Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%

Kwa maana iliyojificha unasapoti walimu kuchapa watoto mpk kuwaua?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wa kufa atakufa tu mkuu.! Mwl isiwe kisingizio wangapi ulio wahi wasikia wameuwawa na walimu?
Mwalimu aweza kuwa mzazi kuliko hata wewe mwalimu anakaa na mwanao kwa miaka saba na huenda zaidi ya masaa nane kila siku anamfahamu mwanao mara elfu kadhaa.
Binti anavunja ungo kwa mara ya kwanza anayejua hilo ni mwalimu wake, kijana ana barehe anayelitambua hilo mwanzo ni mwalimu wake, leo hii unamuona muuaji ila wewe na visaa viwili vyako ndio mzazi na mlezi mwema.. muwe na shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna mwalimu mwenye njaa ya kutandika viboko nadhani ndiye atalilia kutandika watoto. Hakuna mwalim mwenye njaa ya kutandika mitoto yenu. Ila, miaka 2 tu ijayo, wewe unayedhihaki humu, ndio utakuwa wa kwanza kuja lialia humu humu. Acheni dhihaka kwa waalimu. Mtu aliyekutoa tongo tongo ukajua kuumba herufi a leo unamdhihaki?? Laana zingine zitatupatia hapa hapa.
Nazidi kusisitiza kwamba; Hakuna mwalimu mwenye njaa ya kutandika mtoto wa mtu fimbo. Ila, anatamani mwanao awe raia mzuri na mwenye utaalam
Acha porojo wewe...walimu wamemtandika mtoto mpaka wamemuua mtoto still bado unaunga mkono uuaji?

Nadhani baada ya miaka miwili we ndyo utalia kwa kukubali mtoto wako atandikwe km ng'ombe mpaka wamuue!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wa kufa atakufa tu mkuu.! Mwl isiwe kisingizio wangapi ulio wahi wasikia wameuwawa na walimu?
Mwalimu aweza kuwa mzazi kuliko hata wewe mwalimu anakaa na mwanao kwa miaka saba na huenda zaidi ya masaa nane kila siku anamfahamu mwanao mara elfu kadhaa.
Binti anavunja ungo kwa mara ya kwanza anayejua hilo ni mwalimu wake, kijana ana barehe anayelitambua hilo mwanzo ni mwalimu wake, leo hii unamuona muuaji ila wewe na visaa viwili vyako ndio mzazi na mlezi mwema.. muwe na shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yote uliyoyaeleza hpo hayampi uhalali mwalimu wa kushika gongo na kumpiga mwanafunzi kichwani mpaka kumuua!! Naona unachukulia kifo simpo sana angekuwa mwanao ndyo ameuliwa kwa staili hyo ungeandika hyo comment km ulivyoiandika!!?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%
Fuatilia mwongozo huu: Mwalimu hakikisha umefika shule muda husika, simamia usafi na kama wanafunzi hawaonyeshi kushiriki kufanya usafi, tafadhali usishike kiboko. Mwalimu kumbuka muda wa vipindi ukifika hata kama mazingira ya shule ni machafu, wanafunzi waingie darasani tayari kwa masomo. Mwalimu fundisha kipindi chako kama mwongozo unavyoonesha, tafadhali usiwafuatilie wanafunzi wasioandika, kwani inaweza kuhamasisha hisia za kutoa adhabu ili kumjenga mwanafunzi husika. Mwalimu, daftari zikikusanywa kwa ajili ya kusahihisha, tafadhali usifuatilie kubaini wanafunzi wasiokusanya daftari kwani kubaini kwako kunaweza kupelekea kuwepo na mazingira yenye kuchochea adhabu.
Mwalimu wakati utakapoita majina, zingatia kuwa wale waliopo darasani kwa wakati huo ndiyo wanaokuhusu, hitaji lako la kutaka kujua mwanafunzi X ana tatizo gani la kutokuja shuleni linaweza kupelekea mazingira yatakayo chochea adhabu, kwani wanafunzi wenzie wakati mwingine watakupa jibu kuwa mwanafunzi X yupo maeneo ya chooni anacheza tu, hivyo jibu ili linaweza kupelekea mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu, mara upatapo kesi za mwanafunzi X kuwa amepigana darasani au kutoa lugha chafu, tafadhali tumia neno moja tu kuwa "LUGHA ZA MATUSI SI NZURI " kisha mruhusu kurudi darasani ili kuepusha mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu mzazi akikuletea kesi ya mtoto wake kuhusu tabia za nyumbani na hata mwenendo mbovu wa maendeleo yake darasani, tafadhali mueleze mzazi kuwa amalizane na mwanaye kwa namna inayofaa. Mwalimu wangu ukifuata muongozo huu, shutuma na jazba za wana wa nchi hii utaziepuka pia itakusaidia japo kurudisha mwili wako uliopukutika kwa kufuatilia watoto wasiokuhusu, nakutakia kazi njema mwalimu wangu.
U-local wako wa kuzaliwa sehemu moja na kukulia sehemu ile ile ndiyo unakufanya ufukirie viboko ndiyo njia pekee ya kumfanya mwanafunzi awe na tabia nzuri. Ulaya watoto hawachapwi na wanapokuwa wanakuwa na heshima na ni waaminifu. Bongo mnachapa viboko na watoto wakimaliza ndiyo wanakuwa wezi, waongo na waasherati wakubwa!
 
Kama kuna mwalimu mwenye njaa ya kutandika viboko nadhani ndiye atalilia kutandika watoto. Hakuna mwalim mwenye njaa ya kutandika mitoto yenu. Ila, miaka 2 tu ijayo, wewe unayedhihaki humu, ndio utakuwa wa kwanza kuja lialia humu humu. Acheni dhihaka kwa waalimu. Mtu aliyekutoa tongo tongo ukajua kuumba herufi a leo unamdhihaki?? Laana zingine zitatupatia hapa hapa.
Nazidi kusisitiza kwamba; Hakuna mwalimu mwenye njaa ya kutandika mtoto wa mtu fimbo. Ila, anatamani mwanao awe raia mzuri na mwenye utaalam
Maneno hayawezi kubadili nafasi ya fimbo?

Kwanini msijenge mawasiliano mazuri pande zote tatu(mzazi,mwanafunzi na mwalimu) kwenye kufuatilia nyendo za mwanafunzi msumbufu?

Umejiuliza pia kwanini unaona kiboko ndio njia sahihi zaidi kumuelimisha mwanafunzi?

#mtoto umleavyo ndivyo akuavyo,wafanyeni chekechea majaribio kwa kutowachapa tuone wakifika darasa la tatu kama ni pumba au mchele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%
Fuatilia mwongozo huu: Mwalimu hakikisha umefika shule muda husika, simamia usafi na kama wanafunzi hawaonyeshi kushiriki kufanya usafi, tafadhali usishike kiboko. Mwalimu kumbuka muda wa vipindi ukifika hata kama mazingira ya shule ni machafu, wanafunzi waingie darasani tayari kwa masomo. Mwalimu fundisha kipindi chako kama mwongozo unavyoonesha, tafadhali usiwafuatilie wanafunzi wasioandika, kwani inaweza kuhamasisha hisia za kutoa adhabu ili kumjenga mwanafunzi husika. Mwalimu, daftari zikikusanywa kwa ajili ya kusahihisha, tafadhali usifuatilie kubaini wanafunzi wasiokusanya daftari kwani kubaini kwako kunaweza kupelekea kuwepo na mazingira yenye kuchochea adhabu.
Mwalimu wakati utakapoita majina, zingatia kuwa wale waliopo darasani kwa wakati huo ndiyo wanaokuhusu, hitaji lako la kutaka kujua mwanafunzi X ana tatizo gani la kutokuja shuleni linaweza kupelekea mazingira yatakayo chochea adhabu, kwani wanafunzi wenzie wakati mwingine watakupa jibu kuwa mwanafunzi X yupo maeneo ya chooni anacheza tu, hivyo jibu ili linaweza kupelekea mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu, mara upatapo kesi za mwanafunzi X kuwa amepigana darasani au kutoa lugha chafu, tafadhali tumia neno moja tu kuwa "LUGHA ZA MATUSI SI NZURI " kisha mruhusu kurudi darasani ili kuepusha mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu mzazi akikuletea kesi ya mtoto wake kuhusu tabia za nyumbani na hata mwenendo mbovu wa maendeleo yake darasani, tafadhali mueleze mzazi kuwa amalizane na mwanaye kwa namna inayofaa. Mwalimu wangu ukifuata muongozo huu, shutuma na jazba za wana wa nchi hii utaziepuka pia itakusaidia japo kurudisha mwili wako uliopukutika kwa kufuatilia watoto wasiokuhusu, nakutakia kazi njema mwalimu wangu.
Hahaah unataka uitwe na madogo Disminder
 
Umejiuliza pia kwanini unaona kiboko ndio njia sahihi zaidi kumuelimisha mwanafunzi?

Sijasema kuwa kiboko ndio njia sahihi ya kumuelimisha mtoto. Je, hakuna mtoto anayemaliza mwaka bila kuchapwa shuleni?? Nimesema, fimbo zikiondolewa shuleni, nidhamu itatoweka
 
Kuna shule (sitazitaja hapa) walimu ni marufuku hawachapi fimbo na wanafunzi wana nidhamu tu, ukizingua unapigwa suspension au kufukuzwa shule
 
Sijasema kuwa kiboko ndio njia sahihi ya kumuelimisha mtoto. Je, hakuna mtoto anayemaliza mwaka bila kuchapwa shuleni?? Nimesema, fimbo zikiondolewa shuleni, nidhamu itatoweka
Unajitahidi sana kupotosha. HAUTAFANIKIWA.
IMG_20180903_000639.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom