Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%

Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%

Hili swali ni kutaka kujibu swali aliloulizwa daktari wakati wewe ni engineer. Hata siku moja kama sio mwalimu hauwezi kujua umhimu wa viboko. Najua utakimbilia kusema mbona wazungu hawachapi na watoto wanafauli. Ukisahau kuwa mzungu anafundisha watoto 15 hadi 20 ila mwalimu wa kitanzania ana watoto 300 kwa siku. Ukijumlisha mshahara mdogo, ukijumlisha na madeni, jumlisha na mazingira mabaya kazini ne mengine mengi tu. Japo mm sio mwalimu ila nimesomea ualimu pia, viboko haviepukiki mashuleni

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kweli kama watafanya hivyo walimu

Sure wanafunzi watauliwa academically (zero unavoidable)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%
Fuatilia mwongozo huu: Mwalimu hakikisha umefika shule muda husika, simamia usafi na kama wanafunzi hawaonyeshi kushiriki kufanya usafi, tafadhali usishike kiboko. Mwalimu kumbuka muda wa vipindi ukifika hata kama mazingira ya shule ni machafu, wanafunzi waingie darasani tayari kwa masomo. Mwalimu fundisha kipindi chako kama mwongozo unavyoonesha, tafadhali usiwafuatilie wanafunzi wasioandika, kwani inaweza kuhamasisha hisia za kutoa adhabu ili kumjenga mwanafunzi husika. Mwalimu, daftari zikikusanywa kwa ajili ya kusahihisha, tafadhali usifuatilie kubaini wanafunzi wasiokusanya daftari kwani kubaini kwako kunaweza kupelekea kuwepo na mazingira yenye kuchochea adhabu.
Mwalimu wakati utakapoita majina, zingatia kuwa wale waliopo darasani kwa wakati huo ndiyo wanaokuhusu, hitaji lako la kutaka kujua mwanafunzi X ana tatizo gani la kutokuja shuleni linaweza kupelekea mazingira yatakayo chochea adhabu, kwani wanafunzi wenzie wakati mwingine watakupa jibu kuwa mwanafunzi X yupo maeneo ya chooni anacheza tu, hivyo jibu ili linaweza kupelekea mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu, mara upatapo kesi za mwanafunzi X kuwa amepigana darasani au kutoa lugha chafu, tafadhali tumia neno moja tu kuwa "LUGHA ZA MATUSI SI NZURI " kisha mruhusu kurudi darasani ili kuepusha mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu mzazi akikuletea kesi ya mtoto wake kuhusu tabia za nyumbani na hata mwenendo mbovu wa maendeleo yake darasani, tafadhali mueleze mzazi kuwa amalizane na mwanaye kwa namna inayofaa. Mwalimu wangu ukifuata muongozo huu, shutuma na jazba za wana wa nchi hii utaziepuka pia itakusaidia japo kurudisha mwili wako uliopukutika kwa kufuatilia watoto wasiokuhusu, nakutakia kazi njema mwalimu wangu.
Buhahahahahahahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna mwalimu mwenye njaa ya kutandika viboko nadhani ndiye atalilia kutandika watoto. Hakuna mwalim mwenye njaa ya kutandika mitoto yenu. Ila, miaka 2 tu ijayo, wewe unayedhihaki humu, ndio utakuwa wa kwanza kuja lialia humu humu. Acheni dhihaka kwa waalimu. Mtu aliyekutoa tongo tongo ukajua kuumba herufi a leo unamdhihaki?? Laana zingine zitatupatia hapa hapa.
Nazidi kusisitiza kwamba; Hakuna mwalimu mwenye njaa ya kutandika mtoto wa mtu fimbo. Ila, anatamani mwanao awe raia mzuri na mwenye utaalam
Na katika mafunzo ya ualimu hakuna mahali panasema mtoto achapwe viboko. Zaidi mwalimu ni mwanadamu anakosea kama walimu au mwalimu huyo alivyokosea. Tatizo letu tumezidisha sana kusema kana kwamba walimu sasa ni wauaji. Mbona sheria ya nchi haijambagua mwalimu? Cha ajabu kosa analofanya mwalimu ni chuo cha kujifunzia siasa. Na wengi hoja zenu nyingi zinakuwa na double standard.
Mjadala huo pamoja na sheria kuchukua mkondo wake bado wengi hapa wanaona haitoshi. Toeni na suluhisho sio malalamiko tu.
 
kwani watoto wa shule za english medium wanapigwa kama wetu kwani wao wana nidhamu mbaya kuliko wa st kayumba viboko havina umuhimu na ni ukatili usiona maana.
 
kwani watoto wa shule za english medium wanapigwa kama wetu kwani wao wana nidhamu mbaya kuliko wa st kayumba viboko havina umuhimu na ni ukatili usiona maana.
Ushawahi fika huko au unaongea tu?

Tofautisha baina ya private na public school

Private schools mwanafunz akileta ujinga anatolewa (kufukuzwa) hawana muda na mtoto mwenye matatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwani watoto wa shule za english medium wanapigwa kama wetu kwani wao wana nidhamu mbaya kuliko wa st kayumba viboko havina umuhimu na ni ukatili usiona maana.
Mwalimu wa private anafundisha watoto wangapi kwa siku. Sidhani kama wanazidi 100 ila primary utakuta ana vipindi 5 kwa siku na kila darasa lina watoto 150

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushawahi fika huko au unaongea tu?

Tofautisha baina ya private na public school

Private schools mwanafunz akileta ujinga anatolewa (kufukuzwa) hawana muda na mtoto mwenye matatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
tuna watoto watatu wanasoma huko hawachapwi na wana nidhamu na peformance nzuri huku kayumba kuna shida gani mpaka watu wajipe haki ya kuwapiga watoto kama nyoka kazi ya mwalimu ni kufundisha.
 
Hiyo ya bila viboko inawezekana kabisa mbeya vijijini kwenye shule xxx ya private mmiliki wake kapiga marufuku viboko shleni kwake mtoto kuchapwa ni mpaka atoe ruhusa yeye na maisha yanaenda vizuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe ni private!!!! Actually kuna shule za private famous one ambapo academically and morally ziko good na wazaz wanazifaamu shule hizo kuwa ziko vizur.

Thus why mkuu wa shule mwenyewe ainaiamini shule yake na anawaanimi walimu wake pia.

Mtoto anawahi fika shule.
Niadhamu yake iko good.
Mtoto yuko panctual katika mambo yote akiwa shule FIMBO YANINI SASA KWAKE??

Nenda ktk SHULE za SERIKALI two Elimu bure daaaaah
Wanafunzi nidhamu ovyo, mwalimu ampe kazi HAJAFANYA, Andika Notes HAJAANDIKA, Mwanafunzi anakula bangi, Mara wiki, mwezi hajafika shule

Adhabu gani ihusike hapo????????????????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tuna watoto watatu wanasoma huko hawachapwi na wana nidhamu na peformance nzuri huku kayumba kuna shida gani mpaka watu wajipe haki ya kuwapiga watoto kama nyoka kazi ya mwalimu ni kufundisha.
Looh we hujuw kabsa

Huwez sema mwalimu unamsomesha mtoto akiwa na nidhamu mbaya hata siku 1 hawez faulu

Kingine syo kuwa walimu wajipatia haki ya kuwachapa wanafunzi,

Ieeleweke wazi hakuna mwalimu mjinga na alyepata kichaa cha kumchapa mwanafunzi

Shida ni kwamba wengi wao nidhamu "F" mwalimu anakuwa mzazi wa kwanza na mzazi wa pili so how comes?????


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushawahi fika huko au unaongea tu?

Tofautisha baina ya private na public school

Private schools mwanafunz akileta ujinga anatolewa (kufukuzwa) hawana muda na mtoto mwenye matatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Embu wambie wale wasomao shule za seminary tena za RC anavyokuwa na nidhamu
hata wakija rikizo utawapenda, hivi kule viboko vipi.[emoji44]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom