko private (wenye uwezo kiuchumi) wataendelea kufaidi mema ya nchi,lakini walio wengi (st.kayumba) watapotea sana!!!
Wengi wanatoka familia maskini huanza kufanya juhudi binafsi na kupenda shule,wanapovuka O-level,(uelewa wao hufunguka na kutambua umuhimu wa shule)

ANDIKO HILO NI HATARI KWA TAIFA KULIKO TUNAVYOWEZA KUDHANI!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoto wa Manzese Kiwalani Chamwino anataka apate treatment kama ya Mtoto wa Rugemalira

Watu wajiulize shule za Advance zina fimbo kama O level japo walimu ni wale wale?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naskia ulaya hakuna viboko, na maisha na maisha yanaenda kama kawa, na sisi ndio tunategemea wataalamu wao. Tumieni adhabu mbadala acheni kung'ang'ania mifimbo ambayo sheria za matumizi yake tu mmeshindwa kuzielewa kwa zaidi ya miaka 50 sasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom